30/10/2019

 

                                                                                       Vodacom yaboresha mfumo wa huduma kwa wateja

  • Yaja na  menu ya USSD  kwa  huduma binafsi   
  • ‘Cutomer Service’ sasa kuitwa ‘VODACARE’

Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania PLC, hivi karibuni iliadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, kwa kutangaza mabadiliko katika mfumo wake wa huduma kwa wateja. Lengo la mabadiliko hayo ni kutoa uhuru kwa wateja wake kupata huduma kwa urahisi pale inapotakiwa.

“Tuna zaidi ya njia nane ambazo mteja anaweza kuzitumia kutufikia na leo tunaiongeza nyingine ambayo itampa mteja fursa ya kujihudumia; hii ni menu ya USSD, ambayo inapatikana katika simu,” alisema Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, Harriet Lwakatare

Kwa kupiga *149*01# mteja anaweza kufanya miamala ya M-Pesa, kuangalia taarifa za matumizi, kupata huduma muhimu kama vile kununua Luku, kuangalia salio, kifurushi cha intaneti na taarifa kuhusu bidhaa mbalimbali za Vodacom.  

“Kwa idadi ya zaidi ya wateja milioni 14, kitengo cha huduma kwa wateja ni kati ya vitengo vyenye kazi muda wote. Vodacom inaendelea kukua kiteknolojia na kuwapa huduma ya kidigitali wateja wake ili kutoa huduma endelevu kupitia njia kadha wa kadha.

“Tunajali mahitaji ya wateja kwa huduma bora na ya haraka. Ndio maana hatujachoka kufanya kazi na kuendelea kuwapa wateja wetu kilicho chaguo kwao na hasa linapokuja suala la kuhitaji msaada. Tuna huduma kwa wateja kwa njia ya kidigitali kupitia WhatsApp, Mitandao ya kijamii, maelekezo kwa njia ya sauti (IVR) na mawasiliano ya moja kwa moja. Na sasa tunawaletea menu ya USSD kwa ajili ya huduma kwa wateja,” alisema Harriet.

Katika hatua nyingine, Harriet alisema kuwa, kuanzia sasa njia zote za mawasiliano zitakuwa zikifahamika kama VODACARE na sio kama awali ilipokuwa ikifahamika kama Vodacom Customer Service.

“Tunafanya hivyo ili kuendelea kutoa huduma kwa mteja mmoja mmoja lakini pia ya kipekee kwa wateja wetu. Tumebadilisha jina la Customer Care kwenda VODACARE sambamba na maboresho ya kiwango cha juu tuliyoyafanya katika kitengo cha huduma kwa wateja,” alisema Harriet

Huduma za VODACARE zinapatikana kwa mteja kupiga 100/01 kwenda kituo cha huduma au kwa kutumia mitandao ya kijamii; WhatsApp, mawasiliano ya moja kwa moja au My Vodacom App, menu ya msaada binafsi na katika maduka yote ya Vodashops na kupitia dawati la huduma.

“Kwa hiyo usijeshangaa utakapopiga 100/101 na kukutana na salamu ya Karibu Vodacare au ukaona maduka yetu yameandikwa VODACARE,” alisema  Harriet

 Aliongezea kusema “Wiki hii Vodacom si kwamba inasherehekea nguvu ya huduma bora kwa wateja kama sehemu ya maudhui yake, ila tunasema kwamba ukiwa na Vodacom matumizi na upatikanaji wa msaada wa huduma kwa mteja ni rahisi wakati wote kupitia katika njia zetu zote za mawasiliano,” alimalizia kusema  Harriet.

Mwisho .

 

 

 

 

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa