Huduma Binafsi

1.Magic Voice ni nini?

Ni huduma inayokuweza kubadili sauti, mfano sauti ya kuchekesha au sauti nyinginezo wakati unapopiga simu kwa rafiki ukitumia laini ya Vodacom.

2.Ni nani anaweza kutumia huduma?

Huduma hii ni kwa wateja wote wa Vodacom(wa malipo kabla na baada). Pale wanapojiunga na huduma, watweza kupiga simu kwa marafiki kwa kutumia sauti walizobadili.

3.Je ni namna gani wateja watajiunga na huduma?

Kwa kupitia IVR: Mteja atapiga 0901767777 na kisha kufuata maelekezo ya kujiunga.

Kwa kupitia OBD: mfumo wa huduma utampigia simu mteja ambapo anaweza kujiunga kwa kufuata maelekezo baada ya kupokea simu.

4. Je huduma inafanyaje kazi?

Mtaja atapiga * ikifuatiwa na namba ya rafiki kutoka kwenye simu.

Mteja atachagua aina ya sauti .

Baada ya hapo simu itaunganishwa na mteja ataweza kuzungumza na rafiki akitumia sauti aliyobadili.

NB: Mpokeaji atapokea simu kama simu ya kawaida

5.Je utagharamia kiasi gani kutumia huduma?

Tsh. 99 kwa siku

6.Je nini kitatokea kama sitakuwa na salio la Tsh99 kwenye simu yangu?

Hautaweza kutumia huduma mpaka utapokuwa na kiasi cha Tsh 99

7.Je unatakiwa kuwa na simu maalum ili utumie huduma hii?

Hapana. Huduma hii inaweza kufanya kazi kwenye simu ya aina yoyote

8.Je mteja atagharamia kiasi gani kutumia huduma hii?

Kupiga IVR ni BURE. Gharama kwa dakika itaendelea kwa wateja wanaotumia huduma hii

9.Ni wakati gani mteja ataanza kugharamia huduma?

Kuna gharama ya kujiunga na huduma. Bila kujiunga, mteja hataweza kutumia huduma. Gharama kwa dakika itakatwa kwa wateja wanaotumia huduma hii.

10.Je nini kitatokea kama mteja hatabonyeza kuchagua sauti?

Kama mteja hatachagua chaguo katika kipindi fulani cha muda, chaguo la msingi la sauti litawekwa na itapigwa simu kwenda kwa rafiki ikiwa na chaguo hilo.

11.Je wateja wanaweza kubadili sauti kwenda sauti nyingine wakati wanaongea na marafiki?

Ndio, wakati wanaongea wanaweza kubonyeza ‘1’, ‘2’ au ‘3’ kubadili sauti zao kwenda sauti nyingine zilizopo.

12.Je mteja anawezesha kurudisha tena mlio aliochagua awali wakati anaongea na rafiki?

Ndio. Kurudisha sauti ya awali, mteja atabonyeza ‘0’.

13.Je naweza kuwapigia marafiki wanaotumia mitandao mingine nikitumia sauti niliobadili?

Ndio, utabonyeza* ikifuatiwa na namba ya rafiki

14.Ni lugha zipi zinazokubalika na huduma?

Huduma hii haichagui lugha. Inafanya kazi ikitumia matamshi kwa hio mteja anaweza kutumia lugha yoyote.

15.Je sauti zinaweza kubadilishwa kuwa maalum kama za watu mashuhuri?

Hapana

16.Je ni namna gani wateja wanaweza kujiondoa kwenye huduma?

Kwa kupitia IVR: Wateja watapiga 0901767777 na kufuatilia maelekezo kutoka kwenye menu ya huduma ili kujiondoa kwenye huduma.
Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa