14/06/2017

Mamilioni ya wanafunzi nchini watanufaika na mpango wa huduma ya elimu  kupitia mtandao yenye lengo la kuongeza ubora na urahisi wa upatikanaji wa elimu hapa nchini mpango huo umeanza kutekelezwa rasmi leo hii na Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania kupitia taasisi yake inayojishughulisha na shughuli mbalimbali za kijamii”Vodacom Tanzania Foundation”, Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi wa mawasiliano na Vodacom Tanzania Foundation,Rosalynn Mworia alisema wameamua kuleta huduma hii iliyobora kwa wanafunzi itakayojulikana kama Papo hapo ambayo itawawezesha wanafunzi na walimu kupata nakala za masomo bila malipo yoyote na kwa ubora wa lugha ya Kiswahili na Kiingereza,Kwa kweli tumefarijika sana kwa kuleta huduma hii kwani imekuwa muda mrefu sasa, upatikanaji wa elimu nje ya mfumo wa darasani umekuwa ni mgumu – jambo ambalo limesababisha kizuizi kwa watoto wetu wanafunzi  ambao wanataka kupata elimu lakini hawana uwezo wa kuhudhuria darasani.
Copyright © 2018 Vodacom Tanzania. All Rights Reserved.