• Nini maana ya M-Pesa rudisha muamala?
 • Hatua za kufuata ni zipi?
 • Nani anaweza kurudisha muamala?
 • Kuna gharama zozote za kutumia huduma hii?
 • Mteja naweza kuomba kurudisha miamala ndani ya muda gani?
 • Pesa iliyorudishwa itachukua muda gani?
 • Nini kitatokea endapo Pesa iliyokosewa kutumwa imetumika?

Nini maana ya M-Pesa rudisha muamala?

Nini maana ya M-Pesa rudisha muamala?
Hii ni huduma inayokuwezesha mtumiaji wa M-Pesa kurudisha miamala uliyotuma au kupokea kimakosa.

Hatua za kufuata ni zipi?

Hatua za kufuata ni zipi?

Kuna hatua mbili za kufuata:

  1. Mtumaji wa pesa unaweza kurudisha muamala uliokosewa kama ifuatavyo:

  Utapiga *150*00#>7 Akaunti yangu (Jihudumie)>1 Rudisha muamala>Zuia muamala (Muamala umetumwa kimakosa)>Ingiza namba ya risiti ya M-Pesa ya muamala unaotaka kurudisha au chagua kutoka miamala mitatu ya mwisho. Baada ya hatua hizi muamala utarudishwa na utapokea ujumbe mfupi kukutaarifu kurudishiwa muamala.

  2. Je, mpokeaji anaweza kuomba kurudisha muamala kama amepokea kimakosa?

  Ndiyo mpokeaji atapiga *150*00#>7 atachagua Akaunti yangu (Jihudumie)> 1 Rudisha muamala >Rudisha muamala ( Muamala umepokelewa kimakosa) >Ingiza namba ya risiti ya M-Pesa/ chagua kutoka miamala mitatu ya mwisho. Baada ya hatua hizi muamala utarudishwa na atapokea ujumbe mfupi kukutaarifu kurudishwa kwa muamala.

Nani anaweza kurudisha muamala?

Nani anaweza kurudisha muamala?

Mtumaji au mpokeaji wa pesa kimakosa anaweza kurudisha muamala kwa kufuata maelekezo kama yalivyo hapo juu. Mtumiaji au mpokeaji atatakiwa kutumia namba ile ile ambayo ametumia kutuma au kupokea pesa kimakosa ili kurudisha muamala.

Kuna gharama zozote za kutumia huduma hii?

Kuna gharama zozote za kutumia huduma hii?
Ndio, Mtumaji wa Pesa utakatwa Tsh 60 kutoka kwenye akaunti yako ya M-Pesa

Mteja naweza kuomba kurudisha miamala ndani ya muda gani?

Mteja naweza kuomba kurudisha miamala ndani ya muda gani?
Kama wewe ni mtumaji uliyekosea kutuma unaweza kuomba kurudishiwa muamala ndani ya masaa mawili ya kukosea kutuma Pesa. Kama umepokea kimakosa unaweza kuomba kurudishwa muamala wakati wowote.

Pesa iliyorudishwa itachukua muda gani?

Pesa iliyorudishwa itachukua muda gani?
Miamala yote chini ya laki moja itarudishwa ndani ya masaa mawili wakati miamala yenye thamani Zaidi ya laki moja itachukua masaa 72.

Nini kitatokea endapo Pesa iliyokosewa kutumwa imetumika?

Nini kitatokea endapo Pesa iliyokosewa kutumwa imetumika?
Muamala hautoweza kurudishwa na mteja aliyekosea kutuma atapokea meseji ya kumtaarifu kwamba hatoweza kurudishiwa muamala.

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa