Intaneti FAQs

1.4G ni nini?

4G ni kizazi cha nne katika teknolojia ya mitandao ya simu za mikononi yenye kasi mara kumi Zaidi ya 3G

2.Nini faida za kutumia 4G?

 • Internet ya 4G ni nzuri na ya kasi mara kumi zaidi ya 3G
 • Ubora wa kupiga/ kupokea simu ni mzuri Zaidi
 • Kuna bando za kipee za 4G ambazo ni mara mbili zaidi ya bando za kawaida za internet.
 • Matumizi kwa ujumla ya simu yenye 4G ni bora zaidi.

3.Nani anastahili kupata huduma ya 4G?

Wateja wote walio maeneo ambao mtandao wa 4G umewezeshwa (Tanga, Dar es Salaam & Morogoro) wanastahili kupata huduma hii

Wanatakiwa wawe na simu/modem zenye uwezo wa 4G zikiwa na laini za 4G.

4.Je mteja atajuaje kuwa yuko kwenye eneo lenye 4G

Mteja ataona simu au kifaa anachotumia kimeonesha alama ya 4G kwenye alama ya mtandao. Kwa maelekezo zaidi angalia picha hapa chini kwenye mzunguko mwekundu

5.Nina laini ya 4G lakini bado napata mawasiliano ya 3G?

 • Angalia kama simu au kifaa unachotumia kina uwezo wa 4G ( setting – network)
 • Angalia kama 4G imewezeshwa kwenye simu au kifaa chako.
 • Hakikisha kama laini ilio ndani ya simu/kifaa chako ni ile ya 4G
 • Angalia kama mteja yuko kwenye eneo lililo ya mawasiliano ya 4G.

6.Je wateja wanawezaje kujua kama simu au vifaa walivyonavyo vina uwezo wa 4G

 • Wateja wanatakiwa waende kwenye setting kisha nework kutegeme simu au kifaa wanachotumia. Mfano:
 • Settings – Network – Cellular – Voice & Data (IPhone) Settings – Mobile network – Network mode (Samsung) Settings – Mobile data – Network mode (Lenovo)
 • Au watumie tovuti kupata taarifa za uwezo wa simu
 • i.Piga *#06# kupata namba ya IMEI(International Mobile Equipment Identity). ii.Kisha ingia na peruzi kwenye http://www.imei.info/
  iii.Ingiza IMEI namba na kisha bonyeza “Check”.

Taarifa za simu au kifaa chako zitaonekana kama hapo chini.

4G/LTE ikionekana kama kwenye picha chini, Simu/ Kifaa chako kina uwezo wa 4G.

7.Kwa simu za laini mbili, laini gani inafanya kazi vizuri?

Laini ya kwaza inafanya kazi vizuri zaidi.

8. Je ukubwa na gharama za vifurushi vya 4G ni zipi?

Bando za 4G Pekee

Muda wa matumizi Bei Kifurushi cha Intaneti Usiku pekee
Saa 24 Tsh 500 70MB 70MB
Tsh 1000 200MB 200MB
Tsh 2000 1GB 1GB
Siku 7 Tsh 3000 500 MB 500 MB
Tsh 5000 1GB 1GB
Tsh 8000 2GB 2GB
Tsh 15000 10GB 10GB
Siku 30 Tsh 5000 500MB 500MB
Tsh 15000 2GB 2GB
Tsh 35000 10GB 10GB
Tsh 50000 20GB 20GB
Tsh 95000 30GB 30GB

Gharama za Malipo kabla ni Tsh 282 kwa MB

Kiwango cha chini cha malipo kwa uniti kwa matumizi kwa Malipo kabla ni kwa KB 150

Kiwango cha chini cha malipo kwa uniti kwa Intaneti ya Malipo Kabla ni kwa KB 100

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa