Ili kampuni kubwa ziweze kuona mafanikio, ni lazima wawe na mtandao unaowapa mwunganisho kila pale walipo.
Vodacom Business inawapa teknolojia za kisasa zinazowapa huduma za kuwawezesha zaidi.

Kampuni Kubwa

Huduma Kwa Biashara

Huduma hizi ni kwa ajili ya miradi na biashara kama vituo vya afya, mashamba, na shule.

 • Huduma hii inakupa uwezo wa kuona idadi ya vifaa au bidhaa , kukupa taarifa ya matumizi na kukukumbusha pale inapofika wakati wa kuagiza vitu vipya.
 • Huduma hizi ni ya kimapinduzi kwenye soko kwani inatoa nafasi ya kukuza biashara na kuongeza ufanisi zaidi.

AFYA
Stock Visibility Solution (SVS)

Kwa kutumia njia za mtandao (Stock Visibility Solution) ni suluhIsho litowalo uhakika wa akiba ya madawa katika zahanati na maduka ya madawa. Hii ni njia ambayo inaiwezesha mteja kupeleka madawa mahali pasipo na madawa na kuongezea mahali pailpo na uchache kwa wakati muafaka. FAIDA ZAKE Kwa kutumia njia za mtandao (SVS), habari za akiba ya madawa zinapatikana bila kuchelewa kutoka katika zahanati na hivyo mahali palipo na mapungufu panaongezewa na mahali walipoishiwa wanapelekewa kwa kipau mbele. Kwa njia hii, Idara ya Afya ya Taifa inakuwa inasimamia mtiririko wa ugavi wa madawa na inaweza kulinganisha madawa yaliyonunuliwa kutoka sehemu mbali mbali ambayo yako katika madirisha ya zahanati. SVS inaiwezesha mteja kuwa mshiriki mwenye uelewa wa ndani kuliko ni kiungo kinachosukumwa tu.

ELIMU
Instant school

Instant school, ni suluhisho jipya lenye kulenga kufanya wepesi wa masomo kwa kutumia njia za Digitali katika shule ambazo zinaendeshwa zikiwa na mifumo kadhaa. Njia hii inaondoa tofauti baina ya wanafunzi na kuleta maendeleo mazuri kimasomo kwa wote pamoja.
FAIDA

 • Vitabu vyote viko sehemu moja, hivyo wanafunzi na walimu wanaweza kufanya marejeo kwa wepesi. Wanaweza kusoma kwa pamoja na pia kufanya majadiliano wakiwa popote pale na wala hamna haja ya kubeba mzigo wa vitabu. Wanafunzi wa Kidato cha IV wanaweza kufanya marejeo kwa vitabu vya kuanzia Kidato cha I mpaka cha IV.
 • Kusoma kwa kidigitali ni jambo lenye mvuto sana kwa wanafunzi na walimu maana usomaji huo una njia nyingi za ushirikishaji papo hapo ikiwa ni chachu inayoibua uwezo wa kufikiri na watu kupanua mawazo.
 • Somo kwa kidiigitali huwawezesha walimu kutoa maelezo ya misamiati migumu na nadharia ngeni na ngumu. Hii ni njia ambayo ni nyepesi kwa mwanafunzi kuelewa bila kuhangaika.

  • School Management Solution
   Njia ya Digitali inatoa wepesi katika uendeshaji wa shule na katika miamala baina ya Shule na Idara ya Elimu huleta ufumbuzi wa mambo kwa haraka.
   FAIDA ZAKE
   • Njia hii inawawaezesha wakuu wa Shule kutoa taarifa kwa wakuu wao ikiwa pamoja na Idara ya Elimu juu ya mambo ya utendaji wa kawaida na matukio ambayo yasiyo ya kawaida. Idara ya Elimu inakuwa na uelewa wa maendeleo ya shule na mwendelezo wake.
   • Watendaji wa Idara wakiwa wamepata habari za matukio katika shule ni rahisi kwao kutoa suluhisho na misaada kwa muda mfupi sana.
   • Taarifa zinapatikana kwa wadau wa Elimu walio katika daraja mbali mbali kwa wakati muafaka na njia hii inawezesha data kupatikana kwa muda mfupi na hivyo kurahisisha ufanisi wa Idara nzima na utekelezaji mzuri wa mikakati.
    • KILIMO
     Connected Farmer

     Vodacom imeleta suluhisho la kuondoa changamoto zinazowakumba wafanya biashara wa mazao ya kilimo wakiwa wanafanya biashara na SHFs. Ni rahisi kutumia katika kuendesha biashara kwa wadau wote katika mambo ya kilimo. Mtandao huu unaweza kumpa mtu MAELEZO MAFUPI JUU YA MKULIMA, MAWASILIANO KATIKA KILIMO KUPITIA MTANDAO NA MIAMALA YOTE KUPITIA SIMU YA MKONONI
     FAIDA ZAKE
     A. Kwa Biashara ya Kilimo:

     • Hupunguza gharama na hatari za kupata hasara kwa kupitia kifaa kinachokupa uwezo wa kuwa na habari zote kuhusu wakulima wadogo wadogo (Know Your Farmer).
     • Ni rahisi kwa Mkulima mkuu kufanya maamuzi yenye uhakika kutokana na data anazozipata katika mtandao kuhusu mkulima (Maelezo ya Mkulima na Shamba lake).
     • Inaongeza ufanisi, uzalishaji na uwazi wa mambo katika mfumo wote wa kilimo.
     • Inawasaidia wakulima wadogo wadogo na kuwafanya wajiamini hali ambayo inapunguza ulanguzi wa mazao.
     • Malipo yanafanyika kwa wakati muafaka kupitia mtandao wa Mpesa na hali hiyo inapunguza changamoto nyingi na hatari za kubeba mzigo wa pesa.


     • B. Kwa Mkulima
     • Taarifa za ukweli na uhakika zinapatikana kwa watu mahususi; taarifa hizo zikiwa juu ya mkulima na maelezo yake .
     • Mkulima huweza kufahamu masoko ya mazazo yake na yaliyo ya karibu na njia za kupitia kufikia huko
     • Mkulima anakuwa na uwezo wa kupata mbinu mpya za kuwa karibu na misaada
     • Mkulima anakuwa na uwezo mkubwa wa kifedha na njia nyingi za kutumia katika kuendeleza biashara zake.
     • Mkulima anapata malipo kwa wakati muafaka kwa kutumia Mpesa jambo ambalo linapunguza changamoto na hatari za kubeba mizigo ya fedha nyingi mfukoni.
      • Niko Tayari Kuzungumza na Timu ya Mauzo

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa