M-Pawa

Karibu kwenye M-Pawa

Hii ni huduma ya kibenki kutoka Vodacom na CBA ambayo imeleta mapinduzi ya kumwezesha mteja kuhifadhi pesa kwenye simu, kupata riba kutokana na akiba na kupata mikopo unapoihitaji. M-Pawa ipo kama rafiki mwaminifu ambae atakupa msaada wa maendeleao na kufanikisha mipango yako ya maisha.

NB:
Kwa kufuata maelekezo ya mdhibiti, VAT itaondolewa kwa ada zote zitozwazo kwenye mkopo wa M-Pawa kuanzia tarehe 12/08/2017. Hii ina maana kuwa wakati wa malipo ya mkopo ada za mkopo zitataondolewa kwenye kiasi cha mkopo

 • Utaweza kufungua na kutumia akaunti ya akiba kwenye simu yako kwa kutumia M-Pesa bila kutembelea benki na kujaza fomu za maombi
 • Unaweza kuweka akiba kidogo kidogo hata Tsh 1 na upate faida kwa kutoka akiba ulioweka. Faida kutakana na akiba inahesabiwa kila siku na kulipwa kila mwisho wa robo ya mwaka.
 • M-Pawa inakuwezesha kupata mikopo midogo midogo papo papo kwa M-Pesa, kiasi cha chini kikiwa Tsh 1000.
 • Utaweza kuhamisha pesa bila gharama yoyote kati akaunti ya M-Pesa na akaunti ya akiba ya M-Pesa.
 • Hakuna kiasi cha chini cha salio kwenye M-Pawa.
 • M-Pawa ni nyepesi, hakika, papo kwa papo na rahisi
 • Hakuna gharama za ziada.

Kama unaamini ili kupata huduma za kibenki hautakiwi kupata usumbufu basi M-Pawa ndio chaguo lako.

Nini mahitaji ya M-Pawa
Ili kuweza kutumia huduma ya M-Pawa unatakiwa

 • Uwe mteja wa Vodacom na umekamilisha usajili
 • Uwe na akaunti ya M-Pesa inayofanya kazi
 • Uwe na vitambulisho vifuatavyo
  • Pasi ya kusafiria ya Tanzania
  • Kitambulisho cha Taifa
  • Kitambulisho cha kupiga kura
  • Leseni ya udereva
  • Kitambulisho cha Kazi au Barua kutoka Serikali za Mitaa

Nini manufaa ya kutumia M-Pawa?

 • Haitumii makaratasi. Utafungua na kuendesha akaunti ya benki bila kutemebelea benki
 • Unaweza kuweka akiba kidogo kidogo hata Tsh 1 na upate faida kwa kutoka akiba ulioweka. Faida kutakana na akiba inhesabiwa kila siku na kulipwa kila mwisho wa robo ya mwaka.
 • Utahamisha pesa bila gharama kati ya akaunti ya M-Pesa na akaunti ya akiba ya M-Pawa
 • Hakuna kiasi cha chini cha salio kwenye M-Pawa.
 • M-Pawa inakuwezesha kupata mikopo midogo midogo papo papo kwa M-Pesa, kiasi cha chini kikiwa Tsh 1000.
 • Hakuna gharama za ziada.

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa