11/07/2018

KAMPENI YA SHINDA GARI NA M-PESA YATUA KWA KISHINDO JIJINI DODOMA

Kampuni ya mawasiliano ya simu inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania, leo imefanya hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa kampeni yake ya kusherehekea miaka kumi ya mfumo wa M-PESA. Shughuli hiyo imefanyika mjini Dodoma na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake.

Katika kampeni hii ya kushukuru watumiaji wa mfumo wa M-PESA, Vodacom Tanzania imekuwa ikiendesha mashindano nchi nzima ambapo washindi wamejishindia magari mapya aina ya Renault Kwid pamoja na zawadi za pesa taslimu.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Idara ya Huduma kwa wateja Vodacom Bi Harriet Lwakatare   alisema, “Tunaendela kutoa zawadi hizi kama ishara ndogo tu ya shukurani zetu kwa watumiaji wote wa M-PESA pamoja na mawakala wetu. Mafanikio yote yaliyopatikana katika mfumo wenyewe na katika jamii zinazoutumia, zimetokana na wateja wetu kuendelea kutuamini na kututegemea kuwapatia huduma yenye ubora zaidi nchini. Tunawapongeza washindi wote na kuwaambia watumiaji wengine waendelee kutumia M-PESA zaidi na zaidi ili kujiongezea nafasi za ushindi.”

Mgeni rasmi kwenye sherehe hizo, mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mh. Dk Binilith Mahenge  alitoa salaam za shukurani kwa kampuni ya Vodacom kwa kutoa huduma bora inayokubalika na kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa, na kwa msaada inayotoa katika jamii zenye uhitaji.

“Huduma ya M-PESA imesambaa na kuongeza uwezo wake kiasi kwamba inatumika kwa kiwango kinachoshindana na mabenki na taasisi zingine za kifedha. Kutokana na kutumika hivyo, M-PESA inachangia kiasi kikubwa cha kodi kwa taifa. Pamoja na kodi hiyo, tunafurahi kuona M-PESa ikitumika kufanya malipo ya kodi zingine za serikali kama vile VAT, kodi za ardhi na kadhalika. Hivyo M-PESA imekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa letu. Hii imewezekana kutokana na ushirikiano wa karibu uliokuwepo kati ya uongozi wa Vodacom Tanzania na serikali ya Jamuhuri” alisema

Mwakilishi wa Vodacom Tanzania alimalizia kwa kusema, “Tumefurahi sana kuwepo hapa leo hii. Tunawashukuru wakazi wote wa Dodoma kwa mapokezi mazuri mliyotupa na tunawapongeza sana washindi waliopatikana. Tunawaahidi kuwa tutaendeleza na kuongeza huduma tunazozitoa kwani mnastahili kilicho bora kabisa na mnastahili bidii zetu za dhati.”

 

Aloyce Edward mkazi wa Dodoma ambaye ndiye mshindi wa nne kujishindia gari mpya katika promosheni hiyo ya Vodacom alishukuru sana kampuni ya Vodacom kwa kumthamini na kumzawadia gari mpya. Aliwaasa watumiaji wa Vodacom kutumia huduma ya M-Pesa kwani inarahisisha maisha.

 

Kuhusu Vodacom Tanzania Plc

Vodacom Tanzania PLC ni kampuni ya mawasiliano inayoongoza ikiwa na mtandao wa data wenye kasi zaidi nchini. Tunawapatia huduma ya mawasiliano wateja zaidi ya milioni 12. Vodacom Tanzania na kampuni zake tanzu ni sehemu ya Vodacom Group iliyosajiliwa nchini Afrika Kusini ambayo na yenyewe inamilikiwa na Vodacom Group Plc ya uingereza. Imesajiliwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwa na namba ya usajili ISIN:TZ1886102715 na jina: VODA.

Copyright © 2018 Vodacom Tanzania. All Rights Reserved.