HUDUMA NYINGINE MAPITIO

 • Tafadhali Nipigie
 • Tafadhali Niongezee Salio
 • Kuhamisha Salio
 • Soka Letu – Maswali yaulizwayo mara kwa mara
 • Soka Letu- Vigezo na Masharti

Tafadhali Nipigie

Huduma ya BURE kwa wateja wa Vodacom kuomba kupigiwa simu kutoka kwa wateja wa mtandao wowote wa simu za mkononi nchini kwa njia ya SMS.

Hii huduma ni kwa wateja wote wa malipo kabla(prepaid) na malipo baada (Postpaid).

NB: Tuma BURE mpaka mara 5 tu kwa siku.

Jinsi ya Kutumia huduma

Kupitia tovuti ya Vodacom:
 • Fungua www.vodacom.co.tz
 • Bonyeza Huduma
 • Chagua Huduma Nyingine
 • Chagua Tafadhali Nipigie
Kupitia Aplikesheni ya Vodacom:
 • Bonyeza menu ya Hamburger
 • Bonyeza Huduma Nyingine
 • Chagua Tafadhali Nipigie
Kupitia menu ya Simu:
 • Piga *149*01#
 • Chagua Shangwe + Huduma
 • Chagua Huduma kwa Wateja
 • Chagua Tafadhali Nipigie

Tafadhali Niongezee Salio

Ni huduma ya BURE kwa wateja wa Vodacom wa malipo kabla(Prepaid) kuomba kuongezewa salio kutoka kwa mteja mwingine wa Vodacom kwa njia ya SMS.

Huduma hii ni kwa wateja wa malipo kabla wa Vodacom.

NB: Tuma BURE mpaka mara 5 kwa siku

Jinsi ya kutumia huduma

Kupitia tovuti ya Vodacom:
 • Bonyeza www.vodacom.co.tz
 • Chagua Huduma
 • Chagua Huduma Nyingine
 • Chagua Tafadhali Niongezee Salio
Kupitia Aplikesheni ya Vodacom:
 • Bonyeza menu ya Hamburger
 • Bonyeza Huduma Nyingine
 • Chagua Tafadhali Niongezee Salio
Kupitia menu ya Simu:
 • Piga *149*01#
 • Chagua Shangwe + Services
 • Chagua Huduma kwa Wateja
 • Chagua Tafadhali Niongezee Salio

Kuhamisha Salio

Ni huduma kwa wateja wa Vodacom wa malipo kabla inayowaweza kuhamisha salio kwa wateja wengine wa Vodacom wa malipo kabla. Unaweza kuhamisha salio mpaka Tsh 50,000.

Mteja anaehamisha salio ni lazima awe na kiasi kisichopungua Tsh54 kwenye simu yake.

Jinsi ya kutumia huduma

Kupitia tovuti ya Vodacom:
 • Bonyeza www.vodacom.co.tz
 • Chagua Services
 • Bonyeza Huduma Nyingine
 • Chagua Kuhamisha Salio
Kupitia Aplikeshaeni ya Vodacom:
 • Bonyeza Hamburger menu
 • Bonyeza Huduma Nyingine
 • Chagua Kuhamisha Salio
Kupitia menu ya Simu:
 • Piga *149*01#
 • Chagua Shangwe + Services
 • Chagua Huduma kwa Wateja
 • Chagua Kuhamisha Salio

Soka Letu – Maswali yaulizwayo mara kwa mara

1.Je ni namna gani mteja atajiunga na Huduma ya SOKA LETU?

Kujiunga, mteja atapiga * 149*84# .

2.Je ni nani anastahili kujiunga hiduam ya SOKA LETU?

Wateja wote wa Vodacom wanastahili kujiunga na huduma ya SOKA LETU.

3.Nitapata nini kwa kujiunga na Huduma ya SOKA LETU?

Mteja atapata dondoo za timu mbalimbali, taarifa, historia ya ligi kuu ya vodacom,ratiba za michezo, matokea na vingine vingi.

4.Ni faida zipi mteja anapata akiwa kwenye huduma ya SOKA LETU?

Mpema baada ya kuijunga mteja atapa huduma hii BURE kwa siku 3, atapata dakika 5 Voda-Voda atakaiwa kupiga *149*84*05 kuzitumia na pia atapata pointi kama ifuatavyo:

 • Mteja atapata pointi 1000 kama hajanunua kifurushi cha PinduaPindua au RED RLX
 • Mteja aliyenunua kifurushi cha PinduaPindua atapata pointi 2000
 • Mteja alienunua kifurushi cha RED RLX atapata pointi 5,000.

Pia mteja anaweza kushinda tiketi kuangalia timu aipendayo ikicheza uwanjani au kuapata nafasi ya kukutana na mchezaji ampendae kwa kumpigia kura mchezaji bora na kuongeza nafasi ya kushinda zawadi kwa kupokea pointi zaidi!

5.Je mteja atawezaje kutumia dakika 5 za voda-voda atakazopewa?

Mteja atapiga *149*84*05# ili kutumia dakika 5 za Voda-Voda#

6.Je mteja atawezaji kumpigia kura mchezaji bora na kushinda?

Mteja atakaribishwa na kupewa maelekezo namna ya kupiga kura kwa mchezaji bora kupitia namba 15389.

Mteja atatuma jina la mchezaji kwenda 15386 na kupokea pointi wakati wa kupiga kura.

7.Je mteja atagharamia kiasi gani kwa kujiunga na huduma ya SOKA LETU?

Siku 3 za mwanzo zitakuwa bure! Baada ya hapo mteja atatozwa gharama ya Tsh 100 kwa siku itatozwa.

8.Nani anastahili kupta zawadi mbalimbali za SOKA LETU?

Zawadi mbalimbali zitatolewa kwa wateja waliojiunga na kulipia gharama ya huduma ya SOKA LETU na watapata pointi zaidi zitakazowaongezea nafasi ya ushindi kwa kumpigia kura mchezaji wamendae.

9.Je mteja atapataje taarifa zaidi za huduma ya SOKA LETU?

Mteja atapiga *149*84*01#

10.Je mteja atajiondoaje kwenye huduma ya SOKA LETU?

Kujiondoa kwenye huduma, mteja atapiga *149*84*03#.

11.Je mteja atapoteza pointi zake kama akiamua kujiondoa?

Mteja hatapoteza pointi lakini hataweza kumpigia kura mchezaji ampendae na kushinda Zawadi mbalimbali

Masharti na Sheria za Huduma ya SOKA LETU

Maelezo ya Huduma:

Huduma ya SOKA LETU hupatia wateja taarifa kupitia ujumbe mfupi na nafasi ya kupigia kura mchezaji maarufu wanaompenda. Huduma hii hutumia njia ya usajili wa kila siku huku siku za kwanza 3 zikiwa ni bila malipo. Baada ya kujisajili, mteja hujishindia dakika tano za maongezi ndani ya mtandao wa Vodacom. Mteja anapojisajili kwa aina yoyote ya kifurushi cha “Fuata timu yako”, atashinda dakika tano za maongezi katika mtandao va Vodacom kila mara timu yake inaposhinda katika SOKA LETU (masharti ya kuingia yamo ndani ya maelezo haya). Kulingana na sehemu ya wateja aliyopo mteja yupo, matukio anayoyapata ni tofauti. Visehemu tofauti pia zitapata zawadi tofauti nazo ni Base, Pindua Pindua na Red.

Wateja wanaweza kujisajili kwa kupiga *149*84#

Kwa wateja wanaojisajili kwa mara ya kwanza, wataunganishwa siku tatu za kwanza bure. Mteja anapojisajili, afute usajili kasha ajisajili tena, hatakuwa amestahiki kupata usajili wa siku tatu bure tena.

Siku ya tatu ya huduma ya bure, mteja atapata ujumbe wa ukumbusho kuwa huduma ya bure itakatika na atalipishwa kuanzia siku ufuatayo na kumpa nafasi ya kuchagua kama anataka kufuta usajili. Ikiwa hataufuta usajili, maana yake ni kuwa amekubali kulipishwa kuanzia siku ifuatayo ili afurahie huduma hii ya usajili.

Malipo ya usajili ni 100 Tsh kwa siku. Vodacom kwa muda wowote inaweza kutoa huduma hii kwa wateja na gharama hizi zilizopunguzwa;

 • 3Tsh
 • 5Tsh
 • 7Tsh
 • 10Tsh
 • 20Tsh
 • 50Tsh
 • 75Tsh

Baada ya usajili, mteja anaweza piga simu ndani ya mtandao wa Vodacom kwa dakika tano bila malipo. Ili kukomboa muda huu wa maongezi, mteja anafaa kupiga *149*84*05#.

Mteja atapata ujumbe mfupi wenye taarifa ikiwa ni mteja anayeshiriki. Mteja anayeshiriki ni yule anayefurahia siku tatu za huduma ya bure ama yule anayelipa usajili kwa malipo yaliyotajwa hapa juu. Mteja asiyelipa hatastahiki kupata taarifa ile siku ambayo hakutozwa malipo ya huduma.

Mteja anaweza kufuta usajili wa huduma kwa kupiga *149*84*03#

Mteja anaweza kwa wakati wowote kupata maelezo ya usajili wake yakiwemo maelezo ya pointi zake na pia jinsi ya kufuta usajili kwa kupiga *149*84*01#.

Wateja wataalikwa muda kwa muda kupigia kura mchezaji maarufu wa SOKA LETU. Mteja anaweza tuma jibu kupitia ujumbe mfupi kwa 15389 ili kushiriki katika kura. Wateja wanaweza piga kura mara moja tu katika kila raundi.

Fafanuzi za Sehemu:

 • Mteja anayenunua kifurushi chochote cha Vodacom Red, mara moja au zaidi tangu kujisajili kwa huduma ya SOKA LETU atakuwa katika sehemu ya Red.
 • Mteja anayenunua kifurushi chochote cha Vodacom Pindua Pindua, mara moja au zaidi tangu kujisajili kwa huduma ya Ligi kuu ya Vodacom atakuwa katika sehemu ya Youth, bora asiwe amenunua kifurushi cha Red katika maisha ya usajili wake wa Huduma ya SOKA LETU.
 • Mteja ambaye hajawahi nunua vifurushi vilivyotangulia hapa juu atakuwa katika sehemu ya Mass.

Wateja watapata nafasi kushinda zawadi tofauti muda kwa muda kutoka SOKA LETU ikilingana na sehemu ya wateja waliopo.

 • Sehemu ya wateja ya Mass watastahiki kuingia kwenya droo ya raffo kushinda tiketi ya mechi.
 • Sehemu ya wateja ya Youth watastahiki kuingia kwenya droo ya raffo kushinda jezi ya Ligi kuu ya Vodacom.
 • Sehemu ya wateja ya Red watastahiki kuingia kwenye droo ya raffo kushinda tiketi ya VIP ya mechi.
 • Sehemu zote za wateja zitastahiki kuingia kwenye droo ya raffo ili kukutana na mchezaji maarufu zaidi aliyetangazwa kupitia kura.

Ili wateja waweze kustahiki kuingia kwenye droo ya raffo, lazima wawe wametozwa malipo mara moja au zaidi katika kipindi hicho cha raffo. Vodacom itatangaza raffo kwa wateja kupitia ujumbe mfupi katika msimu wa usajili wa mteja.

Ili wateja wastahiki kuingia kwenye droo ya raffo ya kukutana na mchezaji maarufu aliyetangazwa, sharti wawe wameshiriki katika upigaji wa kura na kumpigia kura mchezaji maarufu aliyetangazwa kwa kupata uzito zaidi wa kura.

Kura ya mteja kutoka sehemu ya Mass itakuwa na uzito wa 1.

 • Kura ya mteja kutoka sehemu ya Red itakuwa na uzito wa tano.
 • Kura ya mteja kutoka sehemu ya Youth itakuwa na uzito wa 2.
 • Kura ya mteja kutoka sehemu ya Mass itakuwa na uzito wa 1.

Mshindi wa raffo atachaguliwa bila kutumia mchakato wowote, wateja wanaweza kuongeza nafasi za kushinda katika raffo kwa kupata pointi kupitia mchakato huu wa pointi (kila pointi ni sawia na nafasi moja ya kushinda katika droo ya raffo):

Pointi anazopata mteja anapojisajili Sehemu ya Wateja ya Mass 1,000
Sehemu ya Wateja ya Youth 2000
Sehemu ya Wateja ya Red 5000
Pointi anazopata Mteja anapoboresha sehemu yake. (Uboreshaji unakubaliwa mara moja tu) Mteja anapoboresha kutoka kwa Sehemu ya wateja ya Mass hadi Youth kwa kununua kifurushi cha Pindua Pindua. Pointi za mteja zinazidishwa mara mbili.
Mteja anapoboresha kutoka kwa Sehemu ya wateja ya Mass ama Youth hadi Red kwa kununua kifurushi cha Red Pointi za mteja zinazidishwa mara tano
Pointi mteja anazopata akipiga kura Mass 1,000
Youth 2000
Red 5000
Pointi mteja anazopata baada ya kutozwa malipo ya huduma M/MY/MR 1,000
Youth 2000
Red 5000

Mteja anaweza kushinda mara moja tu katika raffo moja.

Vodacom itakuwa na uhuru wa kubadilisha masharti haya wakati wowote na kumjulisha mteja. Mteja atakapoendelea kuitumia huduma hii atakuwa amekubaliana na msharti mapya yaliyowekwa.

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa