Lipa kwa Simu

 • Lipa kwa SIMU Overview
 • Jinsi ya Kulipa kwa SIMU
 • Maswali yaulizwayo

Lipa kwa SIMU

ULIMWENGU MPYA WA MALIPO KIDIGITALI TANZANIA

Lipa kwa simu’ ni mfumo wa malipo uliozinduliwa na Vodacom Novembam 2016 kwa lengo la kufanya malipo kwenye biashara ndani ya Tanzania kuwa ya kidigitali ili kuwawezesha wafanyabiashara kukusanya malipo kwa urahisi na usalama huku ikiwasaidia wateja kuondokana na hatari za kubeba pesa taslimu. Machi 2017, Vodacom iliboresha huduma kwa kuzindua M-Pesa app ambayo pamoja na faida nyingine, ni kuwezesha malipo kwa kutumia mfumo wa QR ambao unarahisisha zaidi malipo kwa kuondoa ulazima wa mteja kuandika namba ya till uwapo sehemu ya malipo.

Huduma ya Lipa kwa simu imewaunganisha wateja wa mitandao yote na benki kufanya malipo kwa urahisi, usalama ukilinganisha na pesa taslimu ambayo ni gharama na hatari na ndio maana tunasema M-Pesa malipo ndio nyumbani kwani wateja kutoka mitandao yote na benki wamewezeshwa kufanya malipo kwa wafanyabiashara wenye Lipa namba moja kwa kutoka kwenye akaunti zao. Kulipa kwa kutumia simu yako inakuwezesha kupata faida zifuatazo

 • Mitandao yote na mabenki yameunganishwa na malipo ya M-Pesa hivyo kuondoa usumbufu wa wafanyabiasha kulazimika kuwa na Till nyingi za malipo.
 • Salama na haina hatari.(inazuia hatari ya uhalifu, wizi, noti bandia n.k)
 • Haraka na hakika kwa malipo ya kwenda mbali (haraka kulinganisha na pesa taslimu)
 • Rahisi na inaongeza ufanisi. Hakuna usumbufu wa chenji, inaweka kumbukumbu ya miamala yote na ni rahisi zaidi unapotumia mfumo wa QR.
 • Lipa kwa simu inakuwezesha kulipa kwa uhakika kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara wa sekta zote kama Baa, Hoteli, migahawa, Supamaketi, Vituo vya mafuta, kumbi za sinema, maduka ya dawa, Maduka ya vifaa vya ujenzi na kadhalika

JINSI YA KULIPA KWA SIMU KWA WAFANYABIASHARA

JINSI YA KULIPA KWA SIMU KWA WAFANYABIASHARA WENYE LIPA NAMBA ZA M-PESA:
WATUMIAJI WA VODACOM M-PESA Kwa kutumia USSD

 • 1. Piga *150*00#
 • 2. Chagua Lipa kwa Simu
 • 3. Weka Lipa namba
 • 4. Weka kiasi unacholipa
 • 5. Weka namba ya siri
 • 6. Utapokea SMS kuthibitisha muamala.

Kwa kutumia M-Pesa app

 • 1. Fungua M-Pesa APP kisha bonyeza kitufe kinachoonyesha QR.
 • 2. Scan picha ya QR iliyoko kwenye bango la mfanyabiashara.
 • 3. kisha weka KIASI na PIN ya M-Pesa kukamilisha malipo.

JINSI YA KULIPA KWA SIMU:
WATUMIAJI WA TIGO PESA

 • 1. Piga *150*01#
 • 2. Chagua Tuma Pesa
 • 3. Chagua kwenda mitandao mingine
 • 4. Chagua M-Pesa
 • 5. Weka namba ya simu (Tarakimu saba za Lipa Namba)

JINSI YA KULIPA KWA SIMU:
WATUMIAJI WA HALO PESA

 • 1. Piga *150*88#
 • 2. Chagua Tuma Pesa
 • 3. Chagua kwenda mitandao mingine
 • 4. Chagua M-Pesa
 • 5. Weka namba ya simu (Tarakimu saba za Lipa Namba)
 • 6. Weka kiasi
 • 7. Weka namba ya siri
 • Utapokea SMS kuthibitisha muamala. Utatozwa gharama za kawaida za kutuma fedha

JINSI YA KULIPA KWA SIMU:
WATUMIAJI WA EZY PESA

 • 1. Piga *150*02#
 • 3. Chagua kwenda mitandao mingine
 • 4. Chagua M-Pesa
 • 5. Weka namba ya simu (Tarakimu saba za Lipa Namba)
 • 6. Weka kiasi
 • 7. Weka namba ya siri
 • 8. Utapokea SMS kuthibitisha muamala. Utatozwa gharama za kawaida za kutuma fedha za mtandao wako.

JINSI YA KULIPA KWA SIMU:
WATUMIAJI WA AIRTEL MONEY

 • 1. Piga *150*60#
 • 2. Chagua Tuma Pesa
 • 3. Chagua kwenda mitandao mingine
 • 4. Chagua M-Pesa
 • 5. Weka namba ya simu (Tarakimu saba za Lipa Namba)
 • 6. Weka kiasi
 • 7. Weka namba ya siri
 • 8. Utapokea SMS kuthibitisha muamala. Utatozwa gharama za kawaida za kutuma fedha za mtandao wako.

JINSI YA KULIPA KWA SIMU:
WATUMIAJI WA AKAUNTI ZA BENKI

 • 1. Fungua menyu ya huduma za kifedha za benki yako
 • 2. Chagua Malipo
 • 3. Chagua Lipa kwa M-Pesa
 • 4. Weka namba ya simu (Tarakimu saba za Lipa Namba)
 • 5. Weka Kiasi
 • 6. Weka namba ya siri ya benki

Maswali Yaulizwayo

Je, Gharama za kulipa kwa simu zikoje?

Kwa wateja wa Vodacom M-Pesa, Ada za Lipa kwa simu kwa sasa ni 0.5% ya kiasi unacholipa kwa malipo ya Tshs 100 hadi M1.5, Tshs 7500 kwa M1.5-M2 na Tshs 8000 kwa miamala ya Zaidi ya M2.

Je, nitaweza kulipa vipi kutoka mitandao mingine au benki?

Soma maelekezo ya hatua kwa hatua ya jinsi ya kulipa kwa simu kutoka kwenye mtandao ulioko kwa kuangalia kurasa za mwanzo za kipeperushi hiki.

Je, nitapataje msaada wa huduma kwa wateja?

Kwa msaada wa lipa kwa simu yako, piga namba 0746500001/100/101 kutoka kwenye namba ya Vodacom wakati wowote.

Je, nitamsaidiaje mteja aliyelipa kwenye Lipa namba isiyo sahihi?

Mshauri mteja apige simu Vodacom huduma kwa wateja (100) kwa msaada zaidi.

Je, miamala ya Lipa kwa Simu inachukua muda gani kukamilika?

Miamala hii inakamilika papo hapo. Wewe na mteja wote mtapokea SMS zinazothibitisha kila muamala.

Je, nifanye nini iwapo sitapokea SMS ya malipo kwa wakati?

Vodacom itakujulisha kama kuna tatizo lolote. Na ikiwa wewe na mteja hamjapata SMS, piga namba 0746500001/100/101 kwa msaada zaidi.

Je, nini kitatokea iwapo Lipa namba yangu itaibiwa?

Ikiwa LIPA namba yako itaibiwa, utapata SIMcard mpya na kisha utajaza fomu ya kurudishiwa LIPA namba yako katika maduka yote ya Vodacom Tanzania. Namba yako na pesa zako zitakua salama.

Je, naweza kubadili namba ya kupokea malipo kwa M-Pesa ninayoitumia kupokelea malipo?

Ndiyo, unaweza kubadili namba ya kupokea malipo. Kwa kuzingatia usalama wa pesa za wateja wetu. Lipa namba mpya itatolewa endapo maombi yamefanyika na mmiliki wa biashara tu.

Je, ninaweza kumiliki Lipa namba zaidi ya moja?

Ndiyo, unaweza kumiliki Lipa namba zaidi ya moja kama unafungua biashara mpya au unapanua wigo wa biashara yako ya sasa. Piga namba 0746500001 BURE kupata maelezo zaidi.


Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa