M-PAWA Maswali yaulizwayo mara kwa mara

 • Maswali ya Jumla
 • Mkopo
 • Akiba
 • Salio na Taarifa

Maswali ya Jumla

M-Pawa ni nini ?

Hii ni huduma ya kibenki kwenye simu kwa wateja waliojisajili na M-Pesa kwa ushirikiana na CBA.
Wateja wanaweza kuweka akiba na kukopa pesa huku wakipata faida itokanayo na kuweka akiba

Nani anastahili kutumia huduma ya M-Pawa?

Mteja wa Vodacom aliesajiliwa.

Nini mahitaji ya M-Pawa??

Akaunti ya M-Pesa iliosajiliwa
Vitambulisho kama Pasi ya kusafiria ya Tanzania, kitambulisho cha Taifa, kitambulisho cha Kura, leseni ya udereva, kitambulisho cha kazi na barua kutoka Serikali za Mitaa.

Je ni kazi gani za M-Pawa kwenye menu?

Hizi ni aina ya kazi zilizoko kwenye menu ya M-Pawa;
Kutuma fedha
Kutoa pesa
Mkopo
Salio
Taarifa Fupi
Vigezo na Masharti

Je kuna umuhimu wa kuwa na PIN tofauti kati ya akaunti za M-Pesa na M-Pawa?

Hapana. PIN hi hio itatuka kwenye akaunti ya M-Pesa na M-Pawa.

Je inawezekana kutumia M-Pawa ukiwa nje ya Tanzania?

Ndio, unaweza ukatumia M-Pawa ukiwa nje ya Tanzania kama ilivyo kwa M-Pesa ingawa kuweka na kutoa pesa itafanyika tu kwa wakala ukiwa Tanzania.

Je itakuwaje kama utapoteza simu ikiwa na akaunti ya M-Pawa?

Pale simu inapopotea , pesa yako itabaki kuwa kwenye usalama kwa kuwa akaunti ya M-Pawa inalindwa na PIN ya M-Pesa.
Ili kurudisha laini, Utafuata utaratibu wa kubadili laini kwa kutembelea Vodacom shop yoyote.
Baada ya kubadili laini , mfumo utaweka taarifa zako za M-Pawa na utaweza kuona pesa yako

Je nawezeshaji M-Pawa?

Kama wewe ni mteja wa M-Pesa:

Nenda kwenye menu ya M-Pesa (*150*00#)
Chagua "M-Pawa”
Nenda kwenye "Wezesha Akaunti". Chaguo la pili ni Vigezo na Masharti ambayo inakuelekeza kwenda www.cbagroup.com/M-Pawa au www.vodacom.co.tz.
Ingiza PIN ya M-Pesa
Ujumbe utatokea ukukitaka kujua kama umessoma na kukubali Vigezo na Masharti. Baada ya kukubali, utapokea SMS ikikujulisha kuwa ombi lako la M-Pawa limepokelewa na liatshughulikiwa hivi punde.
Utafuata ujumbe mfupi wa kuthibitisha kutengenezwa kwa akaunti yako.
Akaunti yako ya {M-Pawa} imefanikiwa kutengenezwa.

Kama ikishindikana, utapokea ujumbe kukufahamisha na kukushauri uwasiliane na Huduma kwa Wateja.
Hutaweza kutumia akaunti yako ya {M-Pawa} kwa kuwa huduma ina matatizo. Tafadhali wasiliana na Huduma Kwa Wateja kwa namba 100.

Kama wewe si mteja M-Pesa:
Tembelea Wakala wa M-Pesa au Vodacom shop kujisajili na huduma ya M-Pesa.
Neno ya siri ya kianzio litatumwa kwenye simu yako kwa njia ya SMS.
Piga *150*00# kwa kutumia M-Pesa
Chagua “Wezesha” au “M-Pawa” – cheki tena
Weka neno la kianzio ulilopokea
Baada ya hapo, endelea kutumia kama mteja mwingine wa M-Pesa.

Je ni idara gani/shirika gani la Serikali linahusika kusimamia kanuni na sharia zaVAT?

Mamlaka ya Mapato ndio inahusika kutathmini, kukusanya na kufanya mahesabu ya mapato yote ya serikali. Pia wanahakikisha Taasisi zote za kifedha zinatii sharia mpya ya VAT kuhusu malipo ya ada za makusanyo.

Je sharia hii inatumika kwenye huduma ya M-Pawa?

Ndio. M-Pawa inatoza gharama ya 9% kwa maombi yote ya Mikopo.Yes. Gharama hii itategemea makato ya VAT yanayotakiwa kulipwa TRA. Hakuna mabadiliko kwenye Akiba.

Mkopo

Nini kinachangia uwe na sifa za kupata mkopo?

INA RUHUSIWA

 HAIRUHUSIWI

Bidhaa za Vodacom
 1. Uwe mteja wa Vodacom kwa angalau miezi 6; utafaidika zaidi kama umekaa muda mrefu na Vodacom
 2. Tumia simu yako mara kwa mara kwa kupiga, kutuma SMS na  kuperuzi
 3. Hakikisha unaongeza salio mara kwa mara (kiasi chochote)
 4. Tumia M-Pesa mara kwa mara;
 • Kupokea pesa
 • Kutuma pesa
 • Kulipa gharama n.k.
5. Kama unatumia Nipige Tafu;
 • Lipa Nipige Tafu kwa wakati
 • Punguza vitendo vitakavyokufanya uzuiwe kutumia Nipige Tafu

Bidhaa za Vodacom

 1. Usiache matumizi ya laini yako kwa muda mrefu
 2. Usiache laini yako bila muda wa maongezi kwa muda mrefu
 3. Usiache M-Pesa bila matumizi kwa muda mrefu
 4. Kama unatumia Nipige Tafu;
 • Usichelewe kulipa Nipige Tafu
 • Epuka kuzuiwa kutumia Nipige Tafu
M-Pawa Kuwa na m-Pawa na Kaa na M-Pawa; muda mrefu unatakaokaa na M-Pawa manufaa zaidi
 1. Weka akiba kila mara na M-Pawa; chagua kiasi chochote utakachoweza kulipa na weka akiba mfululizo kwa siku/wiki na mwezi
 2. Punguza idadiya kutoa pesa kutoka akaunti ya M-Pawa; salio kwenye M-Pawa likikaa muda zaidi ; Faida kubwa zaidi
 3. Kama ukichukua mkopo wa M-Pawa, lipa muda mara kwa mara kiasi unachomudu na hakikisha unamaliza kabla muda wa kulipa haujakwisha.
M-Pawa
 1. Usiache akaunti yako ya M-Pawa bila kuitumia muda mrefu
 2. Usifunge akaunti yako ya M-Pawa ; utapoteza taarifa za akaunti yako kama ukuiifunga
 3. Punguza idadi ya kutoa pesa kutoka akaunti ya M-Pawa
 4. Kama ukichukua mkopo wa M-Pawa, hakikisha malipo hayachelewi.

Riba ya mkopo ni ipi ukitumia M-Pesa?

Hakuna riba inayotozwa. Gharama ya ushauri ya 9% ya mkopo ndio hutozwa mara moja tu kwa kila mkopo ndani siku 30.

Kama umeomba mkopo wa Tsh. 100,000, utalipa Tsh. 109,000 ndani ya siku 30.

Je kama ukilipa mkopo kabla ya muda wa kulipa kupita, bado utakatwa gharama ya ushauri ya 9% ya kiasi cha mkopo?

Ndio, hii ni gharama ya kukamilisha mkopo . Kulipa mapema kunakupa kunakuongezea nafasi ya kukupa siku zijazo.

Muda wa mkop ni nini?

Mkopo utalipwa ndani ya siku 30. Ila unaweza kulipa kabla muda wa kulipa mkopo haupita na ukope tena. Kama utalipa mkopo chini ya siku 30, kikomo cha kukopa kitaongezwa haraka .

Unawezaje kuangalia kiasi unachoweza kukopa?

Nenda kwenye  menu ya M-Pesa

Chagua “M-Pawa”

Chagua ‘Mkopo’

Nenda kwenye “angalia kikomo cha mkopo”

Ingiza PIN ya M-Pesa

Subiri ujumbe kutoka benki  kama unastahili

Utapokea ujumbe kukufahamisha kama unastahili kupata mkopo au maelezo yako, ukiwa au huna mkopo.

Viwango vya juu na chini vya mkopo ni vipi?

Kutokana na kanuni za  bidhaa, kiwango cha chini kinachweza kukupwa ni Tsh 1000 and kiwango cha juu ni Tsh 500,000. Ingawa kiwango cha juu kwa mtu binafsi kitategemea  namna ya matumizi ya mtu binafsi.

Ni namna gani mteja ataomba mkopo kupitia M-Pawa?

Piga *150*00#

Chagua ‘M-Pawa’ 

Chagua ‘Mkopo’

Chagua ‘Omba Mkopo’

Weka Kiasi

Ingiza PIN

Thibitisha maombi ya mkopo kwa kubonyeza ok. Utapokea ujumbe wa uthibitisho kuwa M-Pawa inafanyia kazi ombi la mkopo.

Mteja atapokea SMS kumfahamisha kuwa ombi limefanikiwa: Ombi lako la mkopo wa M-Pawa limekubaliwa. Salio jipya la M-Pesa ni Tsh XXXX”.

Utapokea SMS nyingine kama ombi halikufanikiwa. Ujumbe huo utaeleza sababu za kukataliwa kwa ombi lako.

Je utalipaje mkopo wa M-Pawa?

Piga ‘*150*00#’

Chagua ‘ M-Pawa'

Chagua ‘Mkopo’

Chagua ‘Lipa Mkopo’

Weka Kiasi

Ingiza PIN

Thibitisha kwenye ujumbe mfano  “Lipa mkopo Tsh. XXXX kasha bonyeza OK.

Uthibitisho utapokelewa kwa maombi yaliokuwaliwa au yaliokataliwa.

 • Kama umeweka akiba ya Tsh 5000 kwenye M-Pawa yako na una mkopoIf you have saved Tsh 5000 in your M-Pawa and have a loan of Tsh 2000 and do not repay within the loan duration (30 days). What happens to the money in your deposit account?

If you do not pay the TSH 2000 within 30 days, the money in your savings account will be frozen to the loan amount and the loan fee (loan amount TSH 2000 loan plus a facilitation fee of TSH 180)

 

You will be able to access any balance above the frozen amount. The frozen amount will be accessible once you pay the loan. However you can continue to deposit money. Note: during the period the frozen savings will continue to earn interest which will be paid into your M-Pawa account after 3 months.

Je inawekana kuwa na mkopo wa M-Pawa zaidi ya mmoja?

Hapana. Unaweza kupata mkopo wa pili kama unalipa mkopo ulionao sasa.

Je ni nini kitatokea kama ukilipa kiasi zaidi ya mkopo unaodaiwa ?

Kiasi unachodaiwa kitapelekwa kwenye malipo ya mkopo na kile kilichozidi kitawekwa kwenye akaunti ya akiba ya M-Pawa

Je ni nini kitatokea kama usipolipa mkopo ndani ya siku 30

Muda wa malipo utaongezwa kwa siku 30 pamoja na riba ya 9% zaidi. Muda unaweza ukaongezwa mara moja tu

VAT ni nini?

VAT ni Value Added Tax. Ni Kodi ya ongezeko la thamani inayokatwa kwenye kila hatua ya uzalishaji wa bidhaa na huduma na wakati wa mauzo kwa mlaji.

Sheria ya VAT ni nini?

Hii ni sheria inafafanua kuhusu maombi na makusanyo , uongozi na usimamizi wa kodi ya ongezeko la thamani

Ni lini sheria hii ilianza kutekelezwa?

Sheria hii ilianza kutekelezwa tarehe 1, Julai,2016

Je ni VAT ni kiwango ngani?

Kiwango cha VAT kinachotumika Tanzania ni 18%

Je ni mhimili gani wa serikali unahakikisha sharia ya VAT inatumika?

Mamlaka ya Mapato Tanzania ina majukumu ya kuhakikisha usimamizi wa makaridio,ukusanyaji na mahesabu ya mapato yote ya serikali kuu na kuhakikisha Taasisi zote za kifedha zinatekeleza sharia mpya ya malipo ya VAT kwa makusanyo yote.

Je sharia hii itabadili nini kwenye taratibu za maombi ya mkopo?

Kulingana na taratibu za TRA, VAT itatozwa kwenye gharama zote zitakatozwa kwenye mkopo wa M-Pawa kuanzia 01/08/2017.

 

Hii inamaana kiasi cha mkopo kitakachohamishwa kwenda akaunti yako ya M-Pesa kitakuwa pungufu ya gharama za ushauri na kodi ya ongezeko la thamani(VAT), ambayo itapelekwa TRA

Je ni kiwango gani cha mkopo kitalipwa baada ya siku 30?

Kiasi ambacho utalipa kabla ya siku 30 ni kiasi cha mkopo ulichoomba

Je nini kitatokea kwenye mkopo nilionao

Kodi ya ongezeko la thamani(VAT) haitakatwa kwenye mkopo ulionao

Je nitatarifiwa pindi nitakapokatwa VAT au malipo ya huduma?

Kabla ya uthibitisho wa maombi ya mkopo, utapokea taarifa fupi itakayoonyesha kiasi gani utakatwa kama gharama kwenye mkopo

 

Vile vile utapokea ujumbe mfupi wenye maelezo ya kiasi gani utakatwa na kiasi gani utalipa ndani ya siku 30 baada ya maombi ya mkopo kukubaliwa

 

Mfano wa maombi ya mkopo:

Kiasi cha mkopo ulioombwa TZS 1,000
Gharama ya huduma(9% ya kiasi cha mkopo) TZS 90
VAT(18% ya gharama ya huduma) TZS 16.20
Kiasi kitakachwekwa kwenye akaunti ya M-Pesa TZS 893.80
Kiasi cha mkopo kitakacholipwa TZS 1,000

Je sheria hii itatumika kwenye huduma za M-Pawa

Ndio. M-Pawa ikata gharama ya 9% kwa kila ombi la Mkopo. Gharama hii inategemea makato ya VAT yatapelekwa TRA. Hakuna mabadiliko kwenye Akiba.

Savings

Je faida gani utapata kwa kusave pesa kwenye M-Pawa?

Utatalipwa faida itokanayo na salio la akiba uliloweka. (Kiwango cha Faida kitahesabiwa kila siku na kulipwa kila baada ya miezi 3)
Bidhaa utakazopewa zinapangwa kulingana kiasi cha akiba kama hapa chini . Hii itategemeana na uthibitisho wa taarifa zako.
Kiasi cha Akiba (Tsh.) Kiwango cha faida (%)
1, 000 - 200,000 2
200,001 - 500,000 3
500,001 - 1,000,000 4
1, 000,000 5

Ni namna gani utatoa pesa kutoka akaunti ya akiba?

Nenda kwenye menu ya M-Pesa

chagua “M-Pawa”
Chagua ‘ Toa pesa kutoka M-Pawa”
Weka Kiasi
Weka PIN ya M-Pesa
Thibitisha taarifa kisha bonyeza 1 kuthibitisha
Subiri SMS ya uthibitisho

Je ni kipi kiasi cha chini cha salio la Akiba la akaunti ya M-Pawa?

Kiasi cha chini kinachowea kubaki kama salio la akaunti ni sifuri. Unaweza kudunduliza hata Tsh 1.

Je ni zipi gharama za huduma?

Hakuna gharama za ziada, hakuna kikomo cha kutoa pesa, hauna kiasi cha chini cha salio na hakuna gharama za kuhamisha salio kati akaunti za M-Pawa na M-Pesa.

Je unaweza kutuma pesa kutoka kwenye akaunti yako ya M-Pawa kwenda kwa akaunti za M-Pawa za watu wengine.

Hapana. Hutaweza kuhamisha pesa kutoka aakaunti yako ya M-Pawa kwenda kewnye akaunti ya M-Pawa ya mtu mwingine. Ingawa unaweza kuhamisha pesa kutoka akaunti yako ya M-Pesa yako kwenda akaunti zao za M-Pesa.

Je unaweza kutumia akaunti yako ya M-Pawa kupitia CBA au tawi la benki nyingine?

Hapana. Utaweza kutumia akaunti yako kwenye simu yako kwa kutumia laini ya Vodacom kupitia menu ya M-Pesa.

Ni kiasi gani cha juu unaweza kuhamisha kutoka M-Pesa kwenda M-Pawa au M-Pawa kwenda M-Pesa?

Viwango vya kikomo vya M-Pesa vitatumika.

Ni mara ngapi unaweza kuweka au kutoa pesa kukoka M-Pesa kwenda akaunti ya M-Pawa?

Unaweza ukafanya maara nyin kadri iwezekanavyo.

Je unaweza kuhamisha pesa kutok akaunti ya M-Pawa kwenda akaunti ya benki kwa kutumia CBA au benki nyingine yoyote?

Hapana. Hii itawezekana tu baada ya kuhamisha pesa kutoka akaunti ya M-Pawa kwenda M-Pesa, kishaa tuma kutoka M-Pesa kwenda benki ziliruhusiwa kwa huduma ya benki kwa kutumia simu.

Je inawezekana kuwa na akaunti zaidi ya moja ya akiba ya M-Pawa?

Ndio, Inawezekana kuwezesha zaidi ya akaunti moja ya M-Pawa,ikiwa tu mteja ana akaunti ya M-Pesa zaidi ya moja. Hii ina maana ana laini zaidi ya moja za Vodacom( kila akaunti moja ya M-Pawa inaunganishwa na laini moja ya simu).

Salio na Taarifa

Namna ya kuangalia salio la akaunti ya M-Pawa

Nenda kwenye menu ya M-Pesa
Chagua "M-Pawa"
Chagua "Salio la Benki"
Weka PIN ya M-Pesa
Subiri ujumbe wenye salio kulingana na taarifa zako

Nawezaje kuomba taarifa fupi za M-Pawa yangu?

Nenda kwenye menu ya M-Pesa
Chagua "M-Pawa"
Chagua "Taarifa Fupi"
Weka PIN ya M-Pesaesa
Subiri ujumbe wenye salio

Nawezaje kuomba taarifa fupi ?

Taarifa fupi ya M-Pawa inaweza kupatikana kutoka Vodacom Shop kwa yule mwenye akaunti
Unaweza kuomba taarifa hizo kwa kujaza fomu
Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa