Wateja wa Vodacom

NAMNA YA KULIPA WAFANYABIASHARA: WATEJA WA VODACOM:

Baada ya kupata huduma kwenye kituo cha huduma kinachokubali M-Pesa(mgahawa, baa, duka, kituo cha mafuta n.k), nenda kwenye menyu ya M-Pesa kupitia *150*00# au aplikesheni ya M-Pesa > chagua Lipa kwa M-Pesa kisha ingiza namba ya Lipa inayoonekana au tambaza kutumia msimbo wa QR inayoonekana. Kisha weka KIASI kama kilivyo kwenye ankara uliopokea na thibitisha kwa PIN ya M-Pesa. Wewe na mfanyabiashara mtapokea SMS papo papo kuthibitisha muamala. Muamala huu ni BURE kwa mteja na mfanyabiashara.

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa