• Safari ya Kwenda AFCON Egypt
 • Jinsi ya kushiriki Soka Letu AFCON
 • Zawadi za Soka Letu AFCON
 • Jinsi ya kujitoa
 • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
 • Masharti na Sheria za Huduma ya SOKA LETU AFCON

Maelezo ya jumla

Soka Letu Ni huduma inayompatia mteja taarifa kuhusu Ligi kuu ya Vodacom kupitia SMS na nafasi ya kumpigia kura mchezaji bora wanaompenda ili aweze kushinda

Pia msimu huu Mteja mwenye pointi nyingi atapata nafasi ya kwenda kuhudhuria AFCON EGYPT

Jinsi ya kushiriki

Jinsi ya kushiriki

1. Mteja atajiunga kwa kupiga *149*84# na kulipia kwa M-Pesa au salio la kawaida kwa kupiga *149*01*54#,*149*01*56# au*149*01*57# na kujiunga kwenye huduma kwa siku 7,10, au 30

2. Mteja atapokea ujumbe kila siku kipindi cha hai cha huduma muda wote anapokua amejiunga

3. Mteja anaweza kwa wakati wowote kupata maelezo ya usajili wake yakiwemo maelezo ya pointi zake na pia jinsi ya kufuta usajili kwa kupiga *149*84*01#.

Faida za kujiunga Soka Letu

Faida za kujiunga Soka Letu

Dakika 5 za bure kupiga Voda kwenda Voda MUHIMU Kuweza kutumia dakika hizi mteja atapiga *149*84*05#.

Siku 3 za mwanzo ni bure kwa wateja wanaojisajili kwa mara ya kwanza

Mteja atatozwa Tsh 100 kila siku baada ya siku tatu za mwanzo.

Kwa kujiunga na Soka Letu, mteja atajiongezea pointi kama ifuatavyo:

 • Mteja mwenye vifurushi vya cheka atapata pointi 1000
 • Mteja aliyejiunga na vifurushi vya Pinduapindua atapata pointi 2000
 • Mteja aliyejiunga na vifurushi vya RED atapata pointi 5000

Mteja mwenye pointi nyingi atapata nafasi ya kwenda AFCON EGYPT

Mteja atapata nafasi ya kushiriki kwenye droo ya kupata tiketi za mechi, kupata jezi za timu aipendayo au kwenda kuangalia timu yake ikifanya mazoezi au kuingia kwenye droo ya kupata tiketi ya kuhudhuria sherehe za kugawa zawadi za washindi wa ligi kuu ya Vodacom

Jinsi ya kujitoa

To Un-Subscribe

Mteja anaweza kufuta usajili wa huduma kwa kupiga *149*84*03# au kwa kutuma ONDOA kwenda 15389

Soka Letu – Maswali yaulizwayo mara kwa mara

1.Je ni namna gani mteja atajiunga na Huduma ya SOKA LETU?

Kujiunga, mteja atapiga * 149*84# .

2.Je ni nani anastahili kujiunga hiduam ya SOKA LETU?

Wateja wote wa Vodacom wanastahili kujiunga na huduma ya SOKA LETU.

3.Nitapata nini kwa kujiunga na Huduma ya SOKA LETU?

Mteja atapata dondoo za timu mbalimbali, taarifa, historia ya ligi kuu ya vodacom,ratiba za michezo, matokea na vingine vingi.

4.Ni faida zipi mteja anapata akiwa kwenye huduma ya SOKA LETU?

Mpema baada ya kuijunga mteja atapa huduma hii BURE kwa siku 3, atapata dakika 5 Voda-Voda atakaiwa kupiga *149*84*05 kuzitumia na pia atapata pointi kama ifuatavyo:

 • Mteja atapata pointi 1000 kama hajanunua kifurushi cha PinduaPindua au RED RLX
 • Mteja aliyenunua kifurushi cha PinduaPindua atapata pointi 2000
 • Mteja alienunua kifurushi cha RED RLX atapata pointi 5,000.

Pia mteja anaweza kushinda tiketi kuangalia timu aipendayo ikicheza uwanjani au kuapata nafasi ya kukutana na mchezaji ampendae kwa kumpigia kura mchezaji bora na kuongeza nafasi ya kushinda zawadi kwa kupokea pointi zaidi!

5.Je mteja atawezaje kutumia dakika 5 za voda-voda atakazopewa?

Mteja atapiga *149*84*05# ili kutumia dakika 5 za Voda-Voda#

6.Je mteja atawezaji kumpigia kura mchezaji bora na kushinda?

Mteja atakaribishwa na kupewa maelekezo namna ya kupiga kura kwa mchezaji bora kupitia namba 15389.

Mteja atatuma jina la mchezaji kwenda 15386 na kupokea pointi wakati wa kupiga kura.

7.Je mteja atagharamia kiasi gani kwa kujiunga na huduma ya SOKA LETU?

Siku 3 za mwanzo zitakuwa bure! Baada ya hapo mteja atatozwa gharama ya Tsh 100 kwa siku itatozwa.

8.Nani anastahili kupta zawadi mbalimbali za SOKA LETU?

Zawadi mbalimbali zitatolewa kwa wateja waliojiunga na kulipia gharama ya huduma ya SOKA LETU na watapata pointi zaidi zitakazowaongezea nafasi ya ushindi kwa kumpigia kura mchezaji wamendae.

9.Je mteja atapataje taarifa zaidi za huduma ya SOKA LETU?

Mteja atapiga *149*84*01#

10.Je mteja atajiondoaje kwenye huduma ya SOKA LETU?

Kujiondoa kwenye huduma, mteja atapiga *149*84*03#.

11.Je mteja atapoteza pointi zake kama akiamua kujiondoa?

Mteja hatapoteza pointi lakini hataweza kumpigia kura mchezaji ampendae na kushinda Zawadi mbalimbali

Masharti na Sheria za Huduma ya SOKA LETU

Maelezo ya Huduma:

1. Soka Letu AFCON kampeni ni kwa wateja wote wa malipo ya kabla wa Vodacom kwa kipindi cha tarehe 1 Juni 2019 hadi 31 Julai 2019

2. Kwa wateja wanaojisajili kwa mara ya kwanza, wataunganishwa siku tatu za kwanza bure. Mteja anapojisajili, afute usajili kasha ajisajili tena, hatakuwa amestahiki kupata usajili wa siku tatu bure tena.

3. Mteja atapata pointi kulingana na kifurushi anachojiunga hii inamaanisha, PinduaPindua (2000), Red (5000) & Cheka (1000) na ataingia droo ya wiki ambayo mshindi mmoja atachaguliwa kushinda kifurushi cha dakika 10,000 za kupiga voda- voda

4. Malipo ya usajili ni 100 Tsh kwa siku. Vodacom kwa muda wowote inaweza kutoa huduma hii kwa wateja na gharama hizi zilizopunguzwa;

 • 3Tsh
 • 5Tsh
 • 7Tsh
 • 10Tsh
 • 20Tsh
 • 50Tsh
 • 75Tsh

5. Mteja hatochajiwa makato ya ziada anapopokea na kujibu maswali, lakini anatakiwa awe amejiunga kifurushi cha soka letu siku husika.

6. Mteja Hai atashiriki kwa kujibu maswali ambayo yatatumwa kila siku kipindi cha Promosheni na kujibu majibu sahihi. Mteja Hai ni yule anaechajiwa kwenye huduma.

7. Ili Mteja ashinde safari ya Kwenda Egypt anatakiwa awe na Passport/Hati ya kusafiria na kuileta ndani ya siku 7 kwa ajili ya kuomba VISA, mteja akishindwa kuleta visa ndani ya siku 7 droo nyingine itachezeshwa na namba ingine itachaguliwa mbadala wa Mshindi.

8. Kama mteja ana pointi nyingi lakini hana Hati/Passport ya kusafiria atashinda dakika 10,000 voda-voda na hatipata nafasi ya kwenda Egypt huku mshindi anayefuata mwenye pointi nyingi atashinda safari hii ya kwenda Egypt kama ana Hati/passport ya kusafiria

9. Vodacom itawasaidia washindi na barua ya Utambulisho wa ushindi wao na kuwasaidia na barua husika ila kukubaliwa kwa maombi ya hati ya kusafiria/passport itakua chini ya bodi/mamlaka husika.

10. Zawadi hii haiwezi kubadilishwa au kupewa kwa mtu Mwingine asiyekua Mshiriki husika alieshinda.

11. Mshindi atatakiwa kuleta kitambulisho chake chochote kinachotambulika kitaifa kama Nida, Mpiga kura, leseni ya udereva kabla ya kutambuliwa kuwa mshindi halali

12. Mshindi atashinda zawadi mara MOJA TU. mfano mshindi akishinda zawadi ya wiki kwa wiki ya kwanza hatoweza kushinda zawadi hii tena kwa wiki zinazofuata

13. Washindi wasiopatikana au kutopokea simu zao mara tatu walipotafutwa hawatokua na sifa za kutetea ushindi wao, na ushindi utaenda kwa mtu anaefuatia

14. Mteja anatakiwa kuwa na Umri wa Miaka 18 na kuendelea ili kushiriki

15. Tunahifadhi haki na taarifa ya awali na sababu ya kubadilisha, kuzuia na / au kukamilisha huduma kwa wewe hasa, au kwa uma kwa ujumla, au kurekebisha masharti haya na hali wakati wowote. Mabadiliko hayo yataonekana kuwa yamekubaliwa  na wewe kama utaendelea kutumia Huduma. Kwa hiyo, wajibu ni wewe kuchunguza masharti haya na hali kwa vipindi vya kawaida (mara kwa mara).

Kwanini utumie soka letu?

 • Shinda nafasi ya kwenda AFCON EGYPT
 • Pata taarifa za papo hapo za ligi kuu kwenye simu yako
 • Jishindie jezi ya timu timu yako uipendayo yenye jina lako
 • jishindie nafasi ya kuangalia mazoezi ya timu yako uipendayo
 • Shinda nafasi ya kuwa mgeni maalum kuangalia timu yako ikicheza

Jiunge sasa na ujiongezee nafasi ya kushinda zawadi nono.

Hakimiliki © 2018 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa