Vodacom, kwa ushirikiano na TPB Bank katika kutambua mahitaji ya wateja wake sasa tumeboresha zaidi huduma ya Songesha ili kukuwezesha kusongesha viwango vikubwa zaidi na kukamilisha miamala ya aina nyingi zaidi pale unapokuwa na salio Pungufu la M-Pesa. Ukiwa na Songesha hakuna kukwama tena kisa salio pungufu.

Songesha na M-Pesa

 • Songesha na M-Pesa
 • Kujiunga na Songesha
 • Kukamilisha muamala wa Songesha
 • Kiwango Cha Matumizi
 • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
 • Vigezo na Masharti
 • Viwango vya Songesha

Songesha na M-Pesa

Songesha na M-Pesa
Ukiwa na Songesha iliyoboreshwa zaidi utaweza kukamilisha miamala mbalimbali ya M-Pesa kama.

 • 1. kutuma pesa mitandao yote.
 • 2. Kulipa bili mbalimbali kama LUKU, Bili za maji na Ving’amuzi nk
 • 3. Kutoa pesa kwa wakala
 • 4. Kununua bando na muda wa maongezi
 • 5. Kuhamisha pesa kwenda benki
 • 6. Kulipa kwa simu kwa wafanyabiashara wenye Lipa namba za M-Pesa n.k.

Hata ukiwa na salio pungufu la M-Pesa, malizia miamala bila kwikwi. Ni rahisi. Piga *150*00# chagua Huduma za kifedha kisha chagua Songesha kujiunga.

Kujiunga na Huduma ya Songesha

Jinsi ya Kujiunga na Songesha na M-Pesa kwa kukubali vigezo na masharti:

Jinsi ya Kujiunga na Songesha na M-Pesa

 1. Piga *150*00#
 2. Chagua Huduma za Kifedha
 3. Chagua Songesha
 4. Chagua 1 kukubali magezo na masharti

Kukamilisha muamala wa kutuma pesa na Songesha

Songesha ni huduma inakuwezesha kukamilisha muamala wako hata ukiwa na salio pungufu. Ni rahisi, anza kufanya muamala husika ukifika mwisho utapokea taarifa fupi isemayo;

“Samahani hauna salio la kutosha kwenye akaunti yako kukamilisha muamala huu. Songesha na M-Pesa Tsh.XXXX, chagua 1 kukubali au 2 kubatilisha. Vigezo na masharti kuzingatiwa.”

Kile kiasi unachopungukiwa kukamilisha muamala husika kitaongezwa na Songesha pindi ukichagua ‘1’ kukubali kukamilisha muamala wako kwa Songesha.

Kiwango Cha Matumizi

Kiwango chako cha matumizi ya Songesha kinaweza kupanda au kushuka kulingana na mwenendo wa matumizi ya Songesha na huduma nyingine za M-Pesa. Ilikuona kiwango chako fuata hatua zifuatazo:

Kiwango Cha Matumizi

 1. PIGA *150*00#
 2. Chagua Huduma za Kifedha
 3. Chagua Songesha
 4. Chagua Kiwango cha matumizi
 5. Weka namba yako ya siri ya M-Pesa

Angalia Salio

Jinsi ya kuangalia salio la Songesha

 1. PIGA *150*00#
 2. Chagua Huduma za Kifedha
 3. Chagua Songesha
 4. Chagua Salio
 5. Weka namba yako ya siri ya M-Pesa

Msaada

Jinsi ya kupata maelezo mafupi kuhusu huduma ya Songesha

 1. PIGA *150*00#
 2. Chagua Huduma za Kifedha
 3. Chagua Songesha
 4. Chagua Msaada

Maswali yaulizwayo mara kwa mara

Je ni vigezo vipi natakiwa kutimiza ili kutumia huduma ya SONGESHA?

Ili kutumia huduma ya SONGESHA inabidi uwe unatumia M-Pesa na mtandao wa Vodacom. Hivyo unatakiwa kujiunga kwa kuingia kwenye menyu ya M-Pesa kisha kukubali vigezo na masharti.

Je ni akaunti ngapi naweza kutumia kujiunga na SONGESHA.

Kila laini ya Vodacom iliyosajiliwa na M-Pesa ikwa angalau miezi mitatu inauwezo wa kutumia SONGESHA. Kama wewe ni mteja mpya wa Vodacom tumia huduma za M-Pesa kwa angalau miezi mitatu uanze kunufaika na huduma hii.

Je kiwango cha Matumizi ni nini?

Hiki ni kiwango cha juu ambacho utaweza kutumia kwenye huduma ya SONGESHA kwa mwezi. Kiwango hiki kitapanda au kushuka kulingana na matumizi yako. Mwenendo mzuri wa marejesho na matumizi ya M-Pesa na Songesha utapelekea kuongozekea kwa kiwango cha Songesha. Mwenendo mbaya utasababisha kushuka kwa kiwango au kukasababishia kufungiwa huduma ya Songesha.

Je ni miamala gani inaweza kukamilshia kutumia SONGESHA?

Ukiwa na Songesha iliyoboreshwa zaidi utaweza kukamilisha miamala mbalimbali ya M-Pesa kama.:

1 - kutuma pesa mitandao yote.
2 - Kulipa bili mbalimbali kama LUKU, Bili za maji na Ving’amuzi nk
3 - Kulipa kwa simu kwa wafanyabiashara wenye Lipa namba za M-Pesa.
4 - Kutoa pesa kwa wakala
5 - Kununua bando na muda wa maongezi
6 - Kuhamisha pesa kwenda benki

Je ntaweza kutumia SONGESHA mara ngapi?

Utaweza kutumia huduma ya SONGESHA kukamilisha muamala mmoja kwa wakati mpka utakaolipa ndipo utakopweza kutumia huduma nyingne ya Songesha.

Je ntawezaje kutumia kiwango changu cha Songesha?

Utatakiwa kufanya miamala ya M-Pesa kama kawaida na pale unapokwa hauna salio la kutosha la kukamilsha miamala iliyoruhusiwa Songesha itatumika kukamilisha muamala huo.

Je kuna gharama/makato yoyote ya kutumia huduma ya SONGESHA?

Unapotumia huduma ya Songesha utalipa Ada ya Maombi: kulingana na kiwango ulichopewa. Ada hii itatozwa mara moja tu kwa kila ombi la huduma ya Songesha. Pia utatozwa ada kwa kila siku inayopita bila ya kulipa huduma ya SONGESHA kulingana na kiwango unachodaiwa.

Vigezo Na Masharti

Bofya kupakua Vigezo na Masharti vya Songesha au bofya alama ya jumlisha kusoma moja kwa moja

Songesha Vigezo na Masharti

M-PESA LIMITED – VIGEZO NA MASHARTI YA SONGESHA NA M-PESA

1. MATUMIZI NA UFAHAMU.

Tafadhali soma Vigezo na Masharti haya, na kiambatanisho/kifungu chochote pamoja na Kanuni na Masharti ya Watumiaji wa M-Pesa kwa pamoja yatakuwa sehemu ya Vigezo na Masharti haya ("Masharti ya Matumizi").

Vigezo na Masharti haya ("Masharti ya Matumizi ") vinanapatikana kwa Watumiaji wa Huduma ya M-Pesa na vitahusika mara moja unapojiunga au kujiandikisha na huduma ya Songesha na M-Pesa ('Huduma').

Songesha na M-Pesa inatolewa kwa wateja hai wa M-Pesa wanaopatikanai katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuzingatia Masharti ya Matumizi haya, chini ya kifungu namba 2.8 na 2.9.

M-Pesa Limited mara kwa mara itahakikisha, nyaraka zako za utambulisho au kurekebisha Masharti ya Matumizi haya au kutathmini/kupitia upya kikomo chako cha Songesha.M-Pesa Limited wanahaki ya kukubali au kukataa ombi lako la huduma ya Songesha na M-Pesa.
2. FAFANUZI NA TAFSIRI.

2.1 "Mkataba" maana yake ni Masharti ya Matumizi

2.2 "Songesha na M-Pesa au Huduma ya Songesha au Huduma" maana yake ni huduma ya fedha ya kieletroniki ya simu ambayo inawawezesha wateja wa M-Pesa kupata huduma ya Songesha ya upataji fedha ya ziada ili kukamilisha miamala yao kila wakati wanapokuwa hawana fedha ya kieletroniki ya kutosha katika akaunti ya M-Pesa na fedha hii italipwa na Mteja pindi anapoweka au kupokea fedha katika akaunti ya M-Pesa (itakatwa moja kwa moja).

2.3 “M-PESA Limited” maana yake ni kampuni ambayo Ofisi Zipo Gorofa ya 7th, Vodacom Tower Ursino Estate Kiwanja No. 23, Barabara ya Bagamoyo S.L.P 2369 Dar Es Salaam, na mtu yeyote au biashara yoyote ambayo inaweza kuhamishiwa haki au majukumu chini ya Mkataba huu..

2.4 "Benki" maana yake ni Kampuni ya Umma ya Benki ya Posta ya Tanzania iiliyoanzishwa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ofisi yake kuu ipo katika Jengo la LAPF, Ghorofa ya 10, barabara ya Bagamoyo Dar Es Salaam, S.L.P 9300 Dar Es Salaam, na ambayo katika muktadha huu inahusisha pamoja na waridhi wake.

2.5 “BOT " maana yake ni Benki Kuu Ya Tanzania.

2.6 "Mteja au Wateja wa M-Pesa" maana yake ni mtumiaji yeyote wa M-Pesa ambaye amesajiliwa kutumia huduma ya M-Pesa na ameingia kwenye makubaliano haya.

2.7 "Kituo cha huduma kwa Wateja” maana yake ni kituo maalumu cha huduma ya mteja kwa mujibu wa mkataba huu.

2.8 "Tukio la Ukiukwaji" linamaanisha hali yoyote iliyohainishwa katika kifungu cha 10 hapo chini.

2.9 "Thamani ya Kieletroniki" au "fedha ya Kieletroniki" inamaanisha pesa ya kieletroniki zilizotolewa na sisi na kuwakilisha kiwango stahili cha fedha taslimu kinachoshikiliwa na mteja kutokana na ununuzi wa thamani hiyo ya fedha ya kieletroniki;

2.10 "Vifaa" vinajumuisha simu yako ya mkononi, Kadi yako ya simu iliyowezeshwa na Vodacom na au vifaa vingine ambavyo vinatumiwa kwa pamoja vinavyowezesha kufanikisha upatikanaji wa mtandao.

2.11 "Upataji Songesha" au "Songesha" maana yake ni upataji wa mkopo unahohusishwa na miamala yako iliyoidhnishwa kwenye M-Pesa Akaunti (unaweza kurejea kifungu cha 9 kwa maelezo), inakuwezesha kutoa / kufanya miamala ya fedha ya kieletroniki kutoka kwenye Akaunti yako ya M-Pesa zaidi ya kiwango chako kilichopo ndani ya viwango kubalika (Kiwango cha Songesha

2.12 "Viwango vya Songesha na M-Pesa" au "Viwango vya Songesha" maana yake ni kiwango cha juu cha upataji Songesha ambacho Mteja anaweza kutumia kwa mwezi.

2.13 "Ada" maana yake ni ada zinazotumika kwa Huduma na ni pamoja na;

 • 2.13.1 Ada ya Uchakataji: (kama ilivyohainishwa kwenye viwango vya ada)
 • 2.13.2 Malipo haya yatakatwa kila mteja anapoomba huduma ya Songesha na M-PESA kikamilifu.
 • 2.13.3 Ada ya Huduma: Inategemea na kiwango ulichopewa na muda utakaochukuwa kulipa deni.
 • 2.13.4 Hii ni ada ya kila siku ambayo mteja atastahili kulipa kulingana na kiasi anachodaiwa. Ada hii ya kila siku itasitishwa siku ya 18.
 • 2.13.5 Malipo mengine yoyote ya Upataji Songesha kama yalivyohainishwa na sisi mara kwa mara kwa mujibu wa Mkataba huu na inajumuisha gharama zozote, na kodi zinazohusika chini ya Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2.14 “Tukio la Ukiukwaji" maana yake ni

 • 2.14.1 Hali ambapo Upataji wa Songesha umekamilika na haujalipwa kwa siku thelathini (30) au zaidi,
 • 2.14.2 Iwapo umefanya uvunjaji wowote au kushindwa kuzifata au kutekeleza, vigezo, maagano ya masharti au masharti ya makubaliano yoyote kati yetu na wewe mwenyewe kuhusiana na Upataji wa Songesha; au
 • 2.14.3 Ikiwa kuna wasiwasi au hofu kwamba hutaweza kulipa madeni yako au tunapokea taarifa yoyote kwamba umekubali kutokuwa na uwezo wowote wa kulipa madeni yako kama ilivyokusudiwa; au
 • 2.14.4 Endapo kwa utaratibu wa kisheria au amri ambatanishi ya mahakama imetolewa dhidi ya amana yako kwenye M-Pesa akaunti au kudaiwa mali inayomilikiwa nawe.

2.15 "Muda wa Kulipa Songesha" maana yake ni pale mbapo hakuna Tukio la Ukiukwaji (kama ilivyoelezwa katika Mkataba huu) ndani ya siku ya thelathini (30) tangu tarehe ya kwanza ya matumizi ya Upataji Songesha.

2.16 "Serikali" ina maana Serikali ya Taifa, Serikali Kuu au Serikali nyingine yoyote iliyowekwa chini ya sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

2.17 "Jua Wateja Wako" pia inajulikana kama KYC ni matakwa yaliyowekwa kisheria dhidi ya Mpesa Limited yanayohusu kumjua na kumfanyia upembuzi yakinifu mteja kama ilivyoainishwa kuagizwa au kupendekezwa na Serikali, Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano ya Tanzania (TCRA) au Benki Kuu ya Tanzania (BOT) mara kwa mara.

2.18 "M-PESA" maana yake ni huduma ya kifedha ya kutuma na malipo ambayo inasimamiwa na kuendeshwa kipekee na M-Pesa Limited nchini Tanzania na kuidhinishwa/kupewa kibali na Benki Kuu ya Tanzania

2.19 “Akaunti ya M-PESA” maana yake ni mfuko maalumu wa M-PESA uliosajiliwa kwa jina lako na unaokuwezesha kujiunga kwenye huduma ya Songesha.

2.20 “M-PESA Data ya Mteja” maana yake ni jina la mtumiaji wa M-PESA na viambatanisho vyake; kadi ya utambulisho ya kitaifa, nambari ya kadi ya mpigakura, namba ya pasipoti au namba ya leseni ya kuendesha gari, kama inavyoonekana mara kwa mara katika mifumo ya M-Pesa Limited Tanzania.

2.21 "Mfumo wa M-PESA" maana yake ni mfumo unganishi wa kiufundi kwa sasa hivi unaotoa huduma ya M-PESA

2.22 “Kadi ya Simu” maana yake ni chombo cha utambulisho wa mtumiaji ambacho kinapotumika na Kifaa kinachostahili cha Simu ya Mkononi kinakuwezesha kutumia Huduma za M-PESA;

2.23 "USSD" maana yake teknolojia ya mawasiliano yenye mfumo wa kimataifa wa Mkononi (GSM) ambayo hutumiwa kutuma ujumbe kati ya simu za mkononi na mfumo maalum wa mtandao. Maombi yanaweza kujumuisha matumizi kabla ya kulipia au huduma za kuzungumza na simu zinazotolewa na Vodacom Tanzania

2.24 “Masuala ya Kiupembuzi ya Mteja”maana yake ni nyaraka za kibinafsi zinazotolewa na wewe kuja kwetu kwa nia ya kuthibitisha jina lako na anwani ya sasa, ili kufikia mahitaji yetu ya kisheria ya kudhibiti.

2.25 "Miamala Iliyoruhusiwa" maana yake ni aina ya miamala ambayo imepewa nafasi ya Upataji wa Songesha mara kwa mara, ambyzo ni pamoja na zifwatazo;

 • 2.25.1 Malipo kutoka kwa Wateja kwenda kwa Mfanyabiashara
 • 2.25.2 Tuma fedha kwa wateja waliosajiliwa na wasiosajiliwa
 • 2.25.3 Malipo ya bili kama vile (LUKU, Malipo ya Serikali zote, Malipo ya Usafiri, Malipo ya Usajili wa TV).

2.26 “Ukurasa wa Tovuti au Tovuti” maana yake ni kikundi cha kurasa zilizounganishwa kwenye habari za Mtandao juu ya somo fulani k.m. www.vodacom.co.tz

2.27 "Mtandao" maana yake ni mfumo wa kimataifa wa mawasiliano wa simu za mkononi ("GSM") mfumo unaondeshwa na Vodacom Tanzania PLC na kufika maeneo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ilivyoelezwa mara kwa mara na Vodacom Tanzania;

2.28 "Matatizo Yasiyozuilika" maana yake ni kitu chochote kisichokuwa na udhibiti wa mtu yeyote yule, ikiwa ni pamoja na majanga, kitendo cha vita au ugaidi, uhamasishaji wa majeshi ya kivita, usumbufu wa kiraia au machafuko, maafa ya asili, maandamano au usumbufu wa kazi (achilia mbali maandamano ya Wafanyakazi wa Mhusika yoyote wa Mkataba huu au washirika wake), kizuizi cha sarafu, kizuizi, au kusitishwa kwa huduma za umma au kushindwa kwa usambazaji wa mawasiliano ya simu au kushindwa kwa mfumo, ucheleweshaji katika uchakataji wa miamala, au ucheleweshaji uliopo nje ya uwezo wetu wa kawaida (ni pamoja na kushindwa kwa nguvu za umeme na kuchelewesha katika mawasiliano na uuzaji katika vituo husika, mtandao au mfumo mwingine na ni pamoja na kushindwa kwa kifaa chako).

2.29 "Sisi," "yetu," na "nasi," inamaanisha M-Pesa Limited na (ikiwa inafaa) Msaidizi;

2.30 “Wewe” au “yako” au “nawe” maana yake ni Mteja na hujumuisha wawakilishi binafsi wa Mteja na warithi

2.31 Maneno yanayowakilisha umoja au wingi yatakuwa sawa na yanaweza kutumika kwa pamoja.

3. KUKUBALI VIGEZO NA MASHARTI

3.1 Kabla ya kuingia au kujiunga na huduma hii, unapaswa kusoma kwa uangalifu na kuelewa Masharti haya ya Matumizi yanayosimamia upatikanaji wa matumizi na uendeshaji wa Huduma. Masharti haya ya Matumizi yanapatikana kwenye tovuti yetu www.vodacom.co.tz .

3.2 Kama hukubaliani na Masharti ya Matumizi haya, tafadhali bonyeza "Sitisha" kwenye huduma ya kujiunga.

3.3 Utaonekana kuwa umeisoma, umeelewa na kukubali Masharti ya Matumizi: Kwa kubonyeza chaguo "Kukubali" wakati wa kujiunga pale inapokuomba uhakikishe kuwa umesoma, umeelewa na umekubali kutekeleza vigezo na masharti haya na utakuwa umekubali Mashart ya Matumizi pia kwa kutumia au kuendelea kutumia na Huduma ya Songesha na M-Pesa.

3.4 Kwa kujiandikisha kwa Huduma hii, unakubali kuzingatia na kufuata Masharti ya Matumizi haya kama yatakavyokuwa yanafanyiwa marejeo na kurekebishwa mara kwa mara na unathibitisha kuwa Vigezo na Masharti hayaathiri haki nyingine yoyote ambayo tunaweza kuwa nayo kisheria au vinginevyo kuhusu usajili wako, upatikanaji na matumizi ya Huduma.

4. KUJIUNGA NA MATUMIZI YA HUDUMA

4.1 Huduma hii inapatikana kwa Wateja, kwa kutumia M-Pesa USSD kuomba kuingia na kwa kufanya hivyo ina maana kwamba unathibitisha kukubali Masharti na Matumizi haya.

4.2 Tuna haki ya kuthibitisha uhalali na hali ya Akaunti yako ya M-Pesa na miamala na tuna hiari ya kusitisha/kukataa maombi yako kwa taarifa au bila taarifa, ingawaje (itambulike kuwa sio wajibu wetu kukujulisha) tunaweza jaribu kukujulisha.

4.3 Unaweza kujiandikisha na Huduma kwa zaidi ya mfumo moja wa MSISDN ingawaje Masharti ya Matumizi yatatatumika kwa kila Akaunti ya M-PESA ambayo imesajiliwa kwa jina lako.

4.4 Unakubali na kutoa mamlaka kwa M-Pesa Limited ya kushirikisha habari zako binafsi tulizonazo kwa Benki kulingana na utoaji wa Huduma hii. Maelezo hayo kibinafsi yanajumuisha bila ya kikomo, pamoja na nambari yako ya simu, jina, tarehe ya kuzaliwa, aina ya Kitambulisho na nambari yake na taarifa nyingine zitakayotuwezesha kutambua na kufuatilia na kukithi maitaji ya udhibiti wa "Jua Wateja wako(KYC)".

4.5 Pia unakubali na kuturuhusu kutumia habari zinazohusiana na matumizi yako ya Huduma ya M-PESA, Huduma ya GSM-(Mtanao wa simu) kwa madhumuni ya kutoa Huduma ("Taarifa za M-PESA").

4.6 Sisi tuna haki ya kuomba taarifa zaidi kutoka kwako kuhusiana na maombi yako ya kujiandikisha kwa Huduma wakati wowote. Kushindwa kutoa maelezo kama hayo wakati tunahitaji kunaweza kusababisha kusitishwa kwa maombi yako ya kujiasajili kwenye Huduma.

4.7 Kukubali au kukataa kwa maombi yako kujisajili kwenye Huduma utafanyika kwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) itakayo tumwa kupitia namba yako ya simu iliyosajiliwa na Vodacom (MSISDN) na inayohusishwa na akaunti yako ya M-PESA na au Vifaa vingine.

4.8 Kwa kukubali Vigezo na Masharti haya, unakubali na kuthibitisha kwamba tuna haki ya msingi na ya kipekee ya kuweka Kiwango Cha Songesha na/au ada yoyote / makato yanayohusiana na huduma hii.

4.9 Unaweza kutumia tu Upataji wa Songesha ili kukamilisha miamala iliyoruhusiwa kwa kupitia M-Pesa USSD kwa kiwango cha fedha ambacho kinapatikana kwenye Akaunti yako ya M-PESA

4.10 Utapata taarifa kukubali Upataji wa Songesha pindi unapokamilisha miamala iliyokubaliwa pamoja na ada zote kulingana na Masharti ya Matumizi.

4.11 Kwa kukubali Vigezo na Masharti haya, unakubaliana na kukiri kwamba tunahaki ya pekee ya kukutuma ujumbe wa maandishi ya matangazo mara kwa mara kuhusiana na Huduma

5. VIWANGO VYA SONGESHA / VIWANGO VYA SONGESHA NA M-PESA

5.1 Baada ya kuingia kwenye Huduma, utapokea ujumbe wa uthibitisho ulio na kiwango cha Songesha.

5.2 Ikiwa haujawekewa Kiwango Cha Songesha, lazima uendelee na matumizi ya M-PESA ili uweze kujenga historia ya matumizi na kuongeza alama yako ya kiupembuzi wa mkopo (credit score) ili uweze kustahili kupata Kiwango Cha Songesha.

5.3 Unaweza kuangalia Kiwango cha Songesha kwa kutumia chaguo sahihi la orodha iliyopo kenye SIMU yako / kwenye vifaa vyako kupitia M-Pesa USSD.

5.4 Mara kwa mara tunaweza kukupangia kiwango cha juu au cha chini cha Songesha iwapo umeomba huduma hiyo, na kiwango hicho kitawasilishwa kwako kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS)

5.5. Viwango vya Songesha vinaweza kupitiwa mara kwa mara na tunahaki ya kupitia tena na kutofautisha Viwango vya Songesha kwa taarifa au bila kutoa taarifa; ingawa (siyo wajibu wetu) tutajaribu kukupa taarifa kuhusu utofauti woyote wa viwango vya Songesha pale itakapobidi.

6. KUOMBA UPATAJI WA SONGESHA

6.1 Unakubali kwamba upataji wa Songesha utapelekea deni kwenye Akaunti yako ya M-PESA, kulingana na dhamani ya kiwango cha Songesha na Ada zote stahiki.

6.2 Ada zote zitajumuhishwa kwenye kiwango cha Songesha na zitalipwa kupitia makato kwenye Akaunti yako ya M-PESA. Ada zitajumuisha ushuru na kodi yoyote inayotambuika, zinazotumika chini ya sheria.

6.3 Kwa kiwango cha Songesha ulichopata, unapaswa kulipa chote ndani ya saa 24, na isizidi siku ya thelathini (30) tangu tarehe ambapo umepata Songesha (tarahe ya kwanza ya kupata Songesha). Hutaweza Kupata Songesha mpya au kuongeza nyingine ikiwa una deni la awali au Umekiuka Masharti na Matumizi ya Songesha

6.4 Unaweza kuomba huduma ya Songesha mara nyingi uwezavyo ndani ya kipindi cha malipo ili mradi maombi hayo hayatazidi Kiwango Cha Songesha ulichoruhusiwa. Ili kupata Songesha ya pili, ni lazima uwe tayari umelipa Songesha ya awali.

6.5 Kulingana na utendaji wako kwenye M-Pesa na Huduma ya Songesha, Viwango vya Songesha vinaweza kuongezwa au kupungua. Utendaji mzuri unaweza kusababisha ukuaji wa Kiwango Cha Songesha. Utendaji mbaya unaweza kusababisha kupungua kwa Kiwango Cha Songesha au kusitisha kabisa.

6.6 Huwezi kutumia Songesha zaidi ya Kwango chako cha juu katika muamala. Ingawa bila kuathiri kifungu cha 6.7 hapo chini inaweza kutokea ukapata Huduma ya Songesha bila kuwa na fedha ya kieletronic kwenye Akaunti yako ya M-Pesa au kupata kiwango kikubwa Zaidi ya kile ulichoruhusiwa. Iwapo hali hii itatotekea, utalazimika kutulipa kwa mujibu wa Masharti ya Matumizi haya.

6.7 Utakuwa na uwezo wa kutumia Kiwango Cha Songesha unapokuwa na salio pungufu kwa Miamala iliyoruhusiwa tu.

7. UKOKOTOAJI WA KIWANGO CHA SONGESHA

7.1 Mifumo ya Kipembuzi ya Benki itatumika kutoa alama ambazo zitaamua Kiwango Cha Upataji Songesha na M-Pesa,

7.2. Kiwango Cha Songesha na muendelezo wa uidhinishaji wetu wa maombi yako ya Songesha kitaamuliwa na alama za kiupembuzi za Benki.. Benki itafanya mahesabu ambayo itaamua Kiwango chako Cha Songesha ambocho kimetokana kulingana na masuala mbalimbali ambayo bila kikomo ni pamoja na matumizi ya huduma za Vodacom, Huduma za M-Pesa na historia ya ulipaji ya Kiwango chako cha Songesha kilichopo.

8. REJESHO LA SONGESHA

8.1 Kiwango cha Songesha ulichopata kinapaswa kulipwa chote ndani ya saa 24, na isizidi siku thelathini (30) tangu tarehe ambapo umepata Songesha (tarahe ya kwanza ya kupata Songesha). Hutaweza Kupata Songesha mpya au kuongeza nyingine ikiwa unadeni la awali au Umekiuka Masharti na Matumizi ya Songesha

8.2 Baada ya kuchukua huduma ya Songesha, akaunti yako ya M-Pesa itawekwa kwenye huduma ya ukataji deni moja kwa moja. Hii inamaanisha kuwa M-Pesa Limited itaondoa moja kwa moja kiasi ulichopokea kwenye akaunti yako ya M-Pesa wakati wote hadi pale ambapo kiwango chote cha Songesha ulichopewa kimerejeshwa kikamilifu.

 • 8.2.1 Kwanza utalipa ada zote zinazohitajika.
 • 8.2.2 Pili utalipa Rejesho lote la Songesha.
 • 8.3 Baada ya kupita kwa muda wa Songesha, sisi tuna haki ya kuhuisha ama kuongeza Muda wa kulipa Songesha. Kwa mujibu/kadri ya mapitio yetu ya mara kwa mara ya kikomo chako kama ilivyoelezwa katika Kifungu cha 5, unakubali kuwa kukokotoa upya ama kuendeleza Upataji wa Sogesha ni sehemu ya vigezo na Masharti yaliyomo humu. Utapata taarifa pindi kila mara muda wa kulipa songesha utakapohishwa au kuongezwa.

9. MATOKEO YA UKIUKWAJI

9.1 Wakati wowote baada ya Tukio la ukiukwaji limetokea, tuna haki ya:

 • 9.1.1 Kusitisha Huduma kwa taarifa au bila taarifa au kwa mujibu wa kifungu cha 13 chini;
 • 9.1.2 Kuamuliwa kulipa mara moja Kiwango chote Cha Songesha (ikiwa ni pamoja na ada na gharama zote) na kiasi kingine chochote kilichopo chini ya Masharti na Matumizi haya, ambapo unawajibika kulipa na;
 • 9.1.3 Unaturuhusu sisi kuwasilisha habari yako (yaani Tukio la Ukiukwaji) wa Mikopo kwa Taasisi za Kumbukizi za Mikopo kulingana na matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Kifedha au kwa taasisi zingine za kiudhibiti.
 • 9.1.4 Kuchukua hatua za kutosha ikiwa ni pamoja na kuhusisha taasisi za ukusanyaji mikopo ili kuwezesha urejeshaji wa kiwango/madeni yaliyokiukwa.

10. ADA, MAKATO NA GHARAMA

10.1 Unawajibika kwa malipo ya ada zote zinazotokana na matumizi ya Huduma.

10.2 Ada zote zinakatwa mwanzoni mwa maombi na zinaweza kubadilika wakati wowote pindi tutakavyoona inafaa.

10.3 Ada zinazolipwa chini ya Songesha zitakatwa kwenye Akaunti yako ya M-PESA. Kwa hiyo unakubali kwamba tuna haki ya kukata kutoka kwenye Akaunti yako ya M-PESA (bila kukutaharifu) ada yoyote ya miamala inayolipwa inatokana na huduma hii;

10.4 Isipokuwa kama inavyofahamika vinginevyo, ada zinajumuisha kodi zote zinazohusika pamoja na kodi ya Ongezeko la Thamani kwa kiwango cha juu. Wewe unakubali kulipa ada zote za miamala.

10.5 Unakubali kulipa gharama zote zilizotumika na sisi katika kupata au kujaribu kupata malipo /rejesho unayodaiwa chini ya Akaunti yako ya M-PESA.

10.6 Unapaswa kukamilishaombi lako la Upataji wa Songesha kwa ufanisi kila mara unapoomba huduma ya Songesha.

10.7 Ada zote zinazohusiana na matumizi yako ya Huduma ya M-PESA zitakuwa chini ya mujibu wa Masharti ya Matumizi ya huduma ya M-PESA.

11. KODI

11.1 Marejesho yote yatajumuisha ushuru wowote unaolipwa kama inavyotakiwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

11.2 Bila pingamizi lolote lile, unatupa ruhusa ya kufanya marekebisho ya Ada pale ambapo kutatokea mabadiliko yoyote ya sharia za kodi

12. MATUMIZI YA TAARIFA BINAFSI

12.1 Kwa hivyo unakubali kwa dhati na umetuidhinisha sisi kupokea,kutoa taarifa zako au kutumia taarifa zako binafsi au habari au data inayohusiana na Akaunti yako ya M-PESA na huduma zingine za Vodacom kuhusu Upataji Songesha uliyopewa chini ya huduma hii na maelezo yoyote juu ya matumizi yako ya huduma kwa;

 • 12.1.1 Kwenda na kutoka kwa watoa huduma zetu, wafanyabiashara, mawakala au kampuni nyingine yoyote ambayo inaweza kuwa au kuwa washirika wetu au kampuni tanzu au kampuni mama kwa madhumuni ya kibiashara yanayohusiana na Huduma;
 • 12.1.2 Kwa Taasisi Kumbukizi za Mikopo;
 • 12.1.3 Kwa taasisi huru za ukusanyaji wa mikopo;
 • 12.1.4 Kwa wanasheria wetu, wakaguzi au washauri wengine wa kitaalam au kwa mahakama yoyote au mahakama ya usuluhishi kuhusiana na kesi yoyote ya kisheria au ukaguzi;
 • 12.1.5 Kwa madhumuni ya kibiashara yenye kuhusiana na matumizi yako ya Huduma, kama uuzaji na shughuli zinazohusiana na utafiti; na
 • 12.1.6 Katika mazoea ya kibiashara pamoja na bila kufungamana na udhibiti wa ubora, mafunzo na kuhakikisha uendeshaji mzuri wa mifumo.

12.2 Unatuidhinisha kutoa habari yoyote inayohusiana na Akaunti yako ya M-PESA kwa Mamlaka ya sheria yoyote ndani e ya nchi au ya kimataifa au mashirika ya serikali ili kusaidia katika kuzuia, kugundua, uchunguzi au uendeshaji mashtaka ya jinai au udanganyifu au kwa taasisi nyingine yoyote au washiriki kama inavyotakiwa na sheria za nchi yoyote na kadiri tunavyoona ni muhimu.

12.3 Unatuidhinisha kutoa, kujibu, kushauri, kubadilishana na kuwasilisha maelezo au habari zinazohusiana na Akaunti yako ya M-PESA na / au Upataji Songesha kwa watu wengine/washiriki wanaohusika katika usimamizi wa Akaunti yako ya M-PESA na Upataji Songesha, usasishaji wa hifadhidata( database), au utoaji ya msaada wa watumiaji.

13. MABADILIKO, USIMAMISHAJI NA USITISHAJI

13.1 Tunaweza wakati wowote, kusitisha au kutofautisha uhusiano wetu wa kibiashara na wewe au kuzuia usajili wako na au upataji Huduma:

 • 13.1.1 Iwapo unatumia Huduma hii kwa madhumuni yasiyoruhusiwa au tunagundua matumizi mabaya, uvunjaji wa yaliyomo, udanganyifu au kujaribu kudanganya matumizi yako ya Huduma;
 • 13.1.2
 • 13.1.3 Ikiwa Akaunti yako ya M-PESA au makubaliano na Vodacom au M-Pesa Limited yamesimamishwa kwa sababu yoyote;
 • 13.1.4 Ikiwa tunahitajika au kuombwa kufuata tii/kuzingatia au agizo la au pendekezo kutoka kwa serikali, mahakama, mdhibiti au mamlaka nyingine inayofaa kwa tahathari hiyo au umuhimu huo;
 • 13.1.5 Ikiwa tunashuku au tunaamini kuwa unakiuka Masharti ya Matumizi (pamoja na kutokulipa malipo yoyote unayodaiwa);
 • 13.1.6 Ambapo akaunti yako ya M-PESA inakuwa haifanyi kazi au mfu au inachukuliwa kuwa imesitishwa.
 • 13.1.7 Ikiwa tutaamua kusimamisha au kusitisha utoaji wa Huduma kwa sababu za kibiashara au kwa sababu nyingine yoyote kama itakavyoamuliwa.
 • 13.2 Unaweza kufuta (i.e. kutengua) usajili wa Huduma wakati wowote kupitia vifaa vyako; Ila hutakiwi kutengua usajili ikiwa una Songesha au unadaiwa rejesho au ada zozote zile.

  13.3 Usitishaji huduma hakutaathiri haki na majukumu yoyote ya kisheria kwa pande yoyote ile na, haswa, haitaathiri majukumu yako ya kukidhi ulipaji deni lolote iliyopatikana kabla ya kusitisha huduma.

  13.4 Tunaweza kusitisha uhusiano wetu na wewe na kusimamisha upatikanaji wa Huduma ikiwa utashindwa kulipa Songesha pamoja na Ada yoyote unayodaiwa ndani ya Muda wa kulipa Songesha ambao ni siku thelathini (30).

  13.5 Ikiwa unadaiwa salio la Songesha kwa zaidi ya siku thelathini (30), haki yako ya kutumia Huduma ya Songesha na M-Pesa itasitishwa mara moja mpaka utakapo fanya malipo ya Songesh,na mpaka pale marejeo ya kiwango yatakapofanyika

  14. MABADILIKO YA VIGEZO NA MASHARTI

  14.1 Tunaweza kuongeza au kubadilisha Masharti ya Matumizi wakati wowote kwa hiari yetu Tunaweza kuongeza ada mpya na makato au kubadilisha ada zilizopo wakati wowote;iwapo kutatokeamatokeo ya moja kwa moja ya sheria mpya, chombo cha kisheria, kanuni au leseni za Serikali, uwekaji au mabadiliko ya kodi za serikali au mapitio yoyote ya kimkakati ya mipango ya biashara ya M-Pesa Limited, mabadiliko ndani ya tasnia ya mawasiliano, mapendekezo kutoka kwa vyombo vya kisheria au kwa Sababu yoyote ile kama tunavyoweza kuamua kwa hiari yetu.

  14.2 Tutajaribu kukujulisha mapema ikiwa tunaongeza au kubadilisha Masharti ya Matumizi. Kiwango na aina ya taarifa ambayo tutakupa itafuata njia muhimu inayotumika na inayopatikana wakati huo. (Kwa mfano, tunaweza kukujulisha kwa barua, barua ya elektroniki, simu (pamoja na ujumbe uliorekodiwa au ujumbe wa simu) au kwa tangazo katika gazeti la kila siku au gazeti la kila wiki au kwenye tovuti yetu au njia nyingine yoyote). Mabadiliko hayo yatatokea kabla au baada ya kukuambia juu ya hiloo, unashauriwa pia kutembelea tovuti yetu mara kwa mara ili kuona mabadiliko iwapo hujapata taarifa hizo kwa sababu yoyote ile iliyo nje ya uwezo wetu.

  15. KWA UJUMLA

  15.1 Vigezo na Masharti haya (kama yanavyoweza kurekebishwa mara kwa mara) ni makubaliano ya kisheria yanayokubana wewe binafsi pamoja wawakilishi wako wa kibinafsi na warithi wako.

  15.2 Hatutawajibika kwa kuchelewesha au kushindwa kutekeleza majukumu yetu yanayohusiana na Utumiaji wa Huduma ya Songesha na M-Pesa iwapo ucheleweshaji huo au kushindwa huko kumesabishwa na sababu au hali yoyote iliyo nje ya uwezo wetu au kwa sababu ya Matatizo Yasiyozuilika.

  15.3 Hauwezi kubadilisja kwa namna yoyote Masharti ya Matumizi na hauwezi kuhamisha majukumu haya kwa mtu mwingine yeyote au biashara.

  15.4 Mkataba huu utasimamiwa na kutafasiriwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania.

  15.5 Mawasiliano yote chini ya Mkataba huu yatakuwa kwa Kiingereza au Kiswahili.

  15.6 Masharti ya Matumizi haya hayasitishi Masharti yoyote ya Matumizi na yatasomwa kwa kushirikiana na Kanuni na Masharti ya Wateja wa Vodacom wa Vodacom na M-Pesa.

  16. MAWASILIANO NA MALALAMIKO

  16.1 Ikiwa haujaridhika na huduma yoyote inayotolewa, tafadhali wasiliana na Kituo cha Huduma kwaa Mteja wa Vodacom kwa kupiga simu namba 100. Tutaoa ushirikiano wa kutatua lalamiko lako na kukuelezea utaratibu wa malalamiko kwa undani zaidi. Tutajaribu kutatua malalamiko yako haraka iwezekanavyo. Mara nyingi hata hivyo, malalamiko yatahitajika kuchunguzwa. Ikiwa hali ndio hii, tutakujibu ndani ya siku 5 za kazi na tutakiri kupokea malalamiko yako na tunaweza kukujibu itachukua muda gani ili malalamiko yako kutatuliwa. Ikiwa malalamiko yako hayawezi kutatuliwa utashauriwa ipasavyo.

  Songesha Terms and Conditions

  Unapotumia huduma ya Songesha utalipa gharama ya Ada ya Maombi: kulingana na kiwango unachopewa. Ada hii itatozwa mara moja tu pale utakapotumia huduma ya Songesha.

  Viwango Ada ya Maombi
  1 – 1000 5.7%
  1001 – 2000 6.0%
  2001 – 3000 6.0%
  3001 – 4000 6.2%
  4001 – 5000 6.9%
  5001 – 6000 6.9%
  6001 – 7000 6.9%
  7001 – 8000 6.9%
  8001 – 9000 6.9%
  9001 – 10000 6.9%
  10001 – 20000 6.0%
  20001 – 30000 5.1%
  30001 – 40000 4.5%
  40001 – 50000 4.1%
  50001 – 80000 4.0%
  80001 – 100000 4.2%

  Ada ya siku: ambayo hulingana na kiwango ulichopewa na siku ya marejesho.

  Viwango Ada ya kila siku
  Siku 1 Siku 2 hadi 5 Siku 6 hadi 10 Siku 11 hadi 15 Siku 16 na Zaidi
  1 – 1000 4% 7% 10% 14% 16%
  1001 – 2000 4% 7% 10% 14% 16%
  2001 – 3000 4% 7% 10% 14% 16%
  3001 – 4000 4% 7% 10% 14% 16%
  4001 – 5000 3% 7% 10% 14% 16%
  5001 – 6000 3% 7% 10% 14% 16%
  6001 – 7000 3% 7% 10% 14% 16%
  7001 – 8000 3% 7% 10% 14% 16%
  8001 – 9000 3% 7% 10% 14% 16%
  9001 – 10000 3% 7% 10% 14% 16%
  10001 – 20000 4% 7% 9% 10% 15%
  20001 – 30000 5% 7% 9% 10% 15%
  30001 – 40000 5% 7% 9% 10% 15%
  40001 – 50000 6% 7% 9% 10% 15%
  50001 – 80000 6% 7% 9% 10% 15%
  80001 – 100000 6% 7% 9% 10% 13%
  Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa