28/06/2018

VODACOM TANZANIA YAWAZAWADIA MAWAKALA NA WATUMIAJI WA MPESA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI

Vodacom Tanzania, kampuni inayoongoza ya mawasiliano ya simu leo imekuwa na hafla ya kuwatambua na kuwazawadia wateja, mawakala na wauzaji wanaotumia mfumo wa M_PESA Mkoa wa Mbeya. Hafla hii iliyofanyika jijini Mbeya ni muendelezo wa kampeni ya Shukurani inayoendeshwa na Vodacom Tanzania kusherehekea kutimiza miaka kumi ya huduma ya M-PESA. Huduma ya Vodacom ya M-PESA ndiyo inayoongoza nchini Tanzania ikiwa imekamata asili mia 42 ya soko.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu alisema, “Leo tunafuraha kubwa sana kupata fursa hii kukutana na wateja na mawakala wetu wa Kanda za Nyanda za Juu Kusini ili kutoa shukurani zetu kwao na kuwakabidhi washindi wa promosheni yetu zawadi wao. Zawadi hizi zinashindaniwa na watumiaji wa M-PESA wote nchini, na wanavyozidi kuitumia, ndivyo wanavyojiongezea nafasi ya kushinda”
Katika kusherehekea mafanikio ya M-PESA na pia kama ishara ya shukurani, Vodacom imekuwa ikiwazawadia wateja, mawakala na wauzaji katika kipindi chote cha kampeni hii. Zawadi ni pamoja na magari mapya na ya kisasa kumi pamoja  na zawadi za pesa taslimu kila wiki ambapo kwenye kipindi cha wiki 10, wateja zaidi ya 100 watajishindia mamilioni. Ili kujiongezea nafasi ya kushinda, wateja wanashauriwa kufanya mihamala mingi zaidi kupitia M-PESA iwe kufanya malipo, kutuma pesa au manunuzi, kununua muda wa maongezi na vifurushi au hata kutuma pesa nje ya nchi. Kujua pointi walizonazo, wateja, wauzaji na mawakala watahitaji kupiga namba *150*00# na kuchagua “JISHINDIE GARI”.
Wateja wasio na akunti hai ya M-PESA wanahitaji kufufua akaunti zao na kufanya mihamala ili kupata nafasi ya kushinda magari haya mapya na ya kisasa au pesa taslimu. Shindano hili pia linawajumuisha mawakala na wauzaji wapya wanaojiunga wakati wa kampeni.
Akihutubia hafla hiyo, mgeni wa heshima, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Amos Makalla  alisema, “Zawadi zinazoshindaniwa ninauhakika zitaleta mabadiliko makubwa katika maisha ya washindi watakaobahatika kujinyakulia. Kwa mfano, zawadi ya magari ya kisasa kabisa yanayoshindaniwa, magari hayo yatawarahisishia washindi usafiri, hii itawawezesha kufanya shughuli zao kwa ufanisi mkubwa zaidi au hata kuanzisha zile walizokuwa wanashindwa kufanya hapo awali. Vile vile, ninaelewa kuwa kuna zawadi nyingi za pesa taslimu.”
 
Katika hotuba yake, mgeni wa heshima alizungumzia umuhimu wa ushirikiano na jamii kama unavyofanywa na Vodacom Tanzania kwa kutumia mtandao wake wa M-PESA, “Mabibi na mabwana, ningependa kutoa pongezi za dhati kutoka kwa serikali kuenda kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na Vodacom Tanzania Foundation kwa matumizi chanya na ya kibunifu ya mtandao wao na huduma yao ya M-PESA kusaidia kuwezesha wanawake na vijana wengi sana nchini. Tunafurahi kuona kuwa Vodacom wamejitahidi sana kuonyesha kujali jamii na kuhakikisha kuwa jitihada zao za kusaidia zinaendana na sera na mahitaaji ya nchi.” Aliongeza mkuu huyo wa mkoa.
Bi. Jacquiline Materu alimalizia kwa kusema, “Nawapongeza washindi wote waliojipatia zawadi hizi. Hii ni ishara ndogo tu ya shukurani kutoka vodacomm Tanzania kwa watumiaji wa M-PESA. Naomba kuwakumbusha Watanzania kuwa shindano bado linaendelea na kuna zawadi nyingi bado zimebaki zikisubiri washindi. Sambamba na kutoa zawadi hizi, tunaahidi kuwa tutaendelea kutoa huduma kwa kiwango cha juu kabisa na tutaendelea kuboresha na kuongeza huduma zetu kwani nyinyi, wateja wetu, mnastahili kilicho bora kabisa, na tunaamini kuwa mnategemea hilo kutoka kampuni ya mawasiliano ya simu inayoongoza nchini, Vodacom.”
Huduma ya M-PESA ya Vodacom Tanzania inaongoza soko nchini kwa kutuma pesa na kufanyia malipo hivyo kufanya mfumo wake wa malipo mtandaoni kuwa na kasi, urahisi na usalama. Vodacom Tanzania imejenga mtandao unaoendelea kupanuka wa wauzaji na watoa huduma nchi nzima wanaokubali malipo kwa njia ya M-PESA. Kulipa kupitia M-PESA ni bure na hakuna gharama zozote zile kwa mnunuzi wala muuzaji. M-PESA iliweza kuboresha mfumo huu wa malipo nchini kwa kuwa wa kwanza kuanzisha malipo kupitia alama za QR kwenye app ya M-PESA, jambo ambalo limerahisisha zaidi shughuli nzima ya malipo kwa wanunuzi na wauzaji.

Copyright © 2018 Vodacom Tanzania. All Rights Reserved.