30/07/2019

M-pesa yawapa unafuu wasafiri wa anga

Wateja wa M-Pesa na Turkish Airline kupata ofa ya asilimia 15

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airlines), wametangaza ofa ya punguzo la bei kwa asilimia 15 kwa kila mteja atakaye nunua tiketi kutoka shirika hilo kupitia huduma ya M-Pesa, Ofa hii ni kuanzia tarehe 1 mwezi wa nane mpaka tarehe 1 Disemba mwaka huu. Ofa hii ilitangazwa katika hafla fupi iliyofanyika ofisi za Ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu na Mkurugenzi wa  M-Pesa Bwana Epimack Mbeteni.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa  Vodacom Business Unit, Arjun Dhillon, M-Pesa Vodacom Tanzania, Epimack Mbeteni , alisema ubia huo umelenga kuchochea malipo ya kifedha kupitia njia za kidijitali kwa kuwawezesha wateja wao kufanya malipo kwa urahisi wanaponunua tiketi za ndege kutoka shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airline) na kuelekea sehemu yeyote duniani wakianzia safari zao Tanzania.

“Tuna wajibu wa kutengeneza bidhaa na huduma za kifedha ambazo zinakidhi mahitaji ya watu binafsi na biashara, kama shirika la ndege la Ututurki. Ulipaji kupitia M-Pesa ni njia rahisi zaidi ya kufanya malipo; wateja wetu watafurahia faida za kulipia tiketi zao mda wowote na wakati wowote kupitia M-Pesa ukizingatia wanazawadiwa pindi wanapofanya malipo”, alisema Arjun

Akizungumza juu ya ofa hiyo Mkurugenzi wa shirka la ndege la Uturuki nchini, Ahmet Sahin, aliwapongeza Vodacom kwa kutumia teknolojia yao kuchochea huduma za kidijitali nchini. Sahin aliongeza kuwa huduma hii ni yakipekee kwa wafanyabiashara nchini Tanzania kulipia usafiri wa ndege kwenda Uturuki au maeneo 312 ambayo ndege zake zinafika, pamoja na kufaidika kibiashara na kujionea vitu ambavyo nchi zingine zinafanya (exposure).

“Wateja ambao watanunua tiketi za shirika la ndege la Uturuki kuanzia tarehe moja mwezi wa nane mpaka Disemba mosi watapata, sio tu pungufu ya bei kwa asilimia 15% kwa safari zote zinazoanzia Dar es Salaam, Zanzibar na Kilimanjaro, bali pia watafurahia huduma zinazotolewa kwa masaa 24 kutoka kwa watoa huduma wetu nchini kote. Napenda kuwahimiza wafanyabiashara, watalii na wateja wetu wote kutumia fursa hii,” alisistiza Sahin.

Shirika la ndege la Uturuki linaruka kwenda maeneo 312 katika nchi 126 duniani na ofa hii inahusu safari zote zinazoanzia nchini Tanzania kuelekea maeneo hayo.

Vodacom Tanzania Plc inaendeleza nia yake ya kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anafaidikia na huduma bunifu zitokanazo na mtandao wa simu, vile vile kufungua fursa za kidijitali kwa Watanzania hasa wakati huu tukielekea kuinua uchumi wa nchi kuwa wa kati ifikapo mwaka 2025.

Mwisho.

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa