FURAHIA ULIMWENGU MPYA WA MALIPO YA KIDIGITALI TANZANIA

Vodacom kwa kushirikiana na Mastercard® pamoja na BancABC tumekuletea kadi ya kwanza na ya pekee Tanzania inayokuwezesha kununua huduma na bidhaa kutoka kwa wafanyabiashara waliopo duniani kote kupitia M-Pesa.M-Pesa mastercard inakuwezesha kulipia huduma, bidhaa, apps, bookings za mahoteli au safari, maudhui ya kidigitali n.k kutoka kwenye biashara mitandaoni popote duniani zinazopokea malipo kwa Mastercard. Hakika, sasa dunia ni soko mkononi mwako ukiwa na M-Pesa.

 • Jinsi ya kulipa kwa M-Pesa Mastercard
 • Jinsi ya kuweka pesa kwenye kadi
 • Jinsi ya kuona taarifa za kadi
 • Jinsi ya kutoa pesa kwenye kadi
 • Mambo muhimu ya kufahamu

Jinsi ya kulipa kwa M-Pesa Mastercard

Jinsi ya kulipa kwa M-Pesa Mastercard
Ukishachagua bidhaa unazotaka kuweka oda yako kwenye mtandao husika,nenda chini hadi kwenye nembo ya malipo ya Mastercard na chagua hapo,Kisha chukua simu ya Vodacom M-Pesa na fuata hatua zifuatazo

 1. Piga *150*00# chagua Lipa kwa M-Pesa
 2. Chagua M-Pesa Mastercard
 3. Chagua Tengeneza kadi
 4. Utapokea ujumbe mfupi wenye namba ya kadi, namba ya CVV na tarehe ya mwisho ya matumizi ya kadi.
 5. Utapokea ujumbe mfupi wenye namba ya kadi, namba ya CVV na tarehe ya mwisho ya matumizi ya kadi.
Hizi tu ndizo taarifa unazohitaji kukamilisha malipo yako mtandaoni. Jaza kwa uangalifu kwenye mtandao husika na utapata ujumbe wa uthibitisho wa malipo yako.

Jinsi ya kuweka pesa kwenye kadi

Jinsi ya kuweka pesa kwenye kadi

 1. Piga *150*00# chagua Lipa kwa M-Pesa
 2. Chagua M-Pesa Mastercard
 3. Weka kiasi unachotaka kuweka
 4. Weka PIN yako ya M-Pesa
Utapokea ujumbe mfupi kuthibitisha muamala wako. Pia unaweza kutoa pesa kwenye kadi yako na kuzirudisha kwenye akaunti kuu ya M-Pesa.

Jinsi ya kuona taarifa za kadi

Jinsi ya kuona taarifa za kadi

 1. Piga *150*00# chagua Lipa kwa M-Pesa
 2. Chagua M-Pesa Mastercard
 3. Chagua maelezo ya Kadi
Utapokea ujumbe mfupi kuthibitisha muamala wako

Jinsi ya kutoa pesa kwenye kadi

Jinsi ya kutoa pesa kwenye kadi
Fuata hatua zifuatazo kutoa pesa kwenye kadi yako na kuzirudisha kwenye akaunti ya M-Pesa wakati wowote

 1. Piga *150*00# chagua Lipa kwa M-Pesa
 2. Chagua M-Pesa Mastercard
 3. Chagua toa pesa kwenye kadi
 4. Weka PIN yako ya M-Pesa
Utapokea ujumbe mfupi kuthibitisha muamala wako na kuona salio jipya la kadi pamoja na salio jipya la akaunti kuu ya M-Pesa

Mambo muhimu ya kufahamu

1. Nani anastahili kutumia M-Pesa Mastercard?

Wateja wote wa Vodacom waliosajiliwa na M-Pesa wanaweza kutumia M-Pesa Mastercard

2.Je Kuna ada za kutumia M-Pesa Mastercard?

Hakuna ada zozote unapoweka pesa kwenye akaunti yako ya M-Pesa Mastercard au kuhamisha kutoka M-Pesa Mastercard kwenda kwenye akaunti kuu ya M-Pesa. Ada pekee ni zile za malipo kwenye mitandao tu.

3.Je kuna kikomo cha pesa ninazoweza kuweka kwenye kadi yangu?

Kiwango unachoweza kuweka kwenye kadi yako kinategemea kikomo cha akaunti yako ya M-Pesa. Mfano Tsh Milioni 3 kwa wateja ambao wamekamilisha usajili.

4. Nitarudishiwa vipi pesa endapo sitapata bidhaa nilizonunua kwa M-Pesa Mastercard?

Endapo utalipa kwa kadi na mfanyabiashara akashindwa kukupatia bidhaa, Piga simu Vodacom huduma kwa wateja utapewa maelekezo ya kufanya.

5. Kwa maelezo zaidi, vigezo na mashari kuhusu huduma hii tembelea

www.vodacom.co.tz/m-pesa au piga simu huduma kwa wateja kupitia namba 100 BURE.
Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa