KUZURU NA KIMATAIFA

Maelezo ya jumla

 • Kuzuru
 • Kujiunga na huduma ya kuzuru Kimataifa
 • Vifrushi vya Kuzuru
 • Viwango vya kupiga na kutuma meseji kimataifa
 • Vifurushi vya kupiga kimataifa
 • Vigezo na Masharti

Kuzuru

Kuzuru

 • Hakuna sababu ya kununua laini nyingine unaposafiri nje ya Tanzania.
 • Pata gharama nafuu zaidi kupiga simu, kuperuzi intaneti na kutuma SMS.
 • Pata punguzo uwapo kwenye maongezi, intaneti na SMS ukiwa nje ya nchi.
 • Tunajua ungependa kuwa na mawasiliano ya uhakika popote iwe ni ndani au nje ya nchi. Ndio maana tumekupa huduma itakayokuwezesha kupiga na kupokea simu bila wasiwasi unapotembea popote duniani. Vumbua gharama zetu nafuu za kupiga simu kimataifa na kuzuru zitazokuwezesha kutumia laini ya Vodacom bila wasiwasi utembeapo popote duniani.
 • Vodacom pamoja na washirika wake wa kimataifa, wamehakikisha vifurushi na gharama za kuzuru ni nafuu zinaazokidhi mahitaji yako ya kibishara na kitalii popote unapokwenda.

Kujiunga na huduma ya kuzuru Kimataifa

Kujiunga na huduma ya kuzuru Kimataifa

 • Hakikisha una salio la kutosha kwenye simu yako. Hakuna kiasi maalum kinachotakiwa itategemea namna ya matumizi yako na bei ya mtandao husika.
 • Piga Hudumaa kwa Wateja +255754700000 kwa msaada wowote ukiwa unazuru.
 • Huduma hii ni BURE na itaondolewa tu kama utaomba kwa kupiga tena Huduma kwa Wateja.

Vifrushi vya Kuzuru

Nchi Mipangilio ya vifurushi na Mitandao Maelezo Information
Kenya Kenya-Safaricom:@Tshs.15,000 PigaDK10,PokeaDK5/Siku7
Kenya-Safaricom:@Tshs.45,000 PigaDK25,PokeaDK5,SMS50&MB200/Siku7
Kenya-Safaricom:@Tshs.55,000 1024MBs/7Siku/ 7 Siku
Kenya-Safaricom: @Tshs. 210,000 5000MBs/7Siku/ 7 Siku
South Africa SouthAfrica-Vodacom:@Tshs.10,000 Piga10Dkk/7Siku/ 7 Siku
SouthAfrica-Vodacom:@Tshs.35,000 Piga25DkkPigaing/Pokea3Dkk/50SMS/200Mbs/7Siku
SouthAfrica-Vodacom:Tshs.55,000 1024MBs/7Siku/ 7 Siku
SouthAfrica-Vodacom: @Tshs. 250,000 5000Mbs/7Siku/ 7 Siku
Uganda Uganda-MTN:@Tshs.15,000 Piga10Dkk/ 7 Siku
Uganda-MTN:@Tshs.70,000 Piga20Dkk/Pokea3Dkk/30SMS/200Mbs/ 7 Siku
Uganda-MTN:@Tshs.75,000 475Mbs/ 7 Siku
Uganda-MTN:@Tshs. 350,000 2500Mbs/ 7 Siku
Rwanda Rwanda-MTN:@Tshs.15,000 Piga9Dkk/ 7 Siku
Rwanda-MTN:@Tshs.70,000 Piga20Dkk/Pokea3Dkk/30SMS/200Mbs/ 7 Siku
Rwanda-MTN:@Tshs.75,000 475Mbs/ 7 Siku
Rwanda-MTN: @Tshs.350,000 2300Mbs/ 7 Siku
Mozambique Mozambique-Vodacom:@Tshs.10,000 Piga10Dkk/ 7 Siku
Mozambique-Vodacom:@Tshs.35,000 Piga25Dkk/Pokea3Dkk/50SMS/200Mbs/ 7 Siku
Mozambique-Vodacom: Tshs.55,000 1024Mbs/ 7 Siku
Mozambique-Vodacom:@Tshs. 250,000 5,000Mbs/ 7 Siku
DRC DRC-Vodacom:@Tshs.10,000 Piga10Dkk/Pokea1Dkk/ 7 Siku
DRC-Vodacom:@Tshs.35,000 Piga25Dkk/Pokea3Dkk/30SMS/200Mbs/ 7 Siku
DRC-Vodacom:@Tshs.55,000 1024Mbs/ 7 Siku
DRC-Vodacom:@Tshs. 250,000 5000Mbs/ 7 Siku
Malawi Malawi- Airtel : @ Tshs.30,000 Piga10Dkk/ 7 Siku
Malawi- Airtel:@ Tshs.100,000 Piga20Dkk/50SMS/100Mbs/ 7 Siku
Malawi- Airtel: @ Tshs.105,000 275Mbs/ 7 Siku
Malawi- Airtel:  @ Tshs.500,000 1375Mbs/ 7 Siku
Afrika Nzima- Safiri Afrika Afrika Nzima- Safiri Afrika@Tsh10,000 10Dkk /Day Kutumika Nchi zote za Afrika isipokuwa Mali, Mauritania, Sao Tome*Principe, Somalia, Cape Verde,
Afrika Nzima- Safiri Afrika@Tsh20,000 20MBs / Day
Afrika Nzima- Safiri Afrika@ Tsh50,000 25Dkk /25SMS/ 50MB / 7Siku
SA, Mozambique, DRC &Lesotho SA, Mozambique, DRC &Lesotho @Tsh14,000 20Dkk/ 10SMS/ 10MBs / Day
UK UK-Vodafone:@Tshs.10,000 Piga10Dkk/Pokea5Dkk/ 7Siku
UK-Vodafone:@Tshs.35,000 Piga25Dkk/Pokea5Dkk/50SMS/200Mbs/ 7Siku
UK-Vodafone:@Tshs.55,000 1024Mbs/ 7Siku
UK-Vodafone:@Tshs. 250,000 5000Mbs/ 7Siku
Germany Germany-Vodafone:@Tshs.10,000 Piga10Dkk/Pokea5Dkk/ 7Siku
Germany-Vodafone:@Tshs.35,000 Piga25Dkk/Pokea5Dkk/50SMS/200Mbs/ 7Siku
Germany-Vodafone:@Tshs.55,000 1024Mbs/ 7Siku
Germany-Vodafone:@Tshs. 250,000 5000Mbs/ 7Siku
Italy Italy - Vodafone: @ Tshs.10,000 Piga10Dkk/Pokea2Dkk/ 7Siku
Italy - Vodafone: @ Tshs.35,000 Piga25Dkk/Pokea5Dkk/50SMS/200Mbs/ 7Siku
Italy - Vodafone: @ Tshs.55,000 1024Mbs/ 7Siku
Italy - Vodafone:   @ Tshs. 250,000 5000Mbs/ 7Siku
Uholanzi Uholanzi - Vodafone: @ Tshs.10,000 Piga9Dkk/Pokea2Dkk/ 7Siku
Uholanzi - Vodafone: @ Tshs.35,000 Piga22Dkk/Pokea5Dkk/50SMS/200Mbs/ 7Siku
Uholanzi - Vodafone: @ Tshs.55,000 1024Mbs/ 7Siku
Uholanzi - Vodafone: @ Tshs. 250,000 5000Mbs/ 7Siku
Uturuki Uturuki - Vodafone: @ Tshs.10,000 Piga10Dkk/Pokea3Dkk/ 7Siku
Uturuki - Vodafone: @ Tshs.35,000 Piga24Dkk/Pokea5Dkk/50SMS/200Mbs/ 7Siku
Uturuki - Vodafone: @ Tshs.55,000 1024Mbs/ 7Siku
Uturuki - Vodafone: @ Tshs. 250,000 5120Mbs/ 7Siku
Special for Europe Ofa Maalum Kwa Ulaya @Tsh10,000 10Dkk/day This Bundle is applicable to all countries with Vodacom/ Vodafone networks except India,Fiji & Australia
Ofa Maalum Kwa Ulaya @Tsh14,000 20Dkk+10SMS+10MB/day
Ofa Maalum Kwa Ulaya @Tsh20,000 20MB/day
Ofa Maalum Kwa Ulaya @Tsh50,000 25Dkk +25SMS+50MB/7Siku
USA USA-AT&T:Tshs.5,000 Piga30Dkk,Pokea10Dkk/ 7Siku
USA-AT&T :Tshs.10,000 Piga50Dkk/Pokea10Dkk/50SMS/100Mbs7Siku
USA-AT&T: Tshs.25,000 1024Mbs7Siku
USA-AT&T : Tshs.100,000 5120Mbs/7Siku7Siku
UAE UAE-DU @Tshs.10,000 Piga10Dkk/Pokea5Dkk/7Siku7Siku
UAE-DU @Tshs.55,000 Piga20Dkk/Pokea3Dkk/50SMS/100Mbs/Siku7Siku
UAE-DUTshs.60,000 250Mbs7Siku
UAE-DUTshs. 300,000= 1250Mbs 1250Mbs7Siku

Viwango vya kupiga na kutuma meseji kimataifa

Viwango vya kupiga na kutuma meseji kimataifa
 • Wasiliana na ndugu na marafiki waliopo nje ya Tanzania
 • kwa vifurushi vyetu, bei za kupiga na kutuma meseji , angalia hapa chini
 • Bei zote ni bila Kodi Excise Duty-17% na VAT-18%

International Calling PAYG Tariffs

Call Category (Zones/Groups) Calling Destinations Retail Tariffs (Tshs/Sec) Tax Exl. Retail Tariffs (Tshs/Sec) Tax Incl.
Zone 1 India, China, Canada, USA. 7.7 10.7
Zone 2 Kenya. 9.2 12.8
Zone 3 UAE. 10.6 14.7
Zone 4. South Africa and UK. 12.4 17.2
Zone 5 Mozambique, Italy, Oman, Germany, Ghana, Botswana, Ethiopia, Nigeria, Netherlands, Angola, Swaziland and Denmark 14.8 20.5
Zone 6 Sweden, Spain, Switzerland, Norway, Lebanon, Ireland, France, Bangladesh, Uganda and Ivory Cost 17.70 24.5
Zone 7 Namibia, Rwanda, Malaysia, Sudan, Turkey, Japan, Thailand, Iran, Cameroon and Rest of Africa. 20.60 28.5
Zone 8 Burundi, Belgium, Comoros, Equatorial Guinea, Sierra Leone, Zimbabwe, Zambia, Malawi, DRC, Ivory Coast and Rest of the World. 25.2 34.8
Zone 9 Tunisia, Lithuania, Vanuatu, Maldives Islands, Yemen, Morocco, Madagascar, Gambia, Algeria, Seychelles, Gabon, Central African Rep, Chad, Congo Brazzaville, Guinea Rep., Guinea-Bissau, Mauritania 45.00 62.2
Zone 10 Somalia, Sao Tome, Tokelau, Cuba, Cook island, Franklin island, Reunion, Diego Garcia, Solomon islands, Falkland, Green land, Kiribati, Papua New Guinea, Nauru, St. Helena, Niue, Tuvalu, Norfolk Island, Christmas Islands, Cocos Islands, Tonga, Western Samoa, Antarctic, and Ascension Island 66.8 92.3
Zone 11 Thuraya, Iradium, Imarsat. 337.4 465.9

International SMS PAYG TARIFFS

 
Nchi Kiasi (Tsh/SMS) Tax Excl
Afghanistan, Philippines, Argentina, Australia, Bangladesh, Belize, Brazil, Brunei, Canada, Cambodia, Colombia, Cook Islands, Costa Rica, Cuba, Dominica, Dominican Rep, Fiji, French Polynesia, Guam, Guatemala, Haiti, Honduras, Hong Kong, India, Indonesia, Jamaica, Japan, Kazakhstan, Kirghizstan, Macau, Malaysia, Mexico, Myanmar, Nepal, New Caledonia, New Zealand, Nicaragua, Pakistan, Panama, Peru, Singapore, Sri Lanka, Suriname, Taiwan, Thailand, Trinidad & Tobago, Venezuela, U.S.A, Vietnam, Andorra, Liechtenstein, Malta, Monaco, Swaziland, Alaska, Samoa, Anguilla, Antarctic, Aruba, Ascension Island, Bahamas, Barbados, Bermuda, Bhutan, British Virgin Islands, Cayman Islands, Chile, Christmas Islands, Cocos Islands, Democratic Republic Of Timor-Leste, Diego Garcia, Eritrea, Falkland, Islands, Faroe Island, French Guyana, Georgia, Greenland, Guyana, Kiribati, North Korea, South Korea, Laos, Latvia, Lithuania, Maldives Islands, Marshall, Islands, Martinique, Micronesia, Moldova, Mongolia, Montserrat, Nauru, Netherland, Antilles, Niue, Oman, Palau, Paraguay, Puerto Rico, Serbia & Montenegro, Solomon Islands, St. Helena, St. Kitts-Nevis, St. Lucia, St. Pierre & Miquelon, St. Vincent & The Grenadines, Tadzhikistan, Tokelau, Turkmenistan, Turks & Caicos Islands, Tuvalu, Uruguay, Uzbekistan, Vanuatu, Virgin Islands (Us), Wallis & Futuna Islands, Kenya, Algeria, Angola, Bahrain, Benin, Botswana, Burundi, Cameroon, Central African Rep., Comoros, Djibouti, Egypt, Equatorial Guinea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Rep., Guinea-Bissau, Iran, Iraq, Israel, Ivory Coast, Jordan, Kuwait, Lebanon, Lesotho, Liberia, Libya, Mali, Mauretania, Mauritius, Mayotte, Morocco, Mozambique, Namibia, Qatar, Reunion, Rwanda, Saudi Arabia, Senegal, Somalia, South Africa, Sudan, Syria, Togo, Tunisia, Turkey, United Arab Emirates, Yemen, Zimbabwe. 156
Austria, Belgium, Denmark, Finland, Germany, Gibraltar, Greece, Iceland, Ireland, Italy, Luxembourg, Netherlands, Norway, Portugal, Spain, Sweden, Burkina Faso, Chad, Congo, Dem. Rep. Congo, Gabon, Ghana, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Seychelles, Sierra Leone, Uganda, Zambia, Albania, Azerbaijan, Belarus, Bosnia Herzegovina, Bulgaria, Croatia, Cyprus, Czech Rep., Estonia, Hungary, Macedonia, Montenegro, Poland, Romania, Russia, Slovakia, Slovenia, Ukraine. 185
Austria, Belgium, Denmark, Finland, Germany, Gibraltar, Greece, Iceland, Ireland, Italy, Luxembourg, Netherlands, Norway, Portugal, Spain, Sweden, Burkina Faso, Chad, Congo, Dem. Rep. Congo, Gabon, France, United Kingdom, Papua New Guinea, Switzerland, Tonga, Western Samoa, China, The Rest Of The World. . 279
International SMS-Satelite 1308

Vifurushi vya kupiga kimataifa

Vifurushi vya kupiga kimataifa

Nchi Garama (Tsh Taxes Inclusive) Kiasi (MIN) Kutumika ndani ya
Hong kong, Germany, India, Canada, China, USA & UK(Landline) 1000 20 7 Days
5000 100 7 Days
10000 200 30 Days
Kenya,Uganda & Rwanda 3000 4 1 Day
5000 8 7 Days
10000 20 30 Days
Burundi 6000 3 7 Days
15000 8 30 Days
South Africa 3000 4 1 Day
5000 8 7 Days
15000 25 30 days
Bostawana,Mozambique, Zambia & Zimbabwe, 3000 3 1 Day
5000 5 7 Days
10000 10 30 Days
DRC& Malawi 5000 3 1 Day
10000 7 7 Days
20000 15 30 Days
Egypt 3000 5 1 Day
10000 18 7 Days
15000 28 30 Days
Nigeria & Ghana 3000 4 1 Day
5000 8 7 Days
10000 20 30 Days
Lebanon, Pakistan, Qatar, UAE, Saudi Arabia & Yemen 2500 4 1 Day
5000 9 7 Days
15000 28 30 Days
Oman 3000 3 1 Day
5000 5 7 Days
15000 15 30 Days
France, Italy& UK(Mobile) 2500 15 1 Day
5000 35 7 Days
10000 75 30 Days
Russia 5000 5 7 Days
15000 12 30 Days
All countries with exception to Satellites, Vanuatu, Papua New Guinea, Maldives, Cuba, Tunisia, Ascension islands, Niue, Madagascar and Chad.” 50000 20 (International) + 50 Voda-Voda 30 Days

Vifurushi vya SMS kimataifa

Nchi Garama (Tsh Taxes Inclusive) Kiasi (SMS) Kutumika ndani ya
Kenya, Rwanda, South Africa, Zimbabwe, Uganda, Nigeria, Ghana, DRC, Zambia, Malawi, Botswana 2000 8 7 Days
France, Germany, Italy & UK 2000 8 7 Days
Lebanon, Oman,Pakistan,Qatar,Saudi Arabia, Yemen 2000 8 7 Days
Canada& USA 1000 10 7 Days

Vigezo na Masharti

VIGEZO NA MASHARTI YA VIFURUSHI VYA KIMATAIFA VYA KUPIGA SIMU NA KUTUMA UJUMBE

1. Fasili;
 • 1.1 Vifurushi vya kupiga simu/kutuma ujumbe ni vifurushi ambavyo vinawawezesha wateja wa Vodacom kupiga au kutuma ujumbe wa simu wa maandishi nje ya nchi wakiwa ndani ya nchi. Hii inajumuisha vifurushi vya kupiga simu na kutuma ujumbe na matumizi ya Huduma nje ya vifurushi.
 • 1.2 Lipa Kadiri Unavyotumia ni gharama/tozo zinazotozwa unapotumia Huduma bila kifurushi
 • 1.3 Nchi maana yake Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

2. Matumizi
 • 2.1 Vigezo na Masharti haya yatatambuliwa humu kama “Vigezo na Masharti/Masharti ya Matumizi” (dhana hizi zitatumika kwa kubadilishana) yametolewa na Vodacom Tanzania PLC (Itatumika/kutambulika kama “Vodacom” au “sisi” au “sisi wenyewe” au “yetu”) kwa ajili ya kutumiwa na watumiaji/wateja wa Vodacom (“Mteja”) (Itatumika/kutambulika kama “wewe” au “yako” au “mtumiaji” “wewe mwenyewe”) ambao hutumia vifurushi vya kimataifa vya kupiga simu na kutuma ujumbe wa simu wa maandishi, na kwa kulipia Kadiri unavyotumia (“Huduma”).
 • 2.2 Tafadhali soma Vigezo na Masharti haya, na Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Watumiaji wa Vodacom ambayo ni sehemu ya Vigezo na Masharti haya, yanayopatikana katika tovuti ya Vodacom. Kwa madhumuni ya Vigezo na Masharti yaliyoelezwa katika waraka huu, Vigezo na Masharti haya yatazingatiwa katika matukio yoyote ya migongano baina ya Vigezo na Masharti haya na Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Watumiaji wa Vodacom..

3. Gharama na Aina ya Huduma
 • 3.1 Huduma hizi zinapatikana kwa wateja wote wa malipo ya kabla, wateja wa malipo ya baada ya matumizi na wateja mseto.
 • 3.2 Kwa kupiga simu: Wateja wanaweza kupiga simu ya mkononi au ya mezani kulingana na mahitaji yao.
 • 3.3 Kwa simu zinazopigwa kwenda Uingereza kuna machaguo mawili.
 • 3.3.1 Kwa kupiga simu za mezani tu Wateja wanaweza kujiunga na vifurushi vya Combo Super pack
 • 3.3.2 Kwa kupiga simu za mkononi tu Wateja wanaweza kujiunga na vifurushi vya Ulaya.
 • 3.4 Kwa ujumbe wa simu wa maandishi; Wateja wanaweza kutuma ujumbe wa simu kwa rafiki na wanafamilia walioko nje ya Tanzania.
 • 3.5 Vifurushi vya kupiga simu/kutuma ujumbe wa simu wa maandishi kimataifa vinaweza kununuliwa kwa njia zote za Vodacom kupitia nambari za USSD (*149*01#), (*149*71#), App ya My Vodacom (My Vodacom App), tovuti ya Vodacom Tanzania kupitia vifurushi> Kimataifa
 • 3.6 Huduma hizi lazima zitumike Tanzania.
 • 3.8 Unaweza kununua vifurushi vya kupiga simu/kutuma ujumbe vya kimataifa kwa ajili yako au kwa ajili ya rafiki/mtu mwingine
 • 3.9 Bei zote za vifurushi vya kupiga simu/kutuma ujumbe kimataifa zinapatikana katika njia zote zilizobainishwa hapo juu na katika tovuti ya Vodacom. Bei zote zinajumuisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT)
 • 3.10 Unaweza kujiunga na zaidi ya kifurushi kimoja, au kifurushi chochote wakati wowote.
 • 3.11 Unaweza kuangalia salio bure kwa kupiga *149*60#

4. Matumizi nje ya Vifurushi/ Lipa Kadiri Unavyotumia
 • 4.1 Tozo au gharama za Lipa Kadiri Unavyotumia zinatumika ikiwa Mteja anatumia Huduma bila kuwa na kifurushi kwa nchi fulani au kutumia Huduma katika maeneo ambayo Vodacom haijaanzisha vifurushi vya aina hiyo. Viwango au tozo za nje ya vifurushi vitatumika kama ilivyoelezwa katika tovuti ya Vodacom.
 • 4.2 Ni wajibu wa Mteja kujijuza Mwenyewe kuhusu tozo na viwango vinavyotumika kutumia Huduma za Vodacom za Kupiga Simu au kutuma ujumbe wa simu wa maandishi Kimataifa nje ya vifurushi au Kulipia Kadiri Unavyotumia. Viwango na tozo hizi zinaweza kubadilika muda wowote.
 • 4.3 Viwango/gharama za Kulipia Kadiri Unavyotumia kwa ajili ya kupiga simu/kutuma ujumbe wa simu wa maandishi kimataifa vinatofautiana kulingana na nchi.
 • 4.4 Kwa Huduma za kupiga simu kwa Kulipia Kadiri Unavyotumia, malipo yanatozwa kwa kila sekunde 1 kwa nchi zote kasoro zile tu ambazo misimbo yake ni +882, +883, +888 ambazo malipo yanatozwa kwa kila sekunde 60.

5. Muda wa Matumizi ya Vifurushi vya Kupiga Simu na Kutuma Ujumbe wa Simu wa maandishi Kimataifa
 • 5.1 Muda wa Matumizi wa kifurushi ni muda ambao kifurushi kitakuwa halali kutumika.
 • 5.2 Vifurushi vya siku vitatumika kwa saa 24 kuanzia muda viliponunuliwa
 • 5.3 Vifurushi vya wiki vitatumika kwa siku 7 kuanzia tarehe viliponunuliwa
 • 5.4 Vifurushi vya mwezi vitatumika kwa siku 30 kuanzia tarehe viliponunuliwa
 • 5.5 Mara baada ya kutumia kifurushi chako ndani ya muda halali au kifurushi chako kikiisha muda wake, viwango vya nje ya kifurushi vitatumika.
 • 5.6 Unaweza kununua kifurushi kingine chenye chenye muda uleule wa matumizi au tofauti katika muda wowote. Kipaumbele cha matumizi kitatolewa kwa kifurushi kilichonunuliwa awali. Pale ambapo muda wa matumizi wa vifurushi vinavyonunuliwa baadaye ni mfupi kuliko vile vilivyonunuliwa hapo kabla, kipaumbele cha matumizi kitaelekezwa kwenye kifurushi cha muda mfupi.
 • 5.7 Wateja hawataweza kutumia tena kifurushi baada ya muda wa kifurushi kilichonunuliwa kuisha
 • 5.8 Wateja hawataweza kutumia kifurushi kilichoisha muda wake. Kifurushi kisichotumika kitaingizwa katika kifurushi kingine ikiwa utajiunga na kifurushi kingine kabla ya muda wa kifurushi cha awali kuisha. Ukijiunga na kifurushi kipya baada ya kile cha awali kuisha muda wake, kifurushi kisichotumika hakitakuwa halali na huduma zote za kifurushi hicho zitasitishwa baada ya muda wake kuisha.

6. Muda wa Matumizi na Spidi
 • 6.1 Vifurushi vyote vya kupiga simu na kutuma ujumbe wa simu wa maandishi vya kimataifa vinaweza kutumiwa kwa muda wowote wa siku katika kipindi cha uhalali wa kifurushi.

7. Vigezo na Masharti Mengine Yanayotumika
 • 7.1 Vigezo na Masharti haya yatatumiwa pamoja na Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Watumiaji wa Vodacom.
 • 7.2 Iwapo itatokea mkinzano, mpishano au mgongano kwa vigezo na masharti haya na Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Watumiaji wa Vodacom kwa Mteja Aliyejiunga, kulingana na umuhimu na matumizi Vigezo na Masharti haya yatazingatiwa yakifuatiwa na Vigezo na Masharti ya Jumla ya Mtumiaji wa Vodacom.
 • 7.3 Mtumiaji au Mteja yeyote anayetumia Huduma zinazotolewa chini ya Vigezo na Masharti haya atachukuliwa kuwa amesoma na kuelewa Vigezo na Masharti husika.
 • 7.4 Tuna haki ya kusitisha Huduma hizi ikiwa:
 • 7.1.1 utatumia Huduma kwa malengo yoyote yasiyoruhusiwa;
 • 7.1.2 tutabaini matumizi mabaya, kukiuka maudhui, vitendo vya udanganyifu au jaribio la udanganyifu linalohusiana na matumizi yako ya Huduma hii;
 • 7.1.3 tutatakiwa au kuombwa kufanya hivyo ili kutekeleza amri au maelekezo au mapendekezo kutoka serikalini, mahakamani, kwa mdhibiti au mamlaka zozote halali;
 • 7.1.4 tutatilia shaka au kujiridhisha kuwa umekiuka Masharti haya ya Matumizi;
 • 7.1.5 tutatakiwa kufanya hivyo ili kutatua matatizo ya kiufundi au kwa sababu za kuhakikisha usalama baada ya kukupa taarifa za kusitisha huduma hii;
 • 7.1.6 kutakuwa na haja ya kusaidia kuhuisha au kuboresha maudhui au utekelezaji wa Huduma hizi mara kwa mara muda baada ya kukupa taarifa za kusitisha huduma hii;
 • 7.1.7 tutaamua kusitisha kwa muda au kuacha kutoa Huduma hii kwa sababu za kibiashara au kwa sababu nyingine yoyote kama itakayoturidhisha.

  • 8. Kusitisha Kutoa Huduma
   • 8.1 Huwezi kukatisha matumizi ya Huduma hii baada ya kujiunga na kifurushi kabla ya muda wa matumizi yake kuisha. Huduma hii zitasitishwa baada ya muda wa matumizi ya kifurushi kuisha.

   9. Mabadiliko katika Vigezo na Masharti haya
   • 9.1 Tunaweza kuongeza au kubadili Vigezo na Masharti haya ya Matumizi kulingana na kifungu cha 9.2. Tunaweza kuongeza ada na tozo mpya au kubadili ada na tozo zilizopo wakati wowote; kutokana na sheria mpya, kanuni za kisheria, kanuni za Serikali au matakwa ya leseni, viwango vya kubadili fedha, kuanzishwa au kubadilishwa kwa kodi ya serikali au kutokana na mapitio yoyote ya mipango ya kibiashara ya Vodacom, mabadiliko ndani ya tasnia, mapendekezo kutoka vyombo vya usimamizi au kutokana na sababu nyingine itakayojitokeza.
   • 9.2 Tutakuarifu mapema ikiwa tunataka kuongeza au kubadili vigezo na masharti haya au ikiwa tunataka kuongeza ada na tozo mpya au kubadili zilizopo wakati au baada ya kujiunga na Huduma hizi. Kiasi cha malipo na aina ya taarifa tutakayokupa zitapitia njia mwafaka zinazotumika na kupatikana kwa wakati huo kwa mfano, tunaweza kukutaarifu kwa barua, barua pepe, simu (ikiwa ni pamoja na ujumbe uliorekodiwa au ujumbe mfupi wa simu wa maandishi) au kwa matangazo katika gazeti la kila siku au kila wiki au katika tovuti yetu au njia nyingine yoyote). Unashauriwa pia kutembelea tovuti yetu mara kwa mara ili kuona mabadiliko hayo kama kwa sababu zisizotarajiwa inawezekana hukupata taarifa za hizo.
   • 9.3 Ikiwa hukubaliani na mabadiliko au nyongeza katika Vigezo na Masharti haya, unaweza kusitisha huduma hizi kwa mujibu wa kifungu cha 10 hapo chini. Ikiwa wewe hujatutaka tusitishe Masharti ya Matumizi na bado unatumia Huduma hizi, utachukuliwa kuwa umekubali mabadiliko hayo tangu yalipoanza kutekelezwa.

   10. Kusitisha Huduma na au Masharti ya Huduma
   • 10.1 Tunaweza kusitisha Masharti haya ya Matumizi wakati wowote tutakapoamua. Usitishaji huo utafanyika baada ya kukupa Taarifa. Taarifa inaweza kuwa kwa barua, baruapepe, simu (ikiwa ni pamoja na ujumbe uliorekodiwa au ujumbe mfupi wa simu wa maandishi) au kwa tangazo katika gazeti la kila siku au la kila wiki au kwenye tovuti yetu au njia nyingine yoyote. Unashauriwa pia kutembelea tovuti yetu mara kwa mara ili kuona mabadiliko yote yaliyofanyika kwa sababu zisizotarajiwa unaweza kuwa hujapata taarifa.
   • 10.2 Unaweza kusitisha Masharti ya Matumizi/Huduma kwa kuacha kutumia Huduma hizi li>

   11. Maelezo ya Jumla
   • 11.1 Hatutahusika kwa kuchelewesha au kushindwa kutekeleza majukumu yetu yoyote yanayohusu matumizi ya Huduma hizi ikiwa kuchelewesha au kushindwa huko kumetokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu wa kutoa Huduma hiyo.
   • 11.2 Huwezi kubadili Masharti haya ya Matumizi na huwezi kuhamisha vigezo hivi kwa mtu au biashara nyingine.
   • 11.3 Masharti haya ya Matumizi yataongozwa na kufasiriwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
   • 11.4 Hatutahusika na hasara isiyo ya moja kwa moja na au inayotarajiwa.
   • 11.5 Mawasiliano yote kuhusu Vigezo na Masharti haya yatafanyika kwa Kiingereza au Kiswahili.
   • 11.6 Huduma kwa Wateja
   • 11.6.1 Unaweza kuwasiliana nasi kupitia kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa kupiga namba 100 au njia nyingine za mawasiliano ya huduma kwa wateja zinazopatikana katika mitandao yetu ya kijamii au Tovuti (yaani TOBi Online au Kutuma maoni) kutoa taarifa kuhusu migogoro, madai au tofauti zozote zinazojitokeza katika Huduma hizi.
   • 11.6.2 Wawakilishi wetu wa huduma kwa wateja watashughulikia masuala yaliyowasilishwa kwa kwa mujibu wa taratibu zetu za kushughulikia malalamiko zinazopatikana katika maduka na tovuti.
   • 11.6.3 Tunaweza kurekodi au kufuatilia simu zinaopigwa kwenye Vituo vyetu vya Huduma kwa Wateja au kufanya mawasiliano nawe kwa malengo ya kutoa mafunzo, kuwezesha uthibitishaji wa maelekezo na kutathmini kama viwango vyetu vya huduma vinafikiwa.
   • 11.7 Tunaweza kuhamishia kwa mtu mwingine yeyote sehemu au haki zote na/au majukumu kwa mujibu wa Masharti ya Matumizi baada ya kukuarifu. Pamoja na hayo, haki zako za kisheria hazitaathiriwa na majukumu yako hayataongezeka kutokana na uhamishaji huo. Hutaweza kuhamisha haki na wajibu wako kwa mujjibu wa Masharti ya Matumizi.

   12. Mawasiliano na Malalamiko
   • 12.1 Ikiwa unataka kupata taarifa zaidi piga simu kupitia huduma kwa wateja kama ilivyoelezwa hapo juu.
   • 12.2 Ikiwa hujaridhika kwa lolote kuhusiana na huduma zinazotolewa, tafadhali wasiliana na Kituo cha Huduma kwa Wateja. Watafurahi kukusaidia na kukufafanulia taratibu za kushughulikia malalamiko kwa undani. Tutajitahidi kushughulikia malalamiko yako mapema iwezekanavyo. Hata hivyo, mara nyingi malalamiko yatapaswa kufanyiwa uchunguzi. Kama hivyo ndivyo, tutakupa mrejesho ndani ya siku 7 za Kazi kuthibitisha upokeaji wa malalamiko yako na muda wa kuyashughulikia. Ikiwa malalamiko yako hayatapata ufumbuzi, utashauriwa namna ya kufanya..

VIGEZO NA MASHARTI YA VIFURUSHI VYA KUZURU (ROAMING)

1. Fasili;;
 • 1.1 Kuzuru (roam) ni huduma za kupiga simu, kutuma ujumbe wa simu wa maandishi na data ambazo zinazopatikana Mteja anapokuwa nje ya nchi tu.
 • 1.1.1 Kuna aina nne za vifurushi vya Kuzuru kama ifuatavyo:
 • 1.1.1.1 Kifurushi cha kuzuru kilichojumuishwa cha . Hiki kinatoa huduma yadakika za kupiga na kupokea simu, ujumbe wa simu wa maandishi na data
 • 1.1.1.2 Kifurushi cha Kuzuru cha Jamii. Hiki ni kwa ajili ya matumizi ya Facebook na WhatsApp tu
 • 1.1.1.3 Kupiga na kupokea simu tu. Kifurushi hiki kinatoa dakika kwa ajili ya kupiga na kupokea simu tu ukiwa nje ya nchi. Kupokea simu nje ya Tanzania kunatozwa, kwa hiyo, kifurushi hiki kinatoa dakika za kupokea simu.
 • 1.1.1.4 Data tu. Kifurushi hiki kinatoa data tu ukiwa nje ya nchi
 • 1.1.2 Vifurushi vya Kuzuru vinapatikana katika mitandao yote nje ya nchi au katika mitandao maalum katika nchi inayotembelewa.
 • 1.1.2.1 Kwa mitandao yote katika nchi inayotembelewa, Mteja anaweza kujiunga na aina yoyote ya kifurushi kama ilivyobainishwa hapo juu isipokuwa Kifurushi cha Kuzuru cha Jamii.
 • 1.1.2.2 Kwa mitandao maalum katika nchi inayotembelewa, Mteja anaweza kujiunga na kifurushi chochote hapo juu na lazima aendelee kutumia mtandao huo.
 • 1.2 Lipa Kadiri Unavyotumia ni gharama/tozo zinazotozwa unapotumia Huduma bila kifurushi

2. Matumizi
 • 2.1 Vigezo na Masharti haya yatatambuliwa humu kama “Vigezo na Masharti/Masharti ya Matumizi” (dhana hizi zitatumika kwa kubadilishana) yametolewa na Vodacom Tanzania PLC (Itatumika/kutambulika kama “Vodacom” au “sisi” au “sisi wenyewe” au “yetu”) kwa ajili ya kutumiwa na watumiaji/wateja wa Vodacom (“Mteja”) (Itatumika/kutambulika kama “wewe” au “yako” au “mtumiaji” “wewe mwenyewe”) ambao hutumia vifurushi vya Kuzuru (“Huduma”).
 • 2.2 Tafadhali soma Vigezo na Masharti haya, na Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Watumiaji wa Vodacom ambayo ni sehemu ya Vigezo na Masharti haya, yanayopatikana katika tovuti ya Vodacom. Kwa madhumuni ya Vigezo na Masharti yaliyoelezwa katika waraka huu, Vigezo na Masharti haya yatazingatiwa katika matukio yoyote ya migongano baina ya Vigezo na Masharti haya na Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Watumiaji wa Vodacom..

3. Tozo/Gharama, Kujiunga na Aina ya Huduma
  • 3.1 Huduma hii inapatikana kwa Wateja wa malipo ya kabla, Wateja mseto na Wateja wa malipo ya baada ya matumizi
  • 3.2 Wateja wanaweza kununua au kujiunga na Huduma hii wakiwa nchini Tanzania au nje ya Tanzania. Hata hivyo, ikitokea unanunua vifurushi ukiwa Tanzania, unashauriwa kufuata muda wa matumizi wa kifurushi au ratiba ya safari Yako ili kuepuka kuishiwa kifurushi hicho ukiwa safarini.
  • 3.3 Vifurushi vya Kuzuru vinaweza kununuliwa kupitia njia zote za Vodacom kama vile kutumia menyu ya USSD kwa nambari (*149*71#), App ya My Vodacom (My Vodacom App), tovuti ya Vodacom Tanzania na, vifurushi> Kuzuru
  • 3.4 Wateja wanaweza kutumia na kufurahia Huduma hizi wakiwa nje ya Tanzania baada ya kujiunga.
  • 3.5 Huduma hizi zinaweza kununuliwa kupitia muda wa maongezi au Mpesa
  • 3.6 Unawaeza kununua vifurushi vya Kuzuru kwa ajili yako mwenyewe au kumnunulia mtu mwingine
  • 3.7 Gharama zote za vifurushi vya kuzuru pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) zinapatikana katika tovuti ya Vodacom https://www.vodacom.co.tz/.
  • 3.8 Unaweza kujiunga na zaidi ya kifurushi kimoja muda wowote.
  • 3.9 Unaweza kuangalia salio la kifurushi chako bure kwa kupiga *149*60# au salio la muda wa maongezi kwa kupiga *102#. Huduma hii inapatikana pia ukiwa nje ya nchi..

  4. Maelezo kuhusu Mpangilio wa Huduma Yako
  • 4.1 Ikiwa wewe ni mteja wa malipo ya kabla, unapaswa kuhakikisha kuwa una muda wa maongezi wa kutosha katika simu yako. Inategemeana na mahitaji na matumizi yako ukiwa unazuru. Pia, unaweza kuweka kikomo cha matumizi ya data.
  • 4.2 Ikiwa wewe ni mteja wa malipo ya baada ya matumizi, unapaswa kuwasiliana na meneja wako wa akaunti ili ahuishe huduma za kuzuru ukiwa nje ya nchi..

  5. Matumizi Nje ya Kifurushi/Lipa Kadiri Unavyotumia
  • 5.1 Tozo au gharama za Lipa Kadiri Unavyotumia zitatumika ikiwa Mteja atatumia Huduma bila ya kuwa na kifurushivifurushi katika nchi fulani au kutumia Huduma hizi kwa nchi ambazo mtandao wa Vodacom haujaanzisha vifurushi. Viwango na tozo za kawaida za nje ya vifurushi zitatumika kama ilivyofafanuliwa katika tovuti ya Vodacom.
  • 5.2 Viwango vya Lipa Kadiri Unavyotumia kwa wateja wa kimataifa na wanaozuru nchi za nje vinatofautiana kulingana na nchi.
  • 5.3 Ni wajibu wa Mteja kujijuza na viwango na tozo zinazotumika kwa huduma za kuzuru za Vodacom. Viwango na tozo hizo zinaweza kubadilika wakati wowote.
  • 5.4 Daima tembelea tovuti ya Vodacom Tanzania https://vodacom.co.tz au wasiliana na Huduma kwa Wateja kwa kupiga namba 100 ukiwa ndani ya Nchi au +255754700000 kupiga bure ukiwa nje ya Nchi, kwa ajili ya kujua viwango na tozo mpya. Pia, mteja anaweza kutumia nambari ya WhatsApp ifuatayo: +255754100100
  • 5.5 Gharama/Tozo za Lipa Kadiri Unavyotumiazinategemeana na mtandao wa nchi inayotembelewa, ili kupata tozo za chini hakikisha unatumia huduma ya kuzuru katika mitandao ya Vodacom, Safaricom au mitandao wabia wa Vodafone. Hata hivyo, unashauriwa kuweka vizuri mipango yako kabla ya safari na kutafuta mitandao unayoweza kuimudu ili utumie huduma ya kuzuru, hasa katika nchi ambazo hazina mtandao wa Vodacom au Vodafone.
  • 5.6 Mitandao inayoendana na Vodacom hapa barani Afrika ni “Vodacom” katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Msumbiji, Lesotho na Afrika Kusini, na Safaricom nchini Kenya. Pia, barani Ulaya Vodacom inajulikana kama “Vodafone” katika nchi za Albania, Jamhuri ya Cheki, Ujerumani, Ugiriki, Hungaria, Irelandi/Ayalendi, Italia, Malta, Uholanzi, Nyuziland, Ureno, Romania, Hispania, Uturuki na Uingereza. Pia barani Afrika katika nchi za Ghana na Misri.
  • 5.7 Ikiwa Mteja ataishiwa kifurushi au akiwa hajajiunga na kifurushi chochote cha kuzuru na anapokea simu akiwa nje ya nchi, atakatwa muda wake wa maongezi.
  • 5.8 Ukiwa nje ya nchi bila kifurushi cha kuzuru, muda wa kulipia/matumizi ya dakika na data vinategemeana na makubaliano tuliyo nayo na mbia wetu. Mteja anaweza kuomba taarifa hii bure kutoka katika duka lolote la Vodacom, dawati la huduma, meneja wa akaunti, au piga simu huduma kwa wateja namba 100 ukiwa Tanzania au +255754700000 ukiwa nje ya Tanzania..

  Muda wa Matumizi ya Vifurushi vya Kuzuru
  • 6.1 Muda wa Matumizi wa kifurushi ni muda ambao kifurushi kitakuwa halali kutumika
  • 6.2 Vifurushi vya siku vitatumika kwa saa 24 kuanzia muda viliponunuliwa
  • 6.3 Vifurushi vya wiki vitatumika kwa siku 7 kuanzia tarehe viliponunuliwa
  • 6.4 Vifurushi vya mwezi vitatumika kwa siku 30 kuanzia tarehe viliponunuliwa
  • 6.5 Mara baada ya kutumia kifurushi chako ndani ya muda halali au kifurushi chako kikiisha muda wake, viwango vya nje ya kifurushi vitatumika
  • 6.6 Unaweza kununua kifurushi kingine chenye chenye muda uleule wa matumizi au tofauti katika muda wowote. Kipaumbele cha matumizi kitatolewa kwa kifurushi kilichonunuliwa awali. Pale ambapo muda wa matumizi wa vifurushi vinavyonunuliwa baadaye ni mfupi kuliko vile vilivyonunuliwa hapo kabla, kipaumbele cha matumizi kitaelekezwa kwenye kifurushi cha muda mfupi.
  • 6.7 Wateja hawataweza kutumia kifurushi kilichoisha muda wake. Kifurushi kisichotumika kitaingizwa katika kifurushi kingine ikiwa utajiunga na kifurushi kingine kabla ya muda wa kifurushi cha awali kuisha. Ukijiunga na kifurushi kipya baada ya kile cha awali kuisha muda wake, kifurushi kisichotumika hakitakuwa halali na huduma zote za kifurushi hicho zitasitishwa baada ya muda wake kuisha..

  7. Muda wa Matumizi na Spidi
  • 7.1 Vifurushi vyote vya kuzuru vinaweza kutumika muda wowote wa siku ndani ya muda wake halali.
  • 7.2 Pia, hakikisha unatumia mtandao wa nchi husika kama ilivyoelezwa kwenye kifurushi ili ufurahie kifurushi chako. Hata hivyo, ikiwa hakuna mtandao maalumu wa nchi husika uliooneshwa, Unaweza kutumia kifurushi kwa mtandao wowote wa simu katika nchi uliyoitembelea.

   • 8. Kujiunga na Huduma ya Kuzuru
    • 8.1 Wakati wa kuzuru, simu yako itachagua na kujiunga na mtandao wa nchi hiyo kiotomati kulingana na masharti ya mtandao huo.
    • 8.2 Ikiwa simu yako haijajiunga na mtandao wowote, zima simu yako kisha iwashe tena (washa tena simu). Ikiwa simu yako haitajiunga na mtandao wowote baada ya kuiwasha tena, unaweza kuchagua mtandao mwenyewe kwa kufuata hatua zifuatazo:
    • 8.2.1 Kama unatumia IPhone nenda settings >> mobile data >>Network selections >> choose your preferred network to roam with the roaming partners / networks.
    • 8.2.2 Kama unatumia Android nenda settings >> connections >>Mobile Networks >>Networks operators>> choose your preferred network to roam with the roaming partners / networks..

    9. Huduma Zinazopatikana Ukiwa Nje ya Nchi
    • 9.1 Ukiwa nje ya nchi na unatumia mitandao ya simu nchi hizo, unaweza kutumia intaneti, kupiga na kupokea simu, kutuma na kupokea ujumbe wa simu wa maandishi, kutumia M-Pesa, kama ambavyo ungetumia Tanzania.
    • 9.2 Si huduma zote zinazopatikana kwa wateja wenye mikataba na Vodacom/wateja wa malipo baada ya matumizi zinapatikana pia kwa wateja mseto na Wateja wa malipo yaa kabla.
    • 9.3 Hata hivyo, huduma zote hapo juu katika kifungu 9.1 zinaweza zisipatikane katika mitandao yote ya kigeni kwa pamoja wakati wa kuzuru. Baadhi ya huduma zinaweza kupatikana katika mtandao mmoja. Kwa mfano, unaweza kupata huduma za kupiga simu na kutuma ujumbe tu lakini usipate data.
    • 9.4 Upatikanaji wa huduma unategemeana na mkataba tulio nao na wabia wetu na ukubwa wa eneo la mtandao wao. Wakati mwingine, huduma hizi zinapatikana kwa Wateja wa malipo baada ya matumizi lakini si kwa wateja wa malipo ya kabla.
    • 9.5 Ikiwa unashindwa kutumia huduma ya kuzuru nje ya nchi, fanya yafuatayo: 9.5.1 Hakikisha simu yako inaonesha mtandao wa mbia uliyechagua katika nchi unayotembelea. (Angalia wabia wetu nchi za nje katika nchi unayoitembelea katika tovuti yetu (www.vodacom.co.tz)
    • 9.5.2 Hakikisha mipangilio (settings) ya simu yako imewekwa vizuri ili kukuwezesha kuzurunchi za nje. Kwa mfano, washa data katika sehemu ya Data Roaming katika simu/kifaa kila mara unapotaka kutumia intaneti.
    • 9.5.3 Hakikisha una muda wa kutosha wa maongezi au umejiunga na kifurushi sahihi.
    • 9.5.4 Kwa tatizo lolote ukiwa nje ya Tanzania, tupigie bure +255754700000 au Wasiliana nasi kwa nambari hii ya WhatsApp +255754100100.

    10. Mshtuko wa Gharama/Kikomo cha Kutumia Data
    • 10.1 Kwa kutambua gharama kubwa za kutumia simu nje ya nchi, Vodacom imekuwezesha kuweka kikomo cha juu cha matumizi ya data ukiwa unatumia simu. Hili linatokana na ukweli kuwa unaweza kulipia tozo za data hata kama hununui au hupakui chochote kwa sababu simu hutumia data kidogo kila baada ya sekunde chache katika tovuti/programu za simu (mfano, kuhuisha tovuti, matangazo yanayopelekwa nyuma n.k.).
    • 10.2 Tafadhali, hakikisha kwamba unafunga programu zote za simu ambazo huzitumii ukiwa nje ya nchi. Vodacom haihuisiki na upakuaji wowote wa data usiodhamiriwa unaoweza kufanywa na simu yako.

    11. Vigezo na Masharti Mengine Yanayotumika
    • 11.2 Iwapo itatokea mkinzano, mpishano au mgongano kwa vigezo na masharti haya na Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Watumiaji wa Vodacom kwa Mteja Aliyejiunga, kulingana na umuhimu na matumizi Vigezo na Masharti haya yatazingatiwa yakifuatiwa na Vigezo na Masharti ya Jumla ya Mtumiaji wa Vodacom.
    • 11.3 Mtumiaji au Mteja yeyote anayetumia Huduma zinazotolewa chini ya Vigezo na Masharti haya atachukuliwa kuwa amesoma na kuelewa Vigezo na Masharti husika.
    • 11.4 Tuna haki ya kusitisha Huduma hizi ikiwa:
    • 11.4.1 utatumia Huduma kwa malengo yoyote yasiyoruhusiwa;
    • 11.4.2 tutabaini matumizi mabaya, kukiuka maudhui, vitendo vya udanganyifu au jaribio la udanganyifu linalohusiana na matumizi yako ya Huduma hii;
    • 11.4.3 tutatakiwa au kuombwa kufanya hivyo ili kutekeleza amri au maelekezo au mapendekezo kutoka serikalini, mahakamani, kwa mdhibiti au mamlaka zozote halali;
    • 11.4.4 tutatilia shaka au kujiridhisha kuwa umekiuka Masharti haya ya Matumizi;
    • 11.4.5 tutatakiwa kufanya hivyo ili kutatua matatizo ya kiufundi au kwa sababu za kuhakikisha usalama baada ya kukupa taarifa za kusitisha huduma hii;
    • 11.4.6 kutakuwa na haja ya kusaidia kuhuisha au kuboresha maudhui au utekelezaji wa Huduma hizi mara kwa mara muda baada ya kukupa taarifa za kusitisha huduma hii;
    • 11.4.7 tutaamua kusitisha kwa muda au kuacha kutoa Huduma hii kwa sababu za kibiashara au kwa sababu nyingine yoyote kama itakayoturidhisha.

    12. Kusitisha Kutoa Huduma
    • 12.1 Huwezi kukatisha matumizi ya Huduma hii baada ya kujiunga na kifurushi kabla ya muda wa matumizi yake kuisha. Huduma hii zitasitishwa baada ya muda wa matumizi ya kifurushi kuisha.

    13. Mabadiliko katika Vigezo na Masharti haya
    • 13.1 Tunaweza kuongeza au kubadili Vigezo na Masharti haya ya Matumizi kulingana na kifungu cha 13.2. Tunaweza kuongeza ada na tozo mpya au kubadili ada na tozo zilizopo wakati wowote; kutokana na sheria mpya, kanuni za kisheria, kanuni za Serikali au matakwa ya leseni, viwango vya kubadili fedha, kuanzishwa au kubadilishwa kwa kodi ya serikali au kutokana na mapitio yoyote ya mipango ya kibiashara ya Vodacom, mabadiliko ndani ya tasnia, mapendekezo kutoka vyombo vya usimamizi au kutokana na sababu nyingine itakayojitokeza.
    • 13.2 Tutakuarifu mapema ikiwa tunataka kuongeza au kubadili vigezo na masharti haya au ikiwa tunataka kuongeza ada na tozo mpya au kubadili zilizopo wakati au baada ya kujiunga na Huduma hizi. Kiasi cha malipo na aina ya taarifa tutakayokupa zitapitia njia mwafaka zinazotumika na kupatikana kwa wakati huo kwa mfano, tunaweza kukutaarifu kwa barua, barua pepe, simu (ikiwa ni pamoja na ujumbe uliorekodiwa au ujumbe mfupi wa simu wa maandishi) au kwa matangazo katika gazeti la kila siku au kila wiki au katika tovuti yetu au njia nyingine yoyote). Unashauriwa pia kutembelea tovuti yetu mara kwa mara ili kuona mabadiliko hayo kama kwa sababu zisizotarajiwa inawezekana hukupata taarifa za hizo.
    • 13.3 Ikiwa hukubaliani na mabadiliko au nyongeza katika Vigezo na Masharti haya, unaweza kusitisha huduma hizi kwa mujibu wa kifungu cha 14 hapo chini. Ikiwa wewe hujatutaka tusitishe Masharti ya Matumizi na bado unatumia Huduma hizi, utachukuliwa kuwa umekubali mabadiliko hayo tangu yalipoanza kutekelezwa.

    14. Kusitisha Huduma na au Masharti ya Huduma
    • 14.1 Tunaweza kusitisha Masharti haya ya Matumizi wakati wowote tutakapoamua. Usitishaji huo utafanyika baada ya kukupa Taarifa. Taarifa inaweza kuwa kwa barua, baruapepe, simu (ikiwa ni pamoja na ujumbe uliorekodiwa au ujumbe mfupi wa simu wa maandishi) au kwa tangazo katika gazeti la kila siku au la kila wiki au kwenye tovuti yetu au njia nyingine yoyote. Unashauriwa pia kutembelea tovuti yetu mara kwa mara ili kuona mabadiliko yote yaliyofanyika kwa sababu zisizotarajiwa unaweza kuwa hujapata taarifa.
    • 14.2 Unaweza kusitisha Masharti ya Matumizi/Huduma kwa kuacha kutumia Huduma hizi

    15. Maelezo ya Jumla
    • 15.1 Hatutahusika kwa kuchelewesha au kushindwa kutekeleza majukumu yetu yoyote yanayohusu matumizi ya Huduma hizi ikiwa kuchelewesha au kushindwa huko kumetokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu wa kutoa Huduma hiyo.
    • 15.2 Huwezi kubadili Masharti haya ya Matumizi na huwezi kuhamisha vigezo hivi kwa mtu au biashara nyingine.
    • 15.3 Masharti haya ya Matumizi yataongozwa na kufasiriwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
    • 15.4 Hatutahusika na hasara isiyo ya moja kwa moja na au inayotarajiwa.
    • 15.5 Mawasiliano yote kuhusu Vigezo na Masharti haya yatafanyika kwa Kiingereza au Kiswahili.
    • 15.6 Huduma kwa Wateja
    • 15.6.1 Unaweza kuwasiliana nasi kupitia kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa kupiga namba 100 au njia nyingine za mawasiliano ya huduma kwa wateja zinazopatikana katika mitandao yetu ya kijamii au Tovuti (yaani TOBi Online au Kutuma maoni) kutoa taarifa kuhusu migogoro, madai au tofauti zozote zinazojitokeza katika Huduma hizi.
    • 15.6.2 Wawakilishi wetu wa huduma kwa wateja watashughulikia masuala yaliyowasilishwa kwa kwa mujibu wa taratibu zetu za kushughulikia malalamiko zinazopatikana katika maduka na tovuti.
    • 15.6.3 Tunaweza kurekodi au kufuatilia simu zinaopigwa kwenye Vituo vyetu vya Huduma kwa Wateja au kufanya mawasiliano nawe kwa malengo ya kutoa mafunzo, kuwezesha uthibitishaji wa maelekezo na kutathmini kama viwango vyetu vya huduma vinafikiwa.
    • 15.7 Tunaweza kuhamishia kwa mtu mwingine yeyote sehemu au haki zote na/au majukumu kwa mujibu wa Masharti ya Matumizi baada ya kukuarifu. Pamoja na hayo, haki zako za kisheria hazitaathiriwa na majukumu yako hayataongezeka kutokana na uhamishaji huo. Hutaweza kuhamisha haki na wajibu wako kwa mujjibu wa Masharti ya Matumizi.

    16. Mawasiliano na Malalamiko
    • 16.1 Ikiwa unataka kupata taarifa zaidi piga simu kupitia huduma kwa wateja kama ilivyoelezwa hapo juu.
    • 16.2 Ikiwa hujaridhika kwa lolote kuhusiana na huduma zinazotolewa, tafadhali wasiliana na Kituo cha Huduma kwa Wateja. Watafurahi kukusaidia na kukufafanulia taratibu za kushughulikia malalamiko kwa undani. Tutajitahidi kushughulikia malalamiko yako mapema iwezekanavyo. Hata hivyo, mara nyingi malalamiko yatapaswa kufanyiwa uchunguzi. Kama hivyo ndivyo, tutakupa mrejesho ndani ya siku 7 za Kazi kuthibitisha upokeaji wa malalamiko yako na muda wa kuyashughulikia. Ikiwa malalamiko yako hayatapata ufumbuzi, utashauriwa namna ya kufanya.

Nunua Kifurushi cha Kimataifa


Nunua Kifurushi cha Kuzuru


Viwango vya kuzuru

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa