MALIPO YA KUJIRUDIA (M-PESA STANDING ORDER)

MALIPO YA KUJIRUDIA (M-PESA STANDING ORDER)

Vodacom M-Pesa kwa mara ya Kwanza tumekuletea Huduma ya kipekee ya M-Pesa Standing Order (Malipo ya kujirudia). Hii ni huduma inayokupa uwezo wa kuifanya M-Pesa ikamilishe miamala au malipo kwa niaba yako. M-Pesa standing order inakuwezesha kuweka malipo ya kujirudia kwenye Miamala Kama Kutuma pesa, Kulipa bili kama LUKU, Malipo ya ving’amuzi kama DSTV, Azam TV, Startimes n.k!
Unaweza kuweka malipo yafanyike Mara moja, Kila Wiki au Kila Mwezi. Malipo haya unaweza kuweka zaidi ya mara moja. Pia unaweza kuangalia orodha ya malipo ya kujirudia uliyoweka na unaweza kusitisha malipo yoyote uliyoyaweka yasifanyike.
Hakuna makato yoyote kutumia huduma hii. Piga *150*00# > chagua Tuma Pesa au Lipa kwa M-Pesa kuweka malipo ya kujirudia.


Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa