Miongozo kwa ufadhili

Walengwa: Jamii zisizojiweza

Vipaumbele: Elimu Shirikishi, Hatua Shirikishi za Tabianchi, Ukuaji Shirikishi

Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation itazingatia kufanya kazi na taasisi zifuatazo:

 • • Mashirika yasiyo ya Serikali (NGOs)
 • • Mashirika yasiyo ya faida (NPO)
 • • Mashirika na taasisi za jumuiya zinazotambuliwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mapendekezo au maombi yafuatayo hayatazingatiwa na Taasisi

 • • Gharama za uendeshaji / utawala kwa mashirika
 • • Mikutano / semina
 • • Uchangishaji
 • • Ziara ya kujifunza au mipango ya kubadilishana wanafunzi
 • • Utafiti
 • • Fursa za michezo na mashindano
 • • Miradi ya dini au kitamaduni
 • • Miradi kutoka / kushikamana na vyama vya siasa
 • • Maombi ya mtu mmjoja/ binafsi
 • • Maeneo nje ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 • • Mambo mengine yanayohusiana na hapo juu.

Ubia
Taasisi itaamua kushirikiana na Shirika lisilo la Serikali yenye sifa nzuri kwa kufanikisha baadhi ya mamlaka yake

Uwasilishaji wa programu
Maombi yanaweza kuwasilishwa moja kwa moja Vodacom Tanzania HQ - Mlimani city Park Jengo na 1, au kwa posta S.L.P 2369 Dar es Salaam, au barua pepe oswalds@vodacom.co.tz

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa