Maswali yaulizwayo mara kwa mara

1. Ofa za Ya Kwako 2 ni nini?

Ofa za Ya Kwako 2 ni huduma inayowapatia wateja wa malipo ya awali wa Vodacom ofa kabambe za Vifurushi vya kupiga simu, Intaneti au SMS kwa gharama nafuu kabisa kulingana na tabia za matumizi binafsi ya kila mteja.

2. Ninapataje Ofa za Ya Kwako 2?

Ni rahisi kabisa, kupata Ofa Maalum, piga *149*03# kwa njia ya moja kwa moja au kupitia menyu kuu kwa kupiga *149*01# kisha chagua Ofa za Ya Kwako 2 ambapo utaona orodha ya Ofa kwaajili yako.

3. Wateja wa aina gani wanaweza kupata Ofa Maalum?

Ofa za Ya Kwako 2 ni kwa ajili ya wateja wote wa Vodacom wa malipo ya awali. Kama huna uhakika kama wewe ni mteja wa malipo ya awali au la, tafadhali piga 100 Huduma kwa Wateja na utapata suluhisho paop hapo.

4. Ofa gani znapatikana ndani Ofa za Ya Kwako 2?

Kila mteja atapata Ofa ya kupiga simu, intaneti na SMS. Kipaumbele kitapewa kwa Ofa ambayo inaendana na matumizi binafsi ya kila mteja.

Mfano: Kama mteja ana matumizi makubwa ya kupiga simu kulinganisha na intaneti/SMS, atapata Ofa Maalum kabambe kwaajili ya matumizi ya intaneti kukidhi mahitaji yake. Mteja pia atapata ofa za intaneti/SMS kama pendekezo.

5. Kwanini nitumie Ofa za Ya Kwako 2?

Ofa za Ya Kwako 2 zimetengenezwa kwa kuzingatia matumizi binafsi ya kila mteja kwahiyo kila mteja atapata ofa inayoendana na mahitaji yake binafsi kwa upande wa vifurushi kabambe kabisa na thamani zaidi ya pesa zako.

6. Naweza kujiunga mara ngapi?

Unaruhusiwa kujiunga mara nyingi na kwa wakati wowote kadri upendavyo katika huduma ya Ofa Maalum.

Vigezo na Masharti
1. Ya Kwako Tu ni huduma inayowapatia wateja wa malipo ya awali wa Vodacom ofa za Vifurushi vya kupiga simu, Intaneti au SMS kwa gharama nafuu kabisa kulingana na tabia za matumizi binafsi ya kila mteja.
2. Ofa za Ya Kwako Tu kwa sasa inapatikana kwa wateja wa Vodacom wa Malipo ya Awali tu!
3. Kupata Ofa za Ya Kwako Tu mteja anatakiwa apige *149*03# kisha ataona orodha ya Ofa za vifurushi vya kupiga simu, Intaneti au SMS ambazo atachangua na kujiunga.
4. Vodacom Tanzania ina ruhusa ya kubadili au kuondoa Ofa za Ya Kwako Tu kwa mteja yeyote wakati wowote bila taarifa yoyote ya awali kwa mteja.
Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa