VPL Updates

Sharaf Shiboub Kurudi Kivingine

Sharaf Shiboub raia wa Sudan, ameliambia Spoti Xtra kuwa, kabla ya Ligio Kuu Bara kusimama kutokana na janga la corona, alikuwa hafurahishwi na kiwango chake uwanjani jambo ambalo lilimfanya akose nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kinachofundishwa na Mbelgiji, Sven Vandenbr-oeck.

Shiboub amedai kuwa, hali hiyo ilikuwa ikimkosesha amani klabuni hapo na kujikuta akitumia muda mwingi kutafakari nini cha kufanya

Kiungo huyo ambaye kwa sasa yupo kwao Sudan akiendelea kujifua, amesema: “Nipo nyumbani kutoka na janga hili la Corona na sijui litaisha lini ili nirudi Tanzania kujiunga na timu yangu.

“Pamoja na hali hiyo, bado ninajifua sana huku ili niweze kuwa fi ti na nitakaporudi Simba nipate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa zamani.

“Kusema kweli hakuna jambo li-naloniumiza kama kutocheza, kwa hiyo napambana huku kwa kufanya mazoezi ya nguvu ili niweze kuwa fi ti na kocha atakapo-niona basi asiwe na shaka tena na mimi

Copyright © 2020 Vodacom Tanzania. All Rights Reserved.