05/06/2017

TANGAZO KWA UMMA

Tukiwa kampuni pekee ya Mawasiliano inayoongoza nchini,Leo hii tunapenda kuwajulisha wateja wetu na watanzania wote kwa ujumla kwamba kutokana na ubora na umakini wa matangazo yetu tunayotengeneza, Vodacom Tanzania PLC hatujahusika na hatutakuja kuhusika na utengenezaji wa tangazo au Matangazo yeyote ambayo hayana maadili ya kitanzania kamwe! Kampuni yetu tunavyo vigezo muhimu vya kutengeneza matangazo na vifuatavyo ndiyo mihimili mikuu mitatu imara ya kampuni yetu katika kutengeza matangazo na jumbe mbalimbali tunazotoa kwa Umma.

Utamaduni na Maadili ya Kitanzania
Weledi
Ustaarabu
Tukiwa tunaendelea na jitihada za kubaini wahalifu wenye mikakati miovu ya kusambaza jumbe mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii tumefungua malalamiko polisi nakufunguliwa faili namba CDRB42192017, CDIR17432017 Tunapenda kuomba radhi kwa wateja wetu wote na watanzania kwa ujumla na kuwasihi kulipuuzia tangazo hilo kwani halina mashiko na halihusiani na Kampuni yetu kabisa.

Ahsanteni na jumatatu njema
Copyright © 2018 Vodacom Tanzania. All Rights Reserved.