Nipige Tafu – Maswali yaulizwayo mara kwa mara

1. Je ni namna gani mteja ataweza kutumia huduma?

Mteja ataweza kutumia huduma kwa kuingia kwenye menu ya bidhaa ya Vodacom kwa kupiga *149*01# kisha chagua Nipige Tafu au kwa kupiga *149*01*99#

2. Je kuna kiwango cha chini ambacho mteja anatakiwa kukopa

Hapana, hakuna kiwango cha chini kinatchotakiwa wakati mteja anapokopa. Mteja anaweza kukopa kiasi chochote ili mradi wamekidhi vigezo. Kwa mfano mteja aliekidhi vigezo asiye na salio au mwenye salio la Tsh 2000 la muda wa maongezi au ana kifurushi ataruhusiwa kukopa

3. Je kuna kiwango cha chini cha mkopo?

Ndio kiwango cha chini cha mkopo kwa wateja waliokidhi vigezo ni Tsh 400.

4. Je kuna aina ngapi za mkopo na kiasi zilizopo kwenye menu

Mkopo ya muda wa maongezi 1. Tsh 400+Tsh 100 (Ada)
2. Tsh 500+Tsh 100 (Ada)
3. Tsh 750+Tsh 150 (Ada)
4. Tsh 1000+Tsh 200(Ada)
5. Tsh 2000+Tsh 400(Ada)

5. Je gharama/ada za mikopo ni zipi

Kwa mkopo wa Tsh 400 gharama/ada ni 25% na kwa mikopo mingine ni 20%

6. Je ni kipi kiwango cha juu cha mkopo ambacho mteja anaweza kukopa?

Kiwango cha juu kinatofautiana baina ya wateja. Jinsi unavyotumia zaidi ndivyo kiwango cha mkopo kinavyozidi kuwa kikubwa

7. Je ni namna gani malipo au ukusanyaji wa mkopo unavyofanyika?

(a) Pale mteja atakapoongeza salio la muda wa maongezi kwa kutumia njia mbalimbali ( Vocha, M-Pesa, Vodafasta, Akaunti ya Benki, POS n.k) (b) Pale mteja atakaponunua kifurushi kupitia M-Pesa. Nipige Tafu itakusanya mkopo na kiasi kitachobaki( kama kipo) kitawekwa kama muda wa maongezi kwenye salio la mteja/au mteja anayetumiwa kifurushi (c) Pale mteja anapopokea kifurushi kutoka kwa rafiki. Nipige Tafu itakusanya mkopo na kiasi kitachobaki( kama kipo) kitawekwa kama muda wa maongezi kwenye salio la mteja/au mteja anayetumiwa kifurushi

8. Wateja wanawezaje kuangalia salio la mkopo?

Piga *149*01#, chagua Nipige Tafu kisha Salio la Mkopo

9. Je ni sababu zipi zitakazomzuia Mteja kutokidhi vigezo vya kupata mkopo

Kama muda wa mteja kwenye mtandao ni chini ya siku 30
Kama deni la mteja limekaa zaidi ya siku 60
Kama mteja hajatumia mtandao kwa zaidi ya siku 60
Kama mteja amefikia kiwango cha juu cha mkopo

10. Je mteja anaweza kukopa zaidi ya mara moja akiwa ajafikisha ukomo wa mkopo na kulipa kidogo kidogo?

Ndio, kukopa zaidi ya mara moja kunaruhusiwa lakini mteja anatakiwa asizidi ukomo wa mkopo aliopangiwa. Mfano, kama ukomo wa mkopo ni Tsh 2000, mteja anaweza kukopa zaidi ya mara moja kulingana na mkopo.

11. Wateja wanawezaje kuangalia ukomo wa mkopo?

Piga *149*01#, chagua Nipige Tafu kisha Kiwango cha Mkopo
Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa