VPL Updates

Kisa Mwamnyeto… Simba Yaanza Jeuri, C.E.O Atoa Kauli Ya Kibabe

MKURUGENZI Mtendaji wa Klabu ya Simba ambaye ni raia wa Afrika Kusini, Senzo Mazingisa ametamba kuwa wachezaji wa ndani hakuna yeyote watakayemtaka na kushindwa kumsajili.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu tetesi zienee za Yanga kufikia muafaka mzuri na nahodha na beki wa kati wa Coastal Union ya mkoani Tanga, Bakari Mwamnyeto.

Simba wanapata jeuri kutoka kwa mwekezaji wao bilionea, Mohammed Dewji ‘Mo’ ambaye alifanikisha usajili wa kiungo wa kiungo mshambuliaji raia wa Msumbiji, Luis Miquissone aliyekuwa anawaniwa na Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi,Senzo alisema kuwa wao wanafanya usajili wao kwa kufuata ripoti ya kocha wao raia wa Ubelgiji, Sven Vandenbroeck atakayeitoa kwa uongozi itakayoelekeza mapendekezo ya usajili.

Senzo alisema kuwa wana uw-ezo wa kum-sajili mche-zaji yeyote watakayem-uhitaji katika kuelekea msimu ujao wakitumia dau lolote la usajili kwa mchezaji wa-nayemtaka.

Aliongeza kuwa hawa-takurupuka katika usa-jili wa msimu ujao na hivi wapo kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji wanaomaliza mi-kataba yao kabla ya kugeukia wapya atakaowapendekeza kocha wao.

“Tumeanza kufanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao inayoelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu kwa kuhakikisha wale wote waliopendekezwa na kocha wanabakia.

“Tayari nimekutana na kocha kujadiliana baadhi ya masuala mbalimbali ya timu likiwemo la usajili ambalo kwa sasa bado hatujalianza rasmi tukisubiria ligi ikimalizika ndiyo tuanze rasmi.“Hivi sasa nguvu na akili zetu tu-meziele-keza kwenye ubingwa wetu wa ligi msimu huu kwa ku-hakikisha tunashinda michezo yote ili-yobakia ili tuchukue ubingwa huo,” alisema Senzo

Copyright © 2020 Vodacom Tanzania. All Rights Reserved.