12/09/2018

VODACOM YAINGIA MAKUBALIANO MAPYA NA GOOGLE PLAY STORE KURAHISISHA UNUNUZI WA ZANA (APP)

Mtandao wa simu unaoongoza nchini, Vodacom Tanzania PLC leo imetangaza makubaliano na Google ili kuwapa wateja wake fursa ya kununua maudhui mbali mbali kwenye Google Play store kwa kutumia salio la simu. Huduma hii, ambayo  inapatikana kwa wateja wote wa Vodacom wenye vifaa au simu za Android, inawezesha ununuzi wa programu mbali mbali kwenye Google Play Store kwa kutumia salio la simu kwenye mtandao wa Voda.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi huo, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa Vodacom, Bi. Jacquiline Materu alisema: "Vodacom tunafurahi kushirikiana na Google kuleta njia hii rahisi, nyepesi na ya kuaminika ya malipo kwenye  Google Play Store  kwa ajili ya ununuzi wa zana (app) ama program mbali mbali kwa Watanzania. Hii inaimarisha zaidi azimio letu la kuzidi kuwakaribisha wateja wetu katika ulimwengu wa kidijitali huku tukiwapatia urahisi na thamani kubwa ya kufanya manunuzi mtandaoni.”

Sasa wateja wa Vodacom wenye vifaa ama simu za Android wanaweza kununua maudhui katika Google Play Store, kama programu, michezo, muziki, filamu, maonesho ya TV na vitabu vya kielektroniki kwa urahisi zaidi, kwa kutumia salio la simu kwenye mtandao wa Voda. Hapo awali ni kadi za benki tu ndizo zilikuwa zikitumika kufanya manunuzi hayo.

Materu aliendelea kufafanua kuwa, uvumbuzi huu utarahisisha mchakato wa malipo na kuboresha huduma za Vodacom kwa wateja wake.

“Kama jukwaa la kuwasilisha maudhui, tunabeba jukumu la kutaarifu, kuelimisha na kuburudisha wateja wetu kwa kutumia teknolojia”. Aliongeza kuwa, Vodacom imepiga hatua kubwa kwa kuwezesha majukwaa mbalimbali ya kidijitali na kijamii kuweza kupatikana kirahisi zaidi kwenye mtandao huku wakitengeneza mifumo ya kidijitali yenye kujumuisha kila mtu”

Kwa upande wake, Meneja wa Ushirikiano wa Jukwaa la Android | Afrika kutoka Google Cassandra Mensah-Abrampah, alisema, "Tumefurahi sana kuongeza wigo wa ushirikiano wa malipo ya moja kwa moja baina ya  Google Play Direct na Vodacom Group ikiwa ni pamoja na kufanya uzinduzi huu na Vodacom Tanzania. Ulipaji kupitia muda wa hewani ni mojawapo ya nguzo muhimu katika huduma jumuishi za kifedha kupitia uuzaji wa zana (app) ama programu katika masoko kwa sababu  watu wengi bado hawajaweza kuziuza.”

Wateja watakaopenda kutumia njia hii bora ya malipo wanahitaji kufanya ifuatavyo: Ingia kwenye Google Play Store > Chagua content (Games/Apps or Movies) nenda kwenye Buy option > kisha chagua Vodacom Airtime billing as mode of payment, kisha utahitajika kuingiza taarifa zako binafsi na kuendelea na malipo baada ya kuthibitishwa. Hatua hizi zinahitajika kwa ununuzi wa kwanza tu. Malipo mengine yote yatakuwa ni ya moja kwa moja baada ya kuchagua mfumo wa malipo wa kutumia salio la simu kwenye mtandao wa Voda.

Mwisho…

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa