01/11/2019

Vodacom yazindua Smart Kitochi, Simu janja ya kwanza Tanzania inayopatikana kwa bei rahisi kutoka KaiOS

  • Simu inapatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini
  • Wateja kupata data, muda wa maongezi na SMS bure kwa miezi 6 ya kwanza

Kampuni inayoongoza kwa teknolojia ya Mawasiliano Tanzania, Vodacom, leo inatangaza uzinduzi wa simu mpya inayofahamika kwa jina la Smart Kitochi. Simu hii inatumia KaiOS, mfumo ambao unaongoza duniani katika teknolojia ya simu janja.

Uzinduzi huu unaongeza hatua kubwa si kwa kampuni hizi mbili tu, bali hata kwa nchi. Ni simu janja ya kwanza kupatikana katika soko nchini Tanzania kwa kiasi cha Tsh 48,000 (takribani dola 20 za Marekani) ikiwa na kifurushi cha GB 4, dakika 100 za maongezi na SMS 500 kwa kila mwezi kwa miezi sita ya kwanza.

Smart Kitochi inatumia zana muhimu kama vile WhatsApp, Google Assistant, Facebook, YouTube na nyingine nyingi zikiwapa fursa watanzania kujiunga na huduma ya intaneti. Ikiwa na sifa zote za simu janja kama vile kuwa na Wi-Fi, GPS, simu hii ina uwezo wa kutumia laini mbili zenye uwezo wa uhifadhi wa GB 4 + MB 512. Pia ina betri yenye nguvu ya mAh 1400 na kudumu saa sita. Ikiwa inazinduliwa leo hapa nchini, simu hii pia itaanza kupatikana katika nchi nyingine za Afrika hivi karibuni.

 “Tuna furaha kuwaleteeni simu hii mpya sokoni kwa ushirikiano na mshirika wetu KaiOS Technologies,” anasema  George Lugata, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na usambazaji wa Vodacom Tanzania Plc. “Pamoja na uwepo wa matumizi  makubwa katika mtandao wa mawasiliano nchini, bado tunakumbana na changamoto za kidijitali kwa sababu ya uwepo mdogo wa matumizi ya simu janja, kwa kufanya hivyo tunawaletea Smart Kitochi kwa bei nafuu kwa kila mtu.”

KaiOS inatumia mfumo mwepesi kabisa ambao una sifa zote za simu janja ambazo ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutosha wa uhifadhi. Pamoja na sifa hizo simu hiyo inatumia mifumo  ya 3G na 4G/LTE, Wi-Fi, GPS, pamoja na NFC.

Simu ya KaiOS inakuja ikiwa na apps maarufu kama WhatsApp, Google Assistant, Facebook, YouTube, and Google Maps. Halikadhalika simu hii ina app ya KaiStore, ambayo ni kati ya apps zaidi ya 200 zinazotumiwa na watoa huduma mbalimbali wa mawasiliano duniani.

 KaiOS Technologies ni ya tatu kwa ukubwa duniani katika mfumo wa utoaji huduma za mawasiliano ya kidigitali, ikiwa na zaidi ya aina 100 za vifaa vinavyosambazwa katika Mabara ya Ulaya, Afrika, Asia na Marekani.

“Mgawanyiko wa matumizi ya mfumo wa kidigitali Afrika bado ni mpana. Tumejikita zaidi katika kutoa fursa pamoja na kuleta teknolojia mpya yenye utatuzi wa mambo mbambali na ndiyo maana tumeamua kufanya kazi na Vodacom. Smart Kitochi ni hatua moja muhimu katika kuuwaunganisha wale ambao walikuwa nyuma katika matumizi ya inteneti na rasilimali zote muhimu za mawasiliano nchini na kwingineko’” anasema Afisa Mtendaji Mkuu wa KaiOS Technologies, Sebastien Codeville.

“Simu ya Smart Kitochi inapatikana katika maduka yote ya Vodashop nchini na katika vituo vyote vya huduma na mauzo ya bidhaa zetu nchini kote kwa bei ya punguzo ya Tsh 48,000. Niwaombe Watanzania na hasa wateja wetu kujitokeza kununua simu hii  ili waweze kufurahia huduma za Mtandao Supa na kufurahia zana kama vile Facebook, WhatsApp, YouTube, Instagram na nyingine nyingi zinazopatikana katika simu janja,” alihitimisha Lugata.

Mwisho

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa