• M-Koba
 • Jinsi ya kufungua akaunti ya M-Koba & kusajili kikundi
 • M-Koba kwa Familia na Marafiki
 • M-Koba kwa VICOBAs , VSLAs nk
 • M-Koba Maswali yaulizwayo Mara kwa Mara

M-Koba

M-Koba
Vodacom kwa kushirikiana na TPB Bank tumewalatea huduma mpya ya kutunza fedha, kupeana mikopo na kugawana faida kwa vikundi kama familia na marafiki, VICOBA, VSLA, SACCOS, Upatu na vikundi mbalimbali vyenye Utamaduni wa kuchanga kwa lengo la kuweka akiba na kukopeshana pesa. Huduma hii inaitwa M-KOBA. M-Koba ni huduma mpya ya kuchanga Kidijitali inayoleta usalama wa fedha za wanakikundi, uwazi na urahisi wa kuchanga kutoka popote kupitia mtandao wa Vodacom.

M-Koba imeletwa ili kutatua changamoto mbalimbali ambazo vikundi vinakutana nazo katika mfumo wa kutumia pesa taslim kama usalama mdogo wa fedha zinazokusanywa, wanavikundi kutokuwa urahisi wa kukusanya pesa.M-Koba ni hatua nyingine kubwa ya kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa Kidijitali kwani inaondoa ulazima wa kubeba pesa taslimu kwenye shughuli za vikundi.

Jinsi ya kufungua akaunti ya M-Koba na kusajili Kikundi

Jinsi ya kufungua akaunti ya M-Koba na kusajili Kikundi

Jiunge na M-KOBA leo ufanikishe malengo ya kikundi chako kiganjani kwako. Jinsi ya kujiunga na kusajili kikundi na M-KOBA ni rahisi, unapiga *150*00#, kisha unachagua namba 6 Huduma za Kifedha na kisha unafuata hatua rahisi kulingana na aina ya kikundi chako kama inavyoonyeshwa hapa chini.

Jinsi ya kufungua akaunti ya M-Koba

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-Koba
 3. Chagua Sajili Kikundi
 4. Chagua Familia/Marafiki

Jinsi ya kusajili Kikundi

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua Sajili Kikundi
 4. Chagua Familia/Marafiki
 5. Ingiza jina la kikundi
 6. Ingiza kiasi cha kufungua akaunti
 7. Chagua 1 kuthibitisha
 8. Weka namba ya siri (M-Pesa)

M-Koba kwa Familia na Marafiki

M-Koba kwa familia na marafiki imeundwa kuwawezesha watejawenye vikundi vidogo-vidogo ambavyo vinaweza kuwa vya kifamilia au marafiki ambao wana lengo lakuweka akiba kwa kipindi cha muda mfupi au mrefu kwa kushirikiana na baadae kuzitoa na kutumia. Vikundi hivi na kama majirani, wanafamilia, watu wanaofanya kazi pamoja, makundi ya whatsapp,Watu waliosoma pamoja, jumuiya n.k. Lengo kuu la akaunti hii ni kuwezesha wenye kikundi kuweka akiba kwa pamoja kwenye njia salama kupitia M-Koba na baadae kugawana pesa iliyowekwa kwa utaratibu uliowekwa na kikundi husika.

Angalia video namna ya kujiunga M-Koba kwa familia na marafiki

Jinsi ya Kuongeza wanachama

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua Kikundi 1
 4. Chagua Wanachama
 5. Chagua Ongeza Wanachama
 6. Ingiza namba ya Simu
 7. Chagua 1 kuthibitisha

Jinsi ya kuthibitisha Viongozi/Wanachama

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua Kikundi 1
 4. Chagua Maombi
 5. Chagua 1 kuthibitisha
 6. Weka namba ya siri (M-Pesa)

Jinsi ya Kuchangia

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua Kikundi 1
 4. Chagua Kuchangia
 5. Ingiza Kiasi
 6. Weka namba ya siri (M-Pesa)

Jinsi ya kuhamisha fedha(Katibu)

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua Kikundi 1
 4. Chagua hamisha fedha
 5. Ingiza namba ya Simu
 6. Ingiza Kiasi
 7. Chagua 1 kuthibitisha

Jinsi ya kuhakiki hamisho la fedha: (Muweka hazina)

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua Kikundi 1
 4. Chagua hakiki
 5. Chagua Mwanachama
 6. Chagua 1 kuthibitisha

Jinsi ya kuidhinisha kuhamisha fedha: (Mwenyekiti)

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua Kikundi 1
 4. Chagua idhinisha
 5. Chagua mwanachama
 6. Chagua 1 kuthibitisha

Jinsi ya kuangalia salio la michango yako

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua Kikundi 1
 4. Chagua salio
 5. Chagua michango yangu

Jinsi ya kuangalia salio la kikundi chako

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua Kikundi 1
 4. Chagua salio
 5. Chagua michango ya kikundi

M-Koba kwa VICOBAs VSLAs nk

M-Koba kwa VICOBAs, VSLAs nk..
Wanachama wa vikundi mbalimbali vyenye mfumo mahususi kama VICOBA, VSAL, CB, VB n.k mtanufaika na akaunti hii kwani mbali ya kuwaongeza urahisi na usalama wa pesa zenu, bado itawezesha kufanya yale yote ambayo mnafanya kwa mfumo wa sasa lakini kwa usalama, uwazi na urahisi Zaidi. Akaunti hii itawezesha kuchagua Viongozi, kuweka na kona kanuni za kikundi,Kununa hisa, Kuomba na kurejesha mikopo, kuweka michango ya jamii, kuona salio la mwanachama, kuona salio la kikundi na mengine mengi

Angalia video namna ya kujiunga M-Koba kwa VICOBAs, VSLAs

Jinsi ya kusajili Kikundi (kama VICOBA, VSLA, CB, VB)

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua VICOBA/VSLA
 4. Ingiza Jina la Kikundi
 5. Ingiza kiasi cha kufungua akaunti
 6. Chagua 1 kuthibitisha
 7. Weka namba ya siri (M-Pesa)

Jinsi ya Kuongeza Viongozi/Wanachama

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua VICOBA/VSLA
 4. Chagua Kikundi 1
 5. Chagua Kiongozi
 6. Chagua Ongeza Wanachama
 7. Ingiza namba ya simu ya mwanachama

Jinsi ya kujua kanuni za kikundi

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua VICOBA/VSLA
 4. Chagua Kikundi
 5. Chagua kanuni za kikundi
 6. Chagua weka bei za hisa moja

Jinsi ya kununua Hisa

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua VICOBA/VSLA
 4. Chagua Kikundi 1
 5. Chagua Nunua Hisa
 6. Ingiza Kiasi
 7. Weka namba ya siri (M-Pesa)

Jinsi ya kurejesha mkopo

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua VICOBA/VSLA
 4. Chagua Kikundi 1
 5. Chagua mkopo
 6. Ingiza Kiasi
 7. Weka namba ya siri (M-Pesa)

Jinsi ya Kuchangia jamii katika Kikundi

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua VICOBA/VSLA
 4. Chagua Kikundi 1
 5. Chagua jamii
 6. Ingiza Kiasi
 7. Weka namba ya siri (M-Pesa)

Jinsi ya kuhamisha fedha (Katibu)

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua VICOBA/VSLA
 4. Chagua Kikundi 1
 5. Chagua hamisha fedha
 6. Chagua Mkopo, Jamii, Gawio au Mwengineyo
 7. Ingiza namba ya Simu
 8. Ingiza Kiasi
 9. Chagua 1 kuthibitisha

Jinsi ya kuhakiki hamisho la fedha: (Muweka hazina)

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua VICOBA/VSLA
 4. Chagua Kikundi 1
 5. Chagua hakiki
 6. Chagua mwanachama
 7. Chagua 1 kuthibitisha

Jinsi ya kuidhinisha kuhamisha la fedha: (Mwenyekiti)

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua VICOBA/VSLA
 4. Chagua Kikundi 1
 5. Chagua hakiki
 6. Chagua mwanachama
 7. Chagua 1 kuthibitisha

Jinsi ya kuangalia salio la michango yako

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua VICOBA/VSLA
 4. Chagua Kikundi 1
 5. Chagua salio
 6. Chagua michango yangu

Jinsi ya kuangalia salio la kikundi chako

 1. Piga *150*00 chagua Huduma za Kifedha
 2. Chagua M-KOBA
 3. Chagua VICOBA/VSLA
 4. Chagua Kikundi 1
 5. Chagua Balance
 6. Chagua michango ya kikundi

M-Koba Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

M-KOBA ni nini?

M-KOBA ni huduma ya kifedha inayoendeshwa na Vodacom kwa ushirikiano na TPB Bank inayolenga kuwezesha wateja wa M-Pesa kufungua na kuendesha Akaunti za kuweka akiba kwa makundi huku wakifurahia huduma za kifedha. Bidhaa hii itazingatia kutoa mazingira mazuri kwa vikundi vya kuchanga fedha kama VICOBA, VSLA na vile vya kifamila na marafiki kufanya kazi kwa muda halisi ili kuhakikisha wanapunguza gharama za uendeshaji, usalama na uwazi kati ya wanachama na kikundi kwa ujumla. Hii inamaanisha wale wenye vikindi vya kuchanga fedha wataweza kujiandikisha wenyewe kupitia M-KOBA na kuendesha vikundi vyao kwa njia ya kidigitali. Huduma hii itapatikana kupitia M-Pesa. Wateja watapiga *150*00# kisha bonyeza Huduma ya Fedha kisha kuchagua M-KOBA.

Kuna Akaunti ngapi kwenye bidhaa ya M-KOBA?

A: M-KOBA inajumuisha Akaunti mbili mbazo mteja ataweza kutumia:

 • Marafiki/Familia
 • VICOBA/VSLA

Marafiki/Familia
Hii ni akaunti maususi kwa vikundi vidogo inaweza kuwa familia ama marafiki ambao wamekusudia kuchanga fedha na baadae kugawana baada ya muda Fulani. Mfano: UPATU.

VICOBA/VSLA
Hii ni akaunti maususi kwa ajili ya vikundi vyenye upana mkubwa wa wanachama na vilivyo na mfumo wa kuuza na kununua hisa, kuweka akiba, Michango ya Kijamii na Kupeana Mikopo. Vikundi hivi ni vile vihusishavyo VICOBA/VSLA/CB/SILC

Nani anaweza kufungua Akaunti ya M-KOBA?

Wateja wa Vodacom wanaotumia M-Pesa pekee ndio watakaoweza kufungua Akaunti ya M-KOBA.

Vigezo vya kufungua akaunti ya M-KOBA ni vipi?

1.Kikundi cha M-KOBA kitatakiwa kuwa na wanachama wasiopungua wanne.

2. Ili kutengeneza akaunti ya M-KOBA Kila kikundi kinapaswa kuwa na viongozi watatu.
Mwenyekiti

Katibu
Mwekahazina

Je kuna ada yoyote mteja anayolipia kutumia M-KOBA

Hakuna ada wala makato yoyote kwa mteja atakapo fungua au kutumia Akaunti ya M-KOBA. Kutakuwa na gharama ndogo ya tozo ya Tsh.100 pale mteja takapokuwa akiangalia salio la Michango.

Je, kuna ada yoyote ya mteja atakayolipa wakati wa kutuma pesa kutoka M-Pesa kwenda kwenye akaunti ya M-KOBA?

Hakuna ada yoyote mteja atakayolipa kwa kutoa pesa kwenye Akaunti yake ya M-Pesa kwenda kwenye akaunti ya Kikundi au kutoa pesa kwenye akaunti ya kikundi kwenda kwa mwanakikundi.

Je ni taarifa gani ambazo Vodacom itazitoa kwa benki ya TPB pindi nitakapo fungua au kujiunga na Akaunti ya vikundi ya M-KOBA?

Mteja atakapo kuwa akifungua au kujiunga na Akaunti ya M-KOBA taarifa za kawaida za Mteja zitatumwa kutoka Vodacom kwenda kwenye benki ya TPB. Taarifa hizi ni Jina la Mteja, Namba ya simu, Jinsia na Umri wa mteja. Hivyo kabla ya kufungua au kujiunga na Akaunti ya M-KOBA mteja atatakiwa kukubali vigezo na Masharti.

Viongozi wa Vikundi ndo nani?

Kila kikundi kwenye M-KOBA kitakuwa na viongozi watatu ambao ni:
MWENYEKITI: Yeye ndiye mwanzilishi na msimamizi wa kikundi. Ana mamlaka ya kuongeza mwanachama yeyote na kuchagua viongozi wengine na yeye ndiye mtu wa mwisho kuidhinisha uhamisho wa malipo kwa mwanachama yeyote
KATIBU: Anaongezwa na mwenyekiti wa kikundi na ndiye anayeanzisha malipo yote na Mkopo kwa wanachama wengine.
MWEKAHAZINA: Anaongezwa na mwenyekiti wa kikundi, ana mamlaka ya kuthibitisha Malipo na Mikopo inayotolewa kwa wanachama.

Je, tunahamishaje fedha kutoka kwa akaunti ya kikundi cha M-KOBA kwenda kwenye Akaunti ya mtu ya M-Pesa?

Fedha zitahamishwa kupitia awamu tatu, Katibu ataanzisha mchakato wa malipo kutoka kwa akaunti ya kikundi kwa mwanachama kisha Mwekezaji atahakiki Malipo na Mwenyekiti wa kikundi ataidhinisha Malipo ndopo fedha zitahamishwa kutoka kwa Akaunti ya Kundi kwenda kwa mwanachama alie kusudiwa.

Ninawasiliana nani nikiwa na malalamiko, maswali, mapendekezo au ombi?

Wateja watatakiwa kuwasiliana na Huduma kwa wateja ikiwa wanamalalamiko au Mapendekezo juu ya bidhaa ya M-KOBA. Wataje watatakiwa kupiga 100.

Ni nini kinachofanyika wakati wa mgogoro wa kundi?

Ikiwa itatokea mgogoro kwa wanachama wa kikundi kutokana na kutoelewana juu ya fedha za kikundi wanakikundi watahitajika kuripoti polisi. Baada ya kuripoti polisi watapewa kibali Maalumu na kuwasilisha Vodacom ili kuzuia fedha za kikundi kutoka. baada ya kupokea ruhusa ya Polisi Vodacom itazuia fedha za akaunti ya kikundi na wanachama wa kikundi watahitajika kutatua tena tofauti zao polisi na kupata kibali kingine cha kuruhusu Vodacom kufungua fedha zao za kikundi.Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa