Self Service

1. Vifurushi vya Cheka Bombastik ni nini?

Vifurushi vya Cheka Bombastik ni vifurushi vya Vodacom vinavyowawezesha wateja kupiga simu, kutuma SMS na kutumia intaneti kwa gharama nafuu. Vifurushi hivi vinaweza kununuliwa wakati wowote( ikiwa pamoja na siku za mapumziko au mwisho wa wiki).

2. Kuna aina ngapi ya vifurushi vya Cheka Bombastik?

i. Mitandao yote: Hivi ni vifurushi vyenye dakika za kupiga simu (Vodacom kwenda mitandao mingine nchini), SMS za ndani ya nchi na vifurushi vya intaneti.

ii. Vodacom – Vodacom. Hivi ni vifurushi vyenye dakika za kupiga simu( Vodacom kwenda Vodacom), SMS za ndani ya nchi na vifurushi vya intaneti.
iii. Cheka Zogo – Hivi ni vifurushi vyenye dakika za kupiga simu (Vodacom kwenda Vodacom na mitandao mingine, mteja anaweza kuona aina tofauti ya Cheka zogo kutegemeana eneo alilopo.

3. Ni wateja gani wanaweza kutumia Cheka Bombastik?

Wateja wa malipo kabla wanaweza kutumia Cheka Bombastik na Cheka Zogo

4. Je ni vipi vifurushi vya Cheka Bombastik na Cheka Zogo?

Vifurushi vya Cheka Bombastik na Cheka Zogo ni kama ifuatavyo;
Cheka Voda-Voda
Itadumu kwa Bei(Tsh) Voda-Voda Min Mtandao wote Min SMS Intaneti(MB)
24 Masaa 495 19 1 10
500 14 2 40 1
600 30 2
645 30 5 20
650 30 2 100 3
995 50 10 40
1000 50 5 Bila kikomo 10
7 Siku 2000 45 5 200 20
2800 75 5 300 30
4000 130 5 500 50
7000 240 5 1000 50
10000 360 5 1000 80
30 Siku 10000 280 20 1000 100
15000 450 20 1500 250
20000 750 20 2000 250
30000 1300 20 3000 250
50000 2300 20 5000 250

Cheka Mitandao Yote
Itadumu kwa Bei(Tsh) Voda-Voda Min Mtandao wote Min SMS Intaneti(MB)
24 Masaa 499 7 40 1 MB
649 12 100 3 MB
999 22 Bila kikomo 10 MB
7 Siku 1999 25 200 20 MB
4999 73 500 50 MB
10000 200 1000 400 MB
30 Siku 9999 135 1000 100 MB
14999 210 1500 250 MB
19999 340 2000 250 MB
30000 600 3000 3 GB
50000 1000 7000 7 GB
95000 2500 30 1500 20 GB

Gharama zote za kupiga simu nje ya vifurushi na bonga ni kama ifuatavyo: Vodacom Tsh 45 kwa sek siku nzima na Vodacom kwenda mitandao mingine ni Tsh 5.5 kwa sek

Gharama ya SMS zote zinatotumwa Tanzania ni Tsh 50 kwa SMS kwenda mtandao wowote

Gharama ya kuperuzi intaneti nje ya vifurushi ni Tsh 0.26 kwa kb

Gharama zote ni bila kodi na Bonga ni Tsh 2 kwa sek kwa mitandao yote siku nzima

5. Ni namna gani wateja wanaweza kununua vifurushi vya Cheka Bombastik na Cheka Zogo?

Wateja wanaweza kununua vifurushi vya Cheka bombastic na Zogo kwa kupiga *149*01#

6. Ni namna gani wateja wataangalia salio la vifurushi?

Kuangalia salio, wateja watapiga *149*60#.

7. Je inawezekana kununua kifurushi zaidi ya kimoja kwa siku?

Ndio. Ununuzi wa kifurushi zaidi ya kimoja unaruhusiwa ambapo dakika, intaneti na SMS zitahamia kwenye kwenye kifurushi kipya na salio litakuwa jumla ya kifurushi kipya na cha zamani cha namna moja. Muda wa mwisho wa matumizi utakuwa wa kifurushi kipya.

8. Je mteja ataruhusiwa kununua huduma nyingine wapo kwenye vifurushi vya Cheka Bombastik?

Ndio.Wateja wataruhusiwa kununua huduma nyingine wakiwa kwenye Cheka

9. Je ni umuhimu upi unapewa kwenye matumizi mteja napokuwa na huduma nyingine za maongezi, SMS na huduma ya intaneti?

Umuhimu kwenye matumizi unapewa vifurushi vya Cheka kwanza.

10. Je mteja anaweza kuwanunulia marafiki au wenzi wao vifurushi vya Cheka Bombastik/Cheka Zogo?

Ndio, Mteja anaweza kuinunulia namba yoyote ya Vodacom vifurushi vya Cheka Bombastik na Cheka Zogo kwa kupiga *149*01# , chagua CHEKA + Zogo, chagua kifurushi, kisha chagua mnunulie mwingine
Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa