05/07/2018

VODACOM TANZANIA YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA KAMPENI YA M-PESA ARUSHA

Kampuni ya mawasiliano ya simu inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania, leo ilikuwa na halfa ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa kampeni yake kanda ya kaskazini. Shughuli hiyo iliyofanyika mjini Arusha ilihudhuriwa na wakaazi wa Arusha na vitongoji vyake.

Kampeni hii inaendeshwa nchi nzima na ni katika kusherehekea miaka kumi ya mfumo wa kwanza nchini wa pesa mtandaoni; M-PESA ya Vodacom Tanzania.

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo, mwakilishi wa Vodacom Tanzania, Polycarp Ndekana alisema, “Vodacom Tanzania inajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye mfumo huu wa M-PESA katika miaka kumi tangu tuwe wa kwanza kuanzisha huduma ya aina hii nchini. Mafanikio hayo yametokana na kukubalika kwa huduma hiyo na kwa wateja kuendelea kuitumia kuliko nyingine zote nchini. Hivyo tumeona ni vyema kuwashukuru wateja, mawakala na biashara zilizojiunga na mfumo huu.”

M-PESA ndiyo mfumo wa pesa mtandaoni unaoongoza nchini uiwa umekamata asili mia 45 ya soko.  Mfumo huu unajivunia kuwa na watumiaji zaidi ya milioni 8, mawakala 106,000 vile vile  biashara zaidi ya 2,000 na benki 30 zimejiunga na M-PESA.

Mgeni wa heshima kwenye hafla hiyo alikuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo. Akihutubia wakati wa makabidhiano, alisema, “Mawasiliano ni kitu muhimu sana kwa Watanzania wote, na kwetu hapa Arusha yametusaidia sana kujijengea maendeleo yetu. Wakulima na wafanyabiashara wa Arusha wamezitumia vizuri sana huduma hizi zinazotolewa na makampuni ya mawasiliano kama Vodacom kwa manufaa ya jamii yetu.”

Katika kampeni hii, watumiaji na mawakala wa M-PESA wanapata nafasi ya kujishindia magari mapya na ya kisasa, pesa taslimu pamoja na zawadi nyingine nyingi.

Mwakilishi wa Vodacom Tanzania alimalizia kwa kusema, “Tunawapongeza washindi wote leo hii na tunawaambia Watanzania wote kuwa shindano bado linaendelea. Zawadi hizi za magari na nyinginezo bado zipo kushindaniwa, endeleeni kutumia M-PESA kwa manunuzi na shughuli zenu za malipo ili kujiongezea nafasi za kushinda.”

Kwa upande Mkomeni Ernest Mgonho ambaye ndiye mshindi wa 3 katika promosheni ya Mpesa inayoendelea alionesha furaha sana baada ya kukabidhiwa gari yake mpya aina ya Renault Kwid

“Mimi nimekuwa mteja wa Vodacom  kwa muda mrefu na ni mtumiaji mahiri sana wa huduma ya M-Pesa katika malipo yangu yote iwe ni kulipia bidhaa dukani, kulipia ada au hata kulipia huduma za maji. Sikuwahi kujua kwamba nitajishindia gari kutoka Vodacom, ni jambo la heri sana kwa Vodacom kutambua na kuwazawadia wateja wake. Nimefurahi sana na ninasema asante Vodacom nawashauri watu  waendelee kutumia Mpesa kwani Pesa ni M-PESA”

 

Mwisho

 

Kuhusu Vodacom Tanzania Plc

Vodacom Tanzania PLC ni kampuni ya mawasiliano inayoongoza ikiwa na mtandao wa data wenye kasi zaidi nchini. Tunawapatia huduma ya mawasiliano wateja zaidi ya milioni 12. Vodacom Tanzania na kampuni zake tanzu ni sehemu ya Vodacom Group iliyosajiliwa nchini Afrika Kusini ambay na yenyewe inamilikiwa na Vodacom Group Plc ya uingereza. Imesajiliwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwa na namba ya usajili ISIN:TZ1886102715 na jina: VODA.

Copyright © 2018 Vodacom Tanzania. All Rights Reserved.