VPL Updates

Kocha Yanga Ataka Usajili Kama Wa Simba

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, ameutaka uongozi wa timu hiyo kusimamia matakwa yake katika zoezi zima la usajili ili kuhakikisha msimu ujao timu hiyo inakuwa na kikosi imara zaidi ya Simba.

Eymael ambaye sasa yupo nyumbani kwao Ubelgiji alipoenda baada ya ligi kusimama kutokana na janga la Corona, amesema kuwa anataka kuwa na kikosi kitakachokuwa na wachezaji wa kuamua matokeo wanapokuwa uwanjani.

Habari ambazo Spoti Xtra, limezipata kutoka ndani ya Yanga, zimedai kuwa, Eymael amefi kia hatua hiyo kutokana na kuvutiwa vilivyo na kikosi cha Simba jinsi kilivyo na wachezaji wengi wenye uwezo huo wa kuamua matokeo muda wowote wanapokuwa uwanjani.

“Kocha ametuambia kuwa kilichoibeba zaidi Simba msimu huu ni kuwa na wachezaji wengi wa kuamua mtokeo wanapokuwa uwanjani ukilinganisha na sisi. ameutaka uongozi kuhakikisha usajili utakaofanyika safari hii uzingatie zaidi mapendekezo yake jambo ambalo uongozi umelipokea na umeshaanza kulifanyika kazi.

“Ni matumaini yetu kuwa msimu ujao tutakuwa na kikosi bora zaidi na chenye wachezaji wa kuamua matokeo wakati wowote ule wanapokuwa uwanjani,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipotafutwa Eymael ili azungumzie hilo hakupatikana, lakini Ofi sa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alipoulizwa kuhusiana na hilo alisema kuwa: “Ni kweli kocha anataka msimu ujao tuwe na kikosi kizuri chenye wachezaji wenye uwezo wa kuamua matokeo uwanjani wakati wowote ule, na sisi kama uongozi tumeyapokea mapendezo yake hayo na yatafanyiwa kazi.”.

Copyright © 2020 Vodacom Tanzania. All Rights Reserved.