Tanzania kwenda Kenya, Pesa ni M-Pesa

Vodacom, mtandao supa pekee Tanzania unakuweka karibu zaidi na jamaa waliopo Kenya kupitia M-PESA. Ukiwa na M-Pesa, Una uwezo wa kutuma na kupokea pesa kutoka Kenya papo kwa papo kwa ndugu, jamaa au marafiki wanaotumia Safaricom.Tuma Pesa kwenda Kenya kwa urahisi, usalama na haraka zaidi kuliko njia yoyote ya kutuma pesa. Kupitia huduma hii utafurahia kupokelewa au kutumwa haraka kwa pesa zako ukilinganisha na njia za kutuma pesa kwa basi au benki ambazo zinatumia masaa hadi siku kadhaa kwa pesa kuwafikia wahusika waliopo nchini Kenya au Tanzania.

International Money Transfer

 • Jinsi ya kutuma M-Pesa Kenya
 • Jinsi ya kutuma M-Pesa Tanzania
 • Huduma hii ina faida gani?
 • Gharama zake ziko vipi?

How to send money to M-Pesa Kenya

Mteja wa Vodacom Tanzania

 • 1. Piga *150*00# chagua TUMA PESA
 • 2. Chagua kwenda M-PESA KENYA
 • 3. Chagua TUMA PESA.(Angalia Kiwango cha Kubadilisha fedha kabla ya kutuma)
 • 4. Weka namba ya mpokeaji ukianza na +254...au 254...
 • 5. Weka KIASI unachotuma (katika Tshs.)
 • 6. Weka namba yako ya SIRI ya M-Pesa kisha Thibitisha muamala

Jinsi ya kutuma M-Pesa Tanzania

Huduma hii ina faida gani?

 • Ni rahisi: Hauhitaji kutembea kwenda benki, vituo vya mabasi au kwa mawakala ili kutuma pesa Kenya. Tuma pesa kwa urahisi ukiwa na simu yako ya mkononi wakati wowote na mahali popote.
 • Ni nafuu: Ina viwango nafuu vya ada ukilinganisha na njia nyingine zote za kutuma pesa.
 • Ni ya Uhakika: Pesa zinamfikia mtu unayemtumia moja kwa moja kwenye akaunti yake ya Safaricom M-Pesa.
 • Ni salama: M-Pesa ni salama zaidi ukilinganisha na njia nyingine kama mabasi au magari ya mizigo.
 • Ni haraka:Tofauti na njia nyingine, Mpokeaji nchini Kenya anapokea pesa haraka zikiwa katika shilingi ya Kenya.
 • Imeunganishwa: Hakuna haja ya kwenda katika Duka la kubadilishia fedha ili kubadili kwani mpokeaji anaipokea kwenye pesa ya nchi yake.

Gharama zake ziko vipi?

Gharama za kutuma pesa Kenya ni sawa na zile zinazotumika kutuma pesa nchini, hivyo kuifanya M-Pesa kuwa njia nafuu zaidi ya kutuma pesa Kenya.

Money Gram
Vodacom kwa kushirikiana na MoneyGram tunakuwezesha kupokea pesa kutoka ulimwenguni kote kupitia mtandao mpana wa mawakala zaidi ya 350,000 wa MoneyGram wanaopatikana nchi zaidi ya 200 duniani kote. Anachotakiwa kufanya anayekutumia pesa ni kutembelea tawi au wakala wa Moneygram akiwa na kiasi anachohotaji kukutumia kikiwa katika pesa ya nchi husika. Mtumaji atampa wakala wa MoneyGram namba yako ya Vodacom M-Pesa na pesa itatumwa moja kwa moja na wakala kwenye akaunti yako ya M-Pesa ambapo utaweza kuitumia papo hapo popote Tanzania. Kwa maelezo zaidi ya jinsi ndugu na rafiki zako walio nje ya nchi wanavyoweza kukutumia pesa kupitia MoneyGram tembelea http://global.moneygram.com/en/send-to-a-mobile-wallet

JUBA EXPRESS
Kupitia ushirikiano na Juba Express, unaweza kupokea pesa kutoka kwa ndugu na jamaa waliopo Australia, Uingereza, marekani, Canada, Sweden, Falme za kiarabu (U.A.E), Kenya, Uganda, Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini. Juba Express inatoa huduma salama na rahisi za kutuma pesa ambapo pesa huingia moja kwa moja kwenye akaunti yako ya M-Pesa na unaweza kuitumia papohapo kufanya malipo, kutuma n.k. kwa maelezo zaidi ya jinsi unavoweza kupokea pesa kimataifa kupitia Juba Express tembelea www.jubaexpress.com
Terms & Conditions for International Money Transfer

Hakimiliki © 2018 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa