Kuhamisha Pesa Kimataifa

Dunia kijiji na M-Pesa.

Vodacom, Vodacom, mtandao supa pekee Tanzania unakuweka karibu zaidi na ndugu na jamaa zako ulimwenguni kupitia M-PESA. Ukiwa na M-Pesa unaweza kutuma na Kupokea pesa PAPO HAPO kutoka nchi zaidi ya 200 kupitia washirika wetu ulimwenguni. Kwa Afrika unaweza kutuma au kupokea pesa kwenda/kutoka Safaricom M-Pesa, MTN Uganda, MTN Rwanda, MTN Zambia na EcoCash Burundi kwenda kwenye akaunti yako ya M-Pesa au kwenye simu ya umtumiaye. Pia wateja wa safaricom M-Pesa wanaweza kutoa pesa kwa mawakala wa Vodacom M-Pesa wanapozuru Tanzania.
Kupitia washirika wetu wa kimataifa MoneyGram, Juba Express na WorldRemit, M-Pesa inakuwezesha kupokea pesa moja kwa moja kwenye akaunti yako ya M-Pesa kutoka nchi zaidi ya 200 kutoka Ulaya, Marekani, Australia, Mashariki ya kati na Afrika bila makato yoyote.

Faida za huduma hii

  • Urahisi: Huna haja ya kutembea kwenda benki, Vituo vya mabasi au kwa mawakala ili kutuma na kupokea pesa kutoka nchi mbalimbali duniani. M-Pesa sasa inakuwezesha kutuma na kupokea pesa moja kwa moja kwenye akaunti yako ya M-Pesa kwa urahisi kupitia washirika wetu kama tulivyo taja apo juu.
  • Unafuu: Sasa unaweza kutuma pesa nje ya nchi kupitia M-Pesa kwa bei nafuu sana ukilinganisha na njia nyingine za kutuma pesa. Kupokea pesa kwa upande mwingine ni bure kabisa kwa mpokeaji.
  • Usalama: Kutuma au kupokea pesa kupitia M-Pesa ni salama zaidi kwasababu pesa hizo zinaingia kwenye akaunti ya M-Pesa ya mpokeaji moja kwa moja bila kupitia mikono mingine hivyo kuifanya kuwa njia salama zaidi ukilinganisha na njia nyingine kama kutuma pesa kupitia mabasi ya kusafiria au magari ya mizigo.
  • Uharaka: Kutuma na kupokea pesa ni PAPO HAPO kwenye akaunti yako ya M-Pesa au kwenye akaunti ya umtumiaye bila makato kwa mpokeaji.
  • Usawa: : Hakuna sababu ya anayetuma au kupokea pesa kwenda ofisi za ubadilishaji fedha bali kupitia M-Pesa unaweza kutuma au kupokea pesa katika sarafu ya Tanzania kisha mpokeaji atapokea pesa ikiwa katika sarafu ya nchini mwake.

Gharama zake ziko vipi?

   Gharama za kutuma pesa nje ya nchi ni sawa na zile zinazotumika kutuma pesa ndani ya nchini, hivyo kuifanya M-Pesa kuwa njia nafuu zaidi ya kutuma pesa kimataifa. Mpokeaji atapokea pesa moja kwa moja kwenye akaunti yake ya M-Pesa BURE.


Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa