RED FAQs

1.RED ni nini?

Ni mpango wenye vifurushi na Malipo ya jinsi unavyotumia. Vifurushi vina dakika za kutosha za mitandao yote, vifurushi vya intaneti(MB), SMS na dakika za kimataifa.

Wakati wa kununua kifurushi, mteja anaweza kuchagua kununua kifurushi mara moja au kwa kujirudia.

2.Kujirudia ni nini?

Ni huduma mpya ambayo Vodacom imewawezesha wateja kuweka vifurushi wavitavyo kujirudia wakati vinapomaliza muda wa matumizi.

3.Je ni tofauti gani kati ya kujirudia na mara moja?

Ukiwa kwenye kujirudia, kifurushi chako cha bei hihio kitajirudia. Unatakiwa kuwa na salio la kutosha ili kijirudie wakati kile kifurushi cha mara moja hakitajirudia.Mteja atatakiwa kununua upya kwa kupiga *149*01#>RED.

4.Je kuna faida yoyote mteja akiwezesha kifurushi cha kujirudia?

NDIO! Mteja ataweza kuhama na dakika,MB na SMS ambazo hazijatumika pale muda wa matumizi wa kifurushi unapokwisha. Wateja ambao watanunua kifurushi cha mara moja hawataweza kuhamisha dakika, MB au SMS ambazo hakutumika pale muda wa matumizi wa kifurushi unapokwisha.

5.Je ni nanma gani naweza kujiunga na kifurushi cha RED?

  • Unaweza kujiunga na vifurushi vya RED kwa njia mbili
  • Menu ya Bidhaa, Piga *149*01# kisha chagua RED RLX
  • Menu ya M-Pesa, Piga *150*00# >Nunua Vifurushi/Muda wa maongezi > RED + PINDUAPINDUA

6.Ni faida zipi utapata kwa kujiunga na kifurushi cha RED?

Zaidi ya kupata dakika za mitandao yote, vifurushi vya intaneti (MBs), SMS na dakika za kimataifa, utapata pia;

  • Huduma ya Sokoni bure
  • Umuhimu wa kwanza unapowasiliana na huduma kwa wateja
  • Umuhimu wa kwanza unapotembelea Vodashop kwa msaada

7.Je ni namna gani mteja atajua kuwa yeye amejiunga na RED au hajajiunga?

Mteja atajua kwa kupiga *149*73*01# au kupitia menu ya bidhaa *149*01#, chagua RED na kisha akaunti yangu

8.Je naweza kupata faida zinatokazo na RED bila kujiunga na kifurushi cha RED?

HAPANA! Wateja waliojiunga na vifurushi vya RED ndio watakaofaidika na manufaa yote yatokanayo na RED.

9.Je nitapata faida za RED pale vifurushi vya RED vitakakwisha muda wa matumizi?

HAPANA! Utasimama kupokea manufaa yatokanayo na RED pale vifurushi vinapokwisha muda wa matumizi

10.Je vifurushi vya RED ni vipi?

Chini ni vifurushi vya RED
Muda wa matumizi Kifurushi Bei Mitandao yote Kimataifa SMS Intaneti
Siku 7 RED SILVER Tsh 7000 Dk 100 1000 200 MB
RED INTERNET SILVER Tsh 7000 Dk 30 1000 1 GB
RED GOLD Tsh 10000 Dk 200 1000 400 MB
RED INTERNET GOLD Tsh 10000 Dk 30 1000 2GB
Siku 30 RED SILVER Tsh 30000 Dk 600 3000 3 GB
RED GOLD Tsh 50000 Dk 1000 7000 7 GB
RED PLATINUM Tsh 95000 Dk 2500 30 Min 15000 20 GB
RED INTERNET SILVER Tsh 30000 Dk 300 300 5 GB
RED INTERNET GOLD Tsh 50000 Dk 300 300 15 GB
RED INTERNET PLATINUM Tsh 95000 Dk 600 Dk 10 600 30 GB

11.Vifurushi vya nyongeza vya RED ni vipi?

Hivi ni vifurushi vya siku 7 vinavyoweza kununuliwa baada ya kifurushi kuisha. Vinaweza kuwa vyenye dakika au MB au vyenye dakika na MB.

Muda wa matumizi Bei(Tsh) Dakika za Mitandao Yote Intaneti (GB)
7 Days 5000 100
7 Days 5000 2
7 Days 5000 100 3

12.Je ninaweza kununua vifurushi vya nyongeza vya RED bila kujiunga na vifurushi vya RED?

HAPANA! Vifurushi vya nyongeza vinaweza kununuliwa pale unapokuwa na kifurushi cha RED. Kama kifurushi cha RED kikiisha muda wa matumizi, hutaweza kununua vifurushi vya nyongeza vya RED.

13.Je nini kitatokea kama dakika,SMS na MB zitaisha kabla ya kifurushi cha RED kuisha?

Unaweza ukanunua kifurushi kingine cha RED cha aina nyingine katika mwezi huo huo au kununua kifurushi cha ziada cha RED au utumie kwa gharama za malipo kabla (Tsh 1 kwa sekunde) kuimiza mahitaji yako kwa siku zilizobakia.

14.Je gharama za matumizi ya RED ni tofauti na gharama za matumizi ya kawaida ya malipo kabla ?

NDIO. Gharama za matumizi ya RED ni za chini ukilinganisha na gharama za kawaida. Kwa simu zipigwazo ndani ya Tanzania ni Tsh 1.5 kwa sekunde na gharama kwa MB ni Tsh 20.

15.Je ninaweza kununua kifurushi kingine wakati nina vifurushi vya RED?

NDIO. Unaruhusiwa kununua vifurushi vingine uvipendavyo.

16.Je ni lazima kuwezesha huduma ya kujirudia ya RED kabla ya kujiunga na kifurushi cha RED?

Sio lazima kuwezesha huduma ya kujirudia ya RED kabla ya kununua kifurushi cha RED. Lakini ni vizuri kuwezesha huduma hio ili upate faida ya kuhamisha dakika, MB na SMS ambazo hukuzitumia.

17.Je naweza kusitisha huduma ya kujirudia pale nitakapoiwezesha?

Ndio, unaweza kuchagua kusitisha huduma ya kujirudia ya RED wakati wowote na hata pale kifurushi kitapoisha muda wa matumizi. Kifurushi hakitajiwezesha chenyewe baada ya hapo. Utatakiwa kwenye kwenye menu ya bidhaa kununua tena kifurushi.

18.Je ninaweza kununua kifurushi cha RED popote pale Tanzania?

Ndio, unaweza kununua kifurushi chochote cha RED mahali popote Tanzania.

19.Kama sijawezesha huduma ya kujirudia ya RED, je ninaweza kununua kifurushi kama hicho cha RED?

Ndio, unaweza kununua kifurushi kama hicho cha RED na unaweza kununua zaidi ya mara moja.

20.Huduma ya kujirudia itafanyaje kazi pale kifurushi kiatapoisha muda wa matumizi?

Kama huduma ya kujirudia imewezeshwa, utapokea ujumbe mfupi kukukumbusha kuwa na salio la kutosha kwa ajili ya kuwezesha kifurushi chako.

Kama una salio la kutosha na kifurushi chako kikaisha muda wa matumizi, basi kifurushi chako cha RED kitawezeshwa moja kwa moja na utapokea ujumbe mfupi wa kuthibitisha kujiunga.

21.What will happened when I don’t have enough funds for auto renewal? Will I still get the RED bundle and charge me when I recharge my airtime wallet?

If you have insufficient funds in your airtime wallet, auto renewal will not take place and your benefits will also be deactivated.

22.Je nini kitatokea kama sina kiasi cha kutosha kwenye salio kwa ajili kuwezesha kujirudia kwa kifurushi? Je pale nitakapoongeza salio nitakatwa salio na kupewa kifurushi cha RED?

Kama huna salio la kutosha, kujirudia kwa kifurushi hakutafanyika na faida za zote za RED zitaondolewa.

23.Je nini kitatokea kama hutajiunga tena na kifurushi cha RED pale kinapoisha muda wa matumizi?

Pale kifurushi cha RED kinapoisha muda wa matumizi, faida zote za ziada nazo zitakoma.

24.Je naweza kununulia rafiki kifurushi cha RED?

Ndio, unaweza ukamnunulia rafiki na wana familia kifurushi cha RED kupitia muda wa maongezi au M-Pesa kutoka kwenye simu yako

25.Je nikimnunulia rafiki kifurushi cha RED na yeye atapata faida za ziada zitokanazo na RED?

Ndio, utakapomnunulia raiki na yeye atapata faida zote za RED lakini kifurushi hakitaunganishwa tena pale kitakapoisha muda wa matumizi

26.Je ninaweza kupata huduma ya RED ninapokuwa nje ya nchi?

Vifurushu vya RED ni kwa matumizi ya Tanzania tu.

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa