Huduma Binafsi

1.Nini maana ya vifurushi hivi?

  • Ni vifurushi kwa matumizi ya intaneti tu.
  • Vifurushi vyote hivi ni kwa matumizi ndani ya Tanzania tu. Nje ya Tanzania, matumizi yote ya intaneti yatakatwa kulingana na gharama za kuzuru
  • Gharama za matumizi nje ya kifurushi ni Tsh.282 kwa MB.

2.Je ni upi ukubwa na gharama za vifurushi?

Muda wa matumizi Bei Kifurushi cha Intaneti
Saa 24 Tsh 500 70MB
Tsh 1000 Whatsapp
Tsh 1000 200MB
Tsh 2000 1GB
Siku 7 Tsh 1000 Whatsapp
Tsh 3000 500 MB
Tsh 5000 1GB
Tsh 8000 2GB
Tsh 15000 10GB
Siku 30 Tsh 5000 Whatsapp
Tsh 5000 500 MB
Tsh 15000 2GB
Tsh 35000 10GB
Tsh 50000 20GB
Tsh 95000 50GB
Usiku 2 Tsh 1500 4GB

Gharama za Malipo kabla ni Tsh 282 kwa MB

Kiwango cha chini cha malipo kwa uniti kwa matumizi kwa Malipo kabla ni kwa KB 150

Kiwango cha chini cha malipo kwa uniti kwa Intaneti ya Malipo Kabla ni kwa KB 100

Gharama zote ni kwa Tsh pamoja na kodi.

3.Namna gani wateja wataweza kununua vifurushi?

  • Wateja wanaweza kununua vifurushi kwa kupiga *149*01#, kisha intaneti.
  • Wateja wanaweza wakanunua kwa ajili ya modem, tableti au kwa marafiki kwa kuchagua”Mnunulie rafiki”. Hii inawezakana tu kama namba ya rafiki haina kifurushi cha intaneti.

4.Je wateja wanawezaje kuona salio la kifurushi cha intaneti?

  • Wateja wanaweza kuona salio la intaneti kwa kupiga *149*60#.

5.Je ni zipi kanuni nyingine za vifurushi vya intaneti?

  • Kifurushi kipya kilicho sawa na kile kilichopo, kitaongeza muda wa matumizi pamoja na salio la kifurushi kipya na cha zamani.
  • Matumizi ya kifurushi yatategemea muda wa matumizi kwa kile chenye muda mfupi wa matumizi kutumika kwanza.
  • Ununuzi wa kifurushi zaidi ya mara moja unakubalika.
Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa