Self Service

General

A. Kununua Vocha mitandao mingine inamaana gani?

Hii ni huduma mpya kutoka Vodacom M-Pesa inayokuwezesha kununua vocha za mitandao mingine kupitia akaunti yako za M-Pesa.

B. Nani anaweza kutumia hii huduma?

Ni wateja wa Vodacom M-Pesa tuu ndo mnaweza kununua vocha za mitandao mingnine kupitia akaunti zenu za M-Pesa.

C. Je, wateja wa mitandao mingine wanaweza nunua vocha za Vodacom?

Hapana, kwa sasa ni wateja wa Vodacom tuu ndo mnaweza kununua vocha za mitandao mengine kupitia akaunti zenu M-Pesa.

D. Tunaweza tumia huduma hii kununua bando pia?

Hapana, kwa sasa unaweza kununua vocha za mitandao mingine tuu.

E. Je, kuna gharama zozote za kutumia huduma hii?

Hapana, hamna gharama zozote za kutumia huduma hii. Kama mteja utanunua vocha ya Tshs 1,000 utakatwa Tshs 1,000 kwenye akaunti yako ya M-Pesa.

F. Tunawezaje kununua vocha ya mitandao mingine?

  • 1. Piga *150*00#
  • 2. Chagua “3” Nunua Vifurushi/Muda wa Maongezi
  • 3. Chagua “6” Airtime – Mitandao Mingine
  • 4. Chagua Mtandao mwingine. mf. Halotel, Airtel
  • 5. Weka Namba ya Simu
  • 6. Weka Kiasi
  • 7. Weka Namba ya Siri
  • 8. Kisha chagua “1” kuthibitisha muamala
Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa