Kuhamisha Pesa Kimataifa

Money Gram

Vodacom kwa kushirikiana na MoneyGram tunakuwezesha kupokea pesa kutoka ulimwenguni kote kupitia mtandao mpana wa mawakala zaidi ya 350,000 wa MoneyGram wanaopatikana nchi zaidi ya 200 duniani kote. Anachotakiwa kufanya anayekutumia pesa ni kutembelea tawi au wakala wa Moneygram akiwa na kiasi anachohotaji kukutumia kikiwa katika pesa ya nchi husika. Mtumaji atampa wakala wa MoneyGram namba yako ya Vodacom M-Pesa na pesa itatumwa moja kwa moja na wakala kwenye akaunti yako ya M-Pesa ambapo utaweza kuitumia papo hapo popote Tanzania. Kwa maelezo zaidi ya jinsi ndugu na rafiki zako walio nje ya nchi wanavyoweza kukutumia pesa kupitia MoneyGram tembelea http://global.moneygram.com/en/send-to-a-mobile-wallet


Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa