Pinduapindua

Pinduapindua ni nini?

Pinduapindua ni aina maalum ya vifurushi ambapo mteja anapata uniti zinazompa uhuru wa matumizi.Kwa ufupi mteja akiwa na Pindua uniti anakuwa na uhuru wa kupiga simu,kuberuzi na kutuma sms kwa sababu matumizi ya uniti unajipangia mwenyewe.
Mteja atapata pia huduma zingine za ziada buree: meseji na WhasApp

Kuna tofauti gani kati ya Pindua uniti na vifurushi vya kawaida?

Aina Pindua Uniti Vifurushi vya kawaida
Muundo Uniti Vifurushi kama MB,SMS au dakika
Matumizi Hakuna mchanganuo wa matumizi, mteja anatumia atakavyo Kuna mchanganuo wa matumizi kwa maana ya matumizi ya MB,SMS na dakika
Faida zaidi Whatsapp, facebook and SMS bure Facebook bure kwa vifurushi vya intaneti

Jinsi ya kujiunga na Pindua units

Kujiunga na pindua unit, Unapiga *149*01#>PINDUAPINDUA

Kuna vifurushi vingapi vya Pinduapindua, na je faida zake za ziada ni zipi ?

Vifurushi vya Pinduapindua pamoja na faida za ziada atakazopata mteja akijiunga ni kama ifuatavyo:
Muda wa matumizi Bei(Tsh) Uniti Faida zaidi za BURE
saa 24 1000 75 WhatsApp, Facebook na Habari za michezo BURE
1000 80 WhatsApp, Facebook na Instagram BURE
1000 100 WhatsApp, Facebook na SMS BURE
2000 260 WhatsApp, Facebook na SMS BURE
Siku 7 5000 400 WhatsApp, Facebook na Instagram BURE
5000 500 WhatsApp, Facebook na SMS BURE
10000 1200 WhatsApp, Facebook na SMS BURE
Siku 30 15000 1400 WhatsApp, Facebook na SMS BURE
15000 1800 WhatsApp, Facebook na Instagram BURE
20000 2500 WhatsApp, Facebook na SMS BURE

Mchanganua wa Gharama za pindua units zikoje?

Mchanganuo ni kama ifuatavyo:
Dakika 1 ( Voda - Voda) = Uniti 1
Dakika 1 ( Mitandao yote) = Uniti 5
MB 1 = Uniti 1
SMS 1 = Uniti 1

Je mteja akijiunga na Pinduapindua kipaumbele katika matumizi itakuaje kati ya uniti na zile huduma za ziada za bure?

Kipaumbele katika matumizi itakuwa ni zile huduma za bure za ziada halafu ndo uniti zitatumika.

Inakuwaje pale ambapo Pindua uniti zikaisha kabla ya muda wake?

Wala usihofu,unaruhusiwa kununua tena ili kuongeza uniti zako na vilevile kabla hujanununua uniti zingine utaendelea kufurahia huduma zifutatzo bure kabisa; Whatsapp ,SMS na Faceboook

Inakuwaje pale muda wa matumizi wa pindua uniti umefika mwisho?

Muda wa matumizi unapofikia mwisho mteja ataingia kwenye gharama za kawaidia

Je naweza nunua na kufurahia huduma za bidhaa zingine ukiwa na pindua uniti?

Ndio, unaweza furahia huduma za bidhaa zingine ukiwa na Pindua uniti

Je naweza mnunulia Pindua uniti rafiki?

Ndio unaweza unaweza mnunulia Pindua uniti Rafiki

Je nikimnunulia Pindua uniti Rafiki,pia anaweza pata pia faida za ziada ?

Ndio umnunuliaopo rafiki pia anapata faidia za ziada.

Je vigezo na masharti ni vipi?

Vifuatavyo ni vigezo & masharti.
• Mteja akijiunga atapata Units tu atakazozitumia kupiga simu, kutuma SMS na kuperuzi katika mtandao • Eligibility - Vifurushi hivi ni kwa wateja wa malipo ya kabla tu • Vigezo vingine:

a) Kujua salio mteja atabonyeza *149*60#
b) b) Vifurushi hivi vinapataikana kupitia Menyu yetu ya Vodacom *149*01#
c) c) Muda wa matumizi wa kifurushi ukiisha, gharama za kawaida zitatumika.
Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa