02/08/2018

KAMPENI YA SHINDA GARI NA M-PESA YATUA KWA KISHINDO JIJINI DAR ES SALAAM

Kampuni ya mawasiliano ya simu inayoongoza nchini, Vodacom Tanzania, leo imefanya hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa kampeni yake SHINDA GARI JIPYA NA M-PESA katika kusherehekea miaka kumi ya mfumo wa M-PESA. Shughuli hiyo ilimefanyika katika viwanja vya Zakhiem hapa Jijini Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Dar Es Salaam na vitongoji vyake.

Katika kampeni hii ya kushukuru watumiaji wa huduma ya M-PESA, Vodacom Tanzania imekuwa ikiendesha mashindano nchi nzima ambapo mpaka sasa washindi watano wamejishindia magari mapya aina ya Renault Kwid (2017).

Watumiaji, mawakala na wafanya biashara wanaopokea malipo kwa huduma hii ya M-PESA wamepata nafasi ya kujishindia pesa taslimu huku wengine wengi wakitegemewa kujishindia zawadi hizo katika kampeni hii inayoendelea.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Kitengo cha biashara cha M-Pesa Polycarp Ndekana   alisema, “Vodacom Tanzania inajivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye mfumo huu wa M-PESA katika miaka kumi tangu tuwe wa kwanza kuanzisha huduma ya aina hii nchini. Mafanikio hayo yametokana na kukubalika kwa huduma hiyo na kwa wateja kuendelea kuitumia kuliko nyingine zote nchini. Hivyo tumeona ni vyema kuwashukuru wateja, mawakala na biashara zilizojiunga na mfumo huu.”

M-PESA ndiyo mfumo wa pesa mtandaoni unaoongoza nchini na watumiaji zaidi ya milioni 8, mawakala 106,000 vile vile  biashara zaidi ya 2,000 na benki 30.Tunawapongeza washindi wote na kuwaambia watumiaji wengine waendelee kutumia M-PESA zaidi na zaidi ili kujiongezea nafasi za ushindi,” aliongeza Ndekana.

Mwakilishi huyo wa Vodacom Tanzania alimalizia kwa kusema, “Tunawapongeza washindi wote leo hii na tunawaambia Watanzania wote kuwa shindano bado linaendelea. Zawadi hizi za magari na nyinginezo bado zipo kushindaniwa, endeleeni kutumia M-PESA kwa manunuzi na shughuli zenu za malipo ili kujiongezea nafasi za kushinda.”

Salum Chande Athumani mkazi wa Mbagala Rangi Tatu Jijini Dar es Salaam ambaye ndiye mshindi wa tano kujishindia gari mpya katika promosheni hiyo ya Vodacom alishukuru sana kampuni ya Vodacom kwa kumzawadia gari jipya. Aliwaasa watumiaji wa Vodacom kutumia huduma ya M-Pesa kwani inarahisisha maisha.

 

Kuhusu Vodacom Tanzania Plc

Vodacom Tanzania PLC ni kampuni ya mawasiliano inayoongoza ikiwa na mtandao wa data wenye kasi zaidi nchini. Tunawapatia huduma ya mawasiliano wateja zaidi ya milioni 12. Vodacom Tanzania na kampuni zake tanzu ni sehemu ya Vodacom Group iliyosajiliwa nchini Afrika Kusini ambayo na yenyewe inamilikiwa na Vodacom Group Plc ya uingereza. Imesajiliwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwa na namba ya usajili ISIN:TZ1886102715 na jina: VODA.

Copyright © 2018 Vodacom Tanzania. All Rights Reserved.