VODACOM TANZANIA LIMITED SUBSCRIBER TERMS AND CONDITIONS

KANUNI NA MASHARTI YA MTUMIAJI WA VODACOM TANZANIA PLC

1. Kanuni na Masharti & Matumzi
 • 1.1 Kanuni na masharti haya yanatolewa na Vodacom Tanzania PLC (ambayo humu yataitwa “Vodacom” au “sisi” au “wenyewe” au “yetu”) kwa Mtumiaji wa Vodacom au Mteja (ambaye humu ataitwa “wewe” au “yako” au “mtumiaji” “mwenyewe”).
 • 1.2 Kanuni na masharti haya yatatumika kwa Watumiaji wote wa Vodacom na au Wateja kwa Huduma zinazotolewa na Vodacom ambazo zinajumuisha japo si hizo tu, Huduma za sauti, data, intaneti, huduma za ongezeko la thamani na huduma za fedha kwa simu ya mkononi (M-PESA).

2. Fafanuzi
 • 2.1 “Akaunti” maana yake ni kumbukumbu za malipo yako yaliyofanywa kwa huduma za Vodacom na Tozo zilizopo, pamoja na maelezo yako binafsi.
 • 2.2 “Zuio” maana yake ni zuio lililowekwa na sisi katika baadhi ya huduma zetu au huduma zetu zote zinazotumika isipokuwa kwa huduma ya miito ya dharura. Inaweza kujumuisha kuzuia uunganishaji wa Huduma ambapo ungeweza kuelekezwa moja kwa moja kuwasiliana na Kituo cha Huduma kwa Mteja wakati unajaribu kupiga simu kwa kutumia simu yako.
 • 2.3 “Tozo” maana yake ni tozo zote kwa ajili ya Huduma, kama zinavyochapishwa na Vodacom katika vipindi mbalimbali katika tovuti ya Vodacom ikiwa ni pamoja na kodi zote zilizopo.
 • 2.4 “Uunganishaji” maana yake ni mchakato wa kukupatia Huduma.
 • 2.5 “Maudhui” maana yake ni taarifa, mawasiliano, picha na sauti, programu za kompyuta au maunzi mengine yoyote yaliyo ndani au yaliyopo kwa Huduma au kutoka katika tovutu ya kampuni, blogu au mitandao ya kijamii.
 • 2.6 “Mawasiliano ya Mteja” maana yake ni taarifa kuhusu Huduma zetu zinazotolewa kwako na Vodacom kwenye simu yako kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi au miito au zinazotolewa kielektroni katika tovuti ya Vodacom na mitandao ya kijamii au zinazosambazwa kwa njia ya mauzo ya bidhaa za Vodacom kwa njia ya mitandao ya kijamii. Mitandao ya kijamii ya Vodacom itajumuisha Instagram, Facebook na Twitter.
 • 2.7 “Masharti ya Matumizi ” maana yake ni kanuni na masharti haya kadri yanavyoweza kubadilishwa nasi katika vipindi mbalimbali kulingana na masharti haya;
 • 2.8 "Ukataji" maana yake ni kukuondoa katika Huduma;
 • 2.9 “Chombo”maana yake ni simu ya mkononi inayotumiwa nawe;
 • 2.10 “Mtandao” maana yake ni mfumo wa mwasiliano ya kielektroni unaotolewa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
 • 2.11 “Huduma za Nyongeza za Vodacom Tanzania PLC” maana yake ni Huduma za hiari (ikiwa ni pamoja na japo si hivi tu, utumiaji wa simu wa nje ya nchi, kupiga simu kimataifa, na maudhui yanayotolewa na Vodacom Tanzania PLC) ambayo yanaweza kukugharimu zaidi ama yawe yanatolewa pamoja na Mipango ya Huduma au nje ya Mipango ya Huduma;
 • 2.12 “Mwongozo wa Bei” orodha ya Tozo za sasa ambayo huwa inahuishwa katika vipindi mbalimbali na ipo kwetu inapoombwa;
 • 2.13 “Bidhaa” maana yake ni chombo, vifuasi, vocha za kukwangua na kitu kingine chochote kinachouzwa na Vodacom;
 • 2.14 “Usajili” maana yake ni kukubali kwetu maombi yako kwa Huduma na kumbukumbu zetu za data zako na data zozote za Mtumiaji kabla ya Uunganishaji. "Sajili" ina maana inayofanana;
 • 2.15 “Kupiga simu kimataifa” maana yake ni Huduma ya hiari ambayo inakuruhusu kutumia chombo chako katika mitandao ya mwendeshaji mwingine, kwa kawaida katika nchi za nje;
 • 2.16 “Huduma” maana yake ni Mtandao na Huduma nyingine, ikiwa ni pamoja na Huduma za Nyongeza za Vodacom Tanzania PLC, zinazotolewa au kusambazwa nasi kwa ajili ya matumizi yako;
 • 2.17 “Mpango wa Huduma” maana yake ni idadi ya bidhaa ambazo zitajumuisha japo si hizi tu, kifurushi cha muda wa maongezi, mkopo (nipige tafu), kifurushi cha intaneti, sauti, ujumbe mfupi wa maandishi, na/au Huduma za Nyongeza za Vodacom Tanzania PLC/Ofa na/au makato ya nyongeza na/au Huduma zozote za Ongezeko la Thamani zinazotolewa na Vodacom Tanzania PLC kwa kipindi cha kila mwezi au kipindi kingine cha malipo kilichokubaliwa ama ndani ya programu ya GSM au kuhusiana/kuunganishwa na mifumo mingine ya upande wa tatu.
 • 2.18 “GSM”maana yake ni Mfumo wa Kimataifa wa mawasiliano ya simu za mkononi (GSM)
 • 2.19 “Kadi ya simu” maana yake ni chombo cha utambulisho wa mtumiaji, kadi au chombo kingine ambacho kwa ajili ya kuepuka shaka kitajumuisha USIM ambayo ina namba yako binafsi ya simu na imewekewa programu kukuruhusu kupata Mtandao.
 • 2.20 “MSISDN” maana yake ni Namba ya Shajara ya Kituo cha Kimataifa cha Mtumiaji wa Simu ya Mkononi; maana yake ni namba ya simu ya pekee inayobainishwa katika mtandao wa simu ya mkononi, namba hii inatolewa kwako wakati wa utumiaji.
 • 2.21 “Ufungaji kutokana na kuibwa” maana yake ni ufungiaji wa muda wa Huduma. "Uondoaji/Ufungiaji" ina maana inayofanana.
 • 2.22 “Mtumiaji” maana yake ni wewe, au mtu mwingine aliyetajwa nawe au kwa niaba yako, ambaye ameidhinishwa kuingia Gharama katika Akaunti yako au kuwajibika kulipa bili zako.
 • 2.23 “Namba yako ya siri” maana yake ni namba yako ya utambulisho iwe nywila/msimbo wa siri unaouchagua kupata na kuendesha chombo chako.
 • kuendesha chombo chako. 2.24 “Sababu zilizo nje uwezo” maana yake na itajumuisha japo si hayo tu, moto, milipuko, kukatika kwa umeme, tetemeko la ardhi, mafuriko, migomo ya wafanyakazi, vizuizi, vitendo vya kiraia au mamlaka ya kijeshi, vita, ugaidi, matendo ya Mungu, matendo ya maadui wa umma na matendo ya usimamizi au wakala wa serikali.

3. Kanusho
 • 3.1 Wakati kila jitihada imefanywa na Vodacom, kampuni zake tanzu, wafanyakazi, wasambazaji, mawakala na au wauzaji kuhakikisha Huduma zinatolewa inavyostahili, Vodacom, kampuni zake tanzu, wafanyakazi, wasambazaji, mawakala na au wauzaji hawahakikishi kuwepo kwa kwa Huduma wakati wote au Huduma hiyo haitaingiliwa au kutokuwa na makosa au sahihi au salama au kamilifu au kukidhi mahitaji yako. Utaarifiwa wakati Vodacom watakapokuwa na ratiba ya kutokuwa na huduma au matengenezo yaliyopangwa isipokuwa kwa matukio ya dharura ambapo mfumo haupo kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu.
 • 3.2 Bidhaa, vifuasi na huduma zote zina dhamana inayotolewa na mtengenezaji wa bidhaa au huduma inayotolewa na Vodacom. Utafuata maelekezo ya mtengenezaji na ukiona dosari yoyote ya wazi kwenye bidhaa, vifuasi au huduma usijaribu kutengeneza dosari ile. Dosari ile itolewe taarifa haraka kama madai ya dhamana ndani ya kipindi cha dhamana. Dosari hiyo itolewe taarifa haraka kama madai ya dhamana ndani ya kipindi cha dhamana cha Vodacom kwa Kituo cha huduma kilichoidhinishwa cha Vodacom. Hatutakubali kwa ujumla maombi kwa ajili ya mabadilishano, marejesho na/au fedha kurudishwa kwa ajili ya matumizi ya Huduma baada ya kuisha kwa kipindi cha dhamana.

4. Fidia
 • 4.1 Pande hizi zitafidiana na kuachana bila ya madhara dhidi ya upotevu, matumizi, gharama au uharibuifu wowote utakaotokana na madai yoyote dhidi ya upande mmoja kwa mtu yeyote wa upande wa tatu ambao utatokana na uvunjaji wa Mkataba huu na/au kitendo chochote cha uzembe au uondoaji wa upande mwingine.
 • 4.2 Pande hizi katika namna yoyote hazitawajibika kwa kila mmoja kwa uharibifu wowote usio wa moja kwa moja, athari au uharibifu maalum wa aina yoyote na utakaotokea kwa namna yoyote, kutokana na uvunjaji wa Mkaba huu utakaofanywa na upande wowote.
 • 4.3 Kila upande utawajibika kwa upande mwingine kwa uharibifu wowote utakaotokea moja kwa moja au utakaohusiana na utendaji au kushindwa kwake kufanya chini ya Mkataba huu.
 • 4.4 Huduma za upigaji simu nje ya Tanzania zinategemea mifumo ya mawasiliano ya simu ya mitandao ya nje ya nchi, jambo ambalo hatuna udhibiti nalo. Kwa hiyo hatuwezi kutoa hakikisho lolote kuhusu huduma za simu za nje ya nchi.
 • 4.5 Iwapo unatumia Huduma kutoka katika nchi iliyo nje ya Tanzania matumizi yako ya Huduma yanaweza kufuata sheria na kanuni nyingine ambazo zinatumiwa katika nchi hiyo nyingine. Hatuwajibiki kwa kushindwa kwako kufuata sheria na kanuni hizo.

5. Matumizi ya Huduma
 • 5.1 Unaweza kutumia Huduma kwa sababu halali tu na unahakikisha kuwa:
 • 5.1.1 hutatumia huduma kupokea au kuhamisha maudhui ambayo yanavunja sheria au kanuni yoyote, huduma chafu, inayotisha, ubaguzi wa kimbari, kuogopesha, makosa, kashfa, uvunjaji wa kujiamini, uvunjaji wa haki yoyote ya milki ya ubunifu, au vinginevyo uchokozi au kinyume cha sheria;
 • 5.1.2 hutatumia Huduma kuendesha au kuwezesha kitendo chochote kinyume cha sheria au ufidadi, rushwa, utakatishaji wa fedha au kitendo kingine chochote kinyume che sheria;
 • 5.2 Utakuwa na haki, kwa hiari yako, kukataa kanuni na masharti haya ndani ya kipindi cha siku kumi baada ya kujisajili kwa Huduma zinazotolewa na Vodacom.
 • 5.3 Hatutahusika au kuwajibika kwa upotevu, kuchelewa, kupokea au kutosomeka kwa chochote kilichopakuliwa, kuhamishwa, au mawasiliano mengine. Maudhui, ambayo yanapatikana yamepatikana kutokana na vyanzo vingi, yanasambazwa kwako katika msingi wa "kama ilivyo" au kutegemea na uwezo wa chombo na hatukuhakikishii kuwa Maudhui yako na ubora unaoridhisha, yanafaa kwa madhumuni maalum, kufaa, kuaminika, usahihi, ukamilifu, usalama au isiyo na makosa au virusi.
 • 5.4 Kupata huduma za upande wa tatu na intaneti: Hatuna uwezo wa kudhibitithamani au ubora wa bidhaa, huduma au maudhui yanayotolewa na pande nyingine. Matokeo yake hatutawajibika au kustahili kwa namna yoyote na hatutaidhinisha, moja wapo ya bidhaa, huduma au maudhui.
 • 5.5 Huduma inaweza kutumiwa nawe kutumia tovuti na mitandao duniani kote. Hatuwajibiki kwa Maudhui au huduma kuhusiana na suala hili na unakubali kufuata maelekezo yanayotolewa na tovuti na mitandao hiyo inayohusiana na matumizi yako ya huduma hizo.
 • 5.6 Iwapo unatumia chombo chako kutumia intaneti au huduma za upande wa tatu huduma hizo zinaweza zisiwe za mazingira salama au maunzi au virusi vinaweza kupakuliwa katika chombo chako bila ya kujua au kwa kujua jambo linaloweza kukusababisha kupata vitu visivyoidhinishwa, au kuharibu chombo chako na taarifa zilizohifadhiwa ndani yake. Hatuwajibiki au kustahili katika namna yoyote kwa upataji huo wa vitu visivyoidhinishwa, uharibifu au kupotea kwa taarifa katika chombo chako.
 • 5.7 Watu chini ya miaka 18 hawaruhusiwi kutumia huduma za Vodacom.
 • 5.8 Kwa kukubali kanuni na masharti haya unakubali kwamba Vodacom itakuwa inakutumia ujumbe mfupi wa maandishi unaohusiana na taarifa za mteja na matangazo ya bidhaa na huduma zake katika vipindi mbalimbali. Iwapo usingependa kupokea ujumbe huu mfupi wa maandishi unatakiwa kuwasiliana na kituo chetu cha huduma au kwenda katika duka lolote la Vodacom haraka kwa msaada ili kuondolewa katika huduma hizo.

6. Taarifa za siri
 • Vodacom na kampuni zake tanzu zinajitolea kuheshimu usiri wa taarifa zako binafsi. Kudhihirisha kujitolea kwetu, Vodacom imeboresha Sera ya Faragha na Vidakuzi ili kuwasilisha kusudi lake la kutoa michakato inayofaa kwa ajili ya ushughulikiaji mzuri wa taarifa hizo za siri na kufuata sheria zilizopo ambazo zinaongoza uthibitishaji, utunzaji na uonyeshaji wa taarifa binafsi. Kwa maelezo ya ziada ya Sera yetu ya Faragha na Vidakuzi pamoja na ushuhulikiaji na matumizi ya taarifa zako binafsi tafadhali tembelea kituo chetu cha huduma kwa wateja au tovuti www.vodacom.co.tz au kwa aplikesheni ya Vodacom App au kwa barua pepe kwenda kwa customercare@vodacom.co.tz.

7. Haki za milki ya ubunifu
 • 7.1 Unakubali kuwa tunamiliki haki za milki ya ubunifu katika Huduma na kuwa matumizi yasiyoidhinishwa yanakatazwa kabisa.

  • 8. Nywila
   • 8.1 Kwa Huduma inayohitaji nywila kama vile M-PESA unatakiwa kuiweka kwa usalama nywila yako na hakikisha kuwa hakuna mtu mwingine atakayetumia Huduma kwa kutumia nywila yako, na unakubali zaidi kuwa unawajibika kuhakikisha kuwa hakuna utumiaji wa Huduma usioidhinishwa utakaofanyika kwa kutumia nywila yako, na kuwa utawajibika kwa shuhghuli
   • 8.2 Matumizi ya Akaunti; Usiruhusu kadi yako ya simu itumiwe na mtu yeyote isipokuwa wewe na utawajibika kwa kitendo chochote kitakachofanywa kupitia kadi yako ya simu na upande huo wa tatu.

   9. Usitishaji na Mabadiliko
   • 9.1 Tuna haki kwa taarifa ya awali na sababu kubadili, kuzuia na/au kusitisha Huduma kwako, au kwa umma kwa ujumla, au kupitia upya kanuni na masharti haya , na/au bei ambazo Huduma zinatolewa, wakati wowote. Mabadiliko hayo yatatakiwa kukubaliwa nawe iwapo utaendelea kutumia Huduma. Kwa hiyo wajibu uko kwako kupitia kanuni na msharti haya mara kwa mara.
   • 9.2 Tuna haki ya kutafuta suluhisho lolote lililopo katika sheria na haki kwa ukiukwaji wa Kanuni na Masharti haya, ikiwa ni pamoja na japo si haya tu kufunga utumiaji wa anwani mahususi ya intaneti na tovuti, makala na mitandao yoyote ya Vodacom.

   10. Tozo
   • 10.1 Tozo kwa ajili ya huduma zinazotolewa katika kanuni na masharti haya ni kulingana na tozo za rejareja zilizotolewa katika tovuti ya Vodacom. Tozo zinaweza kubadilika katika vipindi mbalimbali kwa taarifa kwako kupitia tovuti yetu, au magazeti au ujumbe mfupi wa maandishi au njia nyingine za mawasiliano kwa umma.
   • 10.2 Tozo na ushuru wote katika Huduma ni kulingana na kodi husika.
   • 10.3 Ubia wa upigaji wa simu nje ya nchi; pale ambapo Vodacom inatoa huduma za upigaji simu nje ya nchi na chombo cha kigeni, tozo zitakuwa katika kupanda na kushuka kwa fedha za kigeni au ushuru wa kimataifa.upigaji wa simu nje ya nchi unaweza kuwa ghali kwa kiasi fulani ukilinganisha na huduma za ndani ya nchi hivyo kuendelea kutumia huduma za nje ya nchi maana yake ni kuwa umekubaliana na viwango vya ushuru vya kupiga simu nje nchi.
   • 10.4 Tunaweza kuondoa, kuzuia au kusitisha utoaji wa huduma au bidhaa yoyote iliyoonyeshwa au kuorodhesha katika chombo chako au vyote viwili kwa ujumla au kwa sehemu na/au kufunga Akaunti yako kwa kukuarifu au bila ya kukuarifu na bila ya dhima yoyote ingawa, pale inapowezekana, tutajaribu kukuarifu kuwa hatua hiyo imechukuliwa au inaweza kuchukuliwa chini ya mazingira yafuatayo:-
   • 10.4.1 Iwapo tunafahamu au kushuku au tuna sababu ya kuamini kuwa chombo chako au MSIN/namba ya siri inatumiwa katika namna isiyoidhinishwa, kinyume cha sheria, isivyotakiwa au kwa udanganyifu au kwa shughuli za uhalifu au imekuwa ikitumiwa hivyo siku za nyuma;
   • 10.4.2 Iwapo utakiuka na moja ya masharti haya yanayohusiana na Huduma za GSM ikiwa ni pamoja na Masharti haya ya Matumizi;
   • 10.4.3 Iwapo utatuarifu kuwa chombo chako au kadi yako ya simu imepotea au kuibwa au sababu nyingine yoyote ambayo inaweza kuathiri mitandao yetu ikiwa ni pamoja na sababu zile kutoka katika mamlaka za serikali au vyombo vingine vya Kisheria.

   11. Kwa ujumla
   • 11.1 Kanuni na msharti haya yatasimamiwa na kutafsriwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
   • 11.2 Malalamiko au mgogoro wowote utakaotokea kuhusiana na Huduma au Kanuni na Masharti haya vitapelekwa Vodacom ndani ya siku thelathini tangu kutokea kwa malalamiko au mgogoro huo, kushindwa kupeleka malalamiko au mgororo ndani ya siku hizi kutaipa Vodacom hiari ya kuyakataa malalamiko au mgogoro huo.
   • 11.3 Katika tukio la kutoridhishwa na matokeo kwa mujibu wa kifungu cha 11.2 hapo juu, upande ambao haujaridhishwa utalipeleka suala hilo katika Kamati ya Malalamiko chini ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ndani ya siku thelathini.
   • 11.4 Kanuni na masharti haya ni mengi, hivyo iwapo kifungu chochote kitaonekana kuwa kinyume au kutotekelezeka na mahakama yoyote au mamlaka ya kisheria, kifungu hicho kitatapaswa kufutwa bila ya kuathiri vifungu vilivyobaki vya kanuni na masharti haya.
   • 11.5 Kushindwa kwetu kutekeleza haki au sharti lolote mahususi la kanuni na masharti haya hakutajumuisha msamaha wa haki au sharti hili, isipokuwa kama imekubaliwa na kutamkwa nasi kwa maandishi.
   • 11.6 Kanuni na masharti haya, yanafanyiwa marekebisho nasi katika vipindi mbalimbali ikijumuisha na makubaliano ya pekee kati yako na sisi. Utaarifiwa kuhusu mabadiliko yoyote ya huduma kabla ya kutekelezwa kwa njia ya tovuti ya Vodacom, ujumbe mfupi wa maandishi au njia nyingine zozote za mawasiliano kwa umma. Pale ambapo makubaliano maalum yametiwa saini kati yako na sisi ambayo yatajumuisha kanuni na masharti kama haya, kifungu cha masharti maalum kitazingatiwa katika tukio la mgogoro au kutokubaliana.

KANUNI NA MASHARTI MTUMIAJI WA M-PESA

1. ASILI YA KANUNI NA MASHARTI PAMOJA NA MATUMIZI.
 • 1.1. Kanuni na Masharti haya yametolewa na M-PESA Limited (humu utambuliwa kama "M-PESA Limited" au "sisi" au "sisi" "sisi wenyewe" au "yetu") kwa Wateja wa M-PESA ("Wateja") (humu imehainishwa kama "wewe" au "yako" au "mtumiaji" "mwenyewe").
 • 1.2. Kanuni na Masharti haya yatatumika na kuwafunga Wateja wote wa M-PESA ambao hutumia au wanaweza kutumia Huduma za M-PESA (kama inavyofafanuliwa hapa) ("Masharti ya Matumizi ') na itasomwa pamoja na sera ya faragha na Vidakuzi
 • 1.3. Wakati unapotumia au kujisaji kama Mteja wa M-PESA kwa kujaza Fomu ya Usajili ya M-PESA (kama ilivyoambatishwa humu) unakubali kufuata Masharti haya ya Matumizi. Kwa hiyo unatakiwa kusoma na kuelewa kiukamilifu Masharti haya ya Matumizi na iwapo hukubaliani nayo, usiendelee kujisajili na/au kutumia Huduma za M-PESA.

2. FAFANUZI:
 • Fafanuzi zifuatazo zinahusiana na Masharti haya ya Matumizi:
 • 2.1. Katika kanuni na masharti haya maneno na fafanuzi zifuatayo (zinahusiana na mazingira ya matumizi yanavyohitaji au kwa kuoanisha vinginevyo) hubeba maana zifuatazo:
 • 2.1.1. “Akaunti” maana yake ni Akaunti yako ya M-PESA, ambayo ni kumbukumbu zinazotunzwa na M-PESA Limited za kiasi cha fedha zako za kielektroni katika vipindi mbalimbali zinazowakilishwa na kiasi sawa cha fedha taslimu kilichohifadhiwa na Mdhamini kwa niaba yako;
 • 2.1.2. “Akaunti ya Makusanyo au Akaunti ya Malipo” maana yake ni akaunti ya M-PESA alionayo upande wa tatu kwa madhumuni ya kukusanya au kulipia malipo ya kielektroni kutoka au kwenda kwa wateja wake;
 • 2.1.3. “Wakala au Mawakala wa M-PESA” maana yake ni mtu (watu) aliyesajiliwa na M-PESA Limited kutoa Huduma za M-PESA, maelezo yake yanaweza kupatikana kutoka katika Ofisi Kuu ya M-PESA Limited
 • 2.1.4. “Tozo” maana yake ni gharama na ada nyingine zinazolipwa kwa ajili ya utumiaji wa Huduma za M-PESA kama zinavyochapishwa na M-PESA Limited katika vipindi mbalimbali;
 • 2.1.5. “Masharti ya Matumizi” maana yake ni kanuni na masharti haya kama yanavyoweza kubadilishwa nasi katika vipindi mbalimbali;
 • 2.1.6. “Salio la Fedha” maana yake ni kiasi cha fedha za kielektroni katika vipindi mbalimbali kilichomo katika za Akaunti yako;
 • 2.1.7. “Muamala wa Kutoa” maana yake ni muamala wowote ambao matokeo yake ni Akaunti yako kutolewa fedha kwa njia ya kielektroni kama inavyoweza kuthibitishwa na M-PESA;
 • 2.1.8. “Mteja au Mteja wa M-PESA” maana yake ni wewe na mtu mwingine yeyote ambaye jina lake limesajiliwa katika kwa ajili ya Huduma za M-PESA;
 • 2.1.9. “Kituo cha Huduma kwa Wateja” maana yake ni Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Vodacom kilichoko katika Barabara ya Sam Nujoma, Mlimani City, Mlimani City Office Park, Dar es Salaam au Kituo chochote cha Huduma kwa Wateja cha Mkoa;
 • 2.1.10. “Makato” maana yake ni kutolewa kwa fedha kutoka kwenye Akaunti yako;
 • 2.1.11. “Muamala wa Makato” maana yake ni muamala wowote ambao matokeo yake ni Makato ya fedha za kielektroni kutoka katika Akaunti yako kama itakavyothibitishwa na mfumo wa M-PESA;
 • 2.1.12. “Mlipwaji Aliyekusudiwa” maana yake ni mtu yeyote (ikiwa ni pamoja na wewe, mteja mwingine, Wakala au Muuzaji wa Rejareja) ambaye amekusudiwa na wewe kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi, kuwa mpokeaji wa fedha za kielektroni kutoka katika Akaunti yako;
 • 2.1.13. “Fedha za Kielektroni” maana yake ni fedha za kielektroni zinazotolewa na M-PESA Limited na kuwakilisha stahili ya kiasi sawa cha fedha taslimu kilicho kwa Mdhamini kulingana na ununuzi wa thamani hiyo ya kielektroni;
 • 2.1.14. “Bidhaa na Huduma” maana yake ni bidhaa na huduma kama ambavyo zinaweza kununuliwa kutoka kwa Muuzaji wa Rejareja Aliyeidhinishwa kwa kutumia Mfumo wa M-PESA;
 • 2.1.15. “Namba ya Utambulisho”maana yake ni namba inayohusiana na jinsi utambulisho ulivyotolewa;
 • 2.1.16. “Kifaa cha Simu ya Mkononi” maana yake ni simu yako ya mkononi na kadi ya simu au kifaa kingine ambacho wakati vinapotumiwa pamoja na kinaruhusu kupata Huduma ya M-PESA na, katika kila jambo, iliyothibitishwa kwa ajili ya matumizi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mamlaka inayohusika;
 • 2.1.17. “Simu ya Mkononi” maana yake ni simu yako ya mkononi;
 • 2.1.18. “Muuzaji wa Rejareja anayetumia huduma ya M-PESA” maana yake ni muuzaji wa Bidhaa na Huduma ambaye anapokea Fedha za Kielektroni kwa ajili ya malipo ya Bidhaa na Huduma;
 • 2.1.19. “Huduma za M-PESA” maana yake ni huduma inayotolewa na M-PESA Limited kwa ajili ya kutoa na kufidia Fedha za Kielektroni na kuhamisha Fedha za Kielektroni kati ya Mteja na Mteja kwa msingi wa Maelekezo ya Uhamishaji ikiwa ni pamoja na uwekaji kumbukumbu wa Miamala yote, kuidhinisha na kuthibitisha Miamala yote iliyokamilishwa, udumishaji wa Akaunti, uhuishaji wa kumbukumbu za Akaunti ya Mteja na huduma nyingine kama hizo zinazotolewa au kutambulishwa na M-PESA Limited katika vipindi mbalimbali ;
 • 2.1.20. “Mfumo wa M-PESA au M-PESA” maana yake ni huduma ya uhamishaji wa fedha unaostahili kwa simu ya mkononi ambayo inatafutiwa masoko, kusimamiwa, na kuendeshwa na M-PESA Limited pekee katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
 • 2.1.21. “Tovuti ya M-PESA” inamaanisha sehemu ya M-PESA katika anwani ya tovuti inayopatikana kwenye www.vodacom.co.tz;
 • 2.1.22. “MSISDN” maaana yake ni namba ya utambulisho wa simu ya mkononi inayotolewa kwako pamoja na kadi ya simu na namba ya utambulisho inayohusika na PUK kwa ajili ya kutumia mtandao wa Vodacom;
 • 2.1.23. “Mtandao” maana yake ni Mfumo wa Kimataifa kwa ajili ya mfumo wa mawasiliano ya simu ya mkononi (“GSM”) unaoendeshwa na Vodacom na ulioko kwenye maeneo yaliyo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama inavyoelezwa na Vodacom katika vipindi mbalimbali;
 • 2.1.24. “Mtoa Huduma wa Mtandao” maana yake ni mtoaji wa huduma za simu ya mkononi;
 • 2.1.25. “Mwendeshaji wa Kibanda” maana yake ni msaidizi anayekuhudumia katika Kibanda;
 • 2.1.26. “Kibanda” maana yake ni duka, kitengo au majengo yoyote ya rejareja yanayoendeshwa na Wakala;
 • 2.1.27. “Malipo” maana yake ni fedha zinazolipwa kwa Wakala, kwa ajili ya kununua kiasi kilekile cha Fedha za Kielektroni kinachowekwa katika Akaunti yako, fedha nyingine zozote baada ya hapo ambazo zitashikiliwa na Mdhamini kwa ajili ya dhamana yako kama ilivyoainishwa humu;
 • 2.1.28. “Namba ya Siri” maana yake ni namba yako binafsi ya utambulisho ambayo ni msimbo wa siri uliouchagua kutumia na kuendesha Akaunti yako;
 • 2.1.29. “Malipo ya awali ya muda wa Maongezi” maana yake ni salio la kupigia simu ya mkononi katika Mtandao wa Vodacom;
 • 2.1.30. “Fomu ya Usajili” maana yake ni fomu ya usajili yenye maelezo ya usajili na kukubali kwako Kanuni hizi za Matumizi katika fomu iliyoambatishwa humu ama nakala halisi au katika mfumo wa eletronik;
 • 2.1.31. “Kadi ya Simu” maana yake ni chombo cha utambulisho wa mtumiaji ambacho kinapotumika na Kifaa kinachostahili cha Simu ya Mkononi kinakuwezesha kutumia Huduma za M-PESA
 • 2.1.32. “Ujumbe Mfupi wa Maandishi” maana yake ni ujumbe mfupi wa maandishi wenye ujumbe ulioandikwa unaohamishwa kutoka katika simu moja ya mkononi kwenda kwenye simu nyingine;
 • 2.1.33. “Namba za Kuanzia” maana yake ni Namba ya Siri ya tarakimu nne unayotumiwa wakati wa usajili kwa madhumuni ya kuanza kutumia Akaunti yako;
 • 2.1.34. “Mamlaka ya Kodi” maana yake ni Mamlaka ya Mapato Tanzania;
 • 2.1.35. “Mwongozo wa Ushuru” maana yake ni katalogi iliyochapishwa kwa ajili ya Ushuru unaolipwa kwa ajili ya Huduma za MPESA, kama inavyohuishwa katika vipindi mbalimbali;
 • 2.1.36. “Kanuni na Masharti” maana yake ni Masharti haya ya Matumizi pamoja na au bila ya Fomu ya Usajili;
 • 2.1.37. “Maelekezo ya Uhamishaji” maana yake ni maelekezo yanayotolewa kupitia katika ujumbe mfupi wa maandishi kwa ajili ya uhamishaji wa fedha za kielektroni kutoka kwa mteja mmoja kwenda kwa mwingine au kutoka katika asasi moja kwenda nyingine;
 • 2.1.38. “MSISDN Iliyorejezwa” maana yake ni akaunti ya M-PESA iliyoondolewa kutoka katika mfumo wa M-PESA pindi mteja anapokuwa ama ameacha kutumia kwa muda mrefu mtandao wetu kwa kipindi fulani maalum au amehamia mtandao mwingine au kwa sababu nyingine zozote;
 • 2.1.39. “Msimbo wa USSD” maana yake ni msimbo wa kupata M-PESA (yaani *150*00#) kama inavyoainishwa katika vipindi mbalimbali na M-PESA Limited unaotumiwa na mteja kuwasiliana na mfumo wa M-PESA;
 • 2.1.40. “Mteja Asiyesajiliwa” maana yake ni mpokeaji wa Fedha za Kielektroni ambaye ama ni Mteja asiyesajiliwa wa M-PESA au Mteja kutoka kwa mtoaji mwingine wa huduma ya mtandao;
 • 2.1.41. “Vocha” maana yake ni msimbo wa siri wenye Fedha za Kielektroni zilizopokewa na Mteja Asiyesajiliwa kupitia ujumbe mfupi wa maandishi ambao iwapo utaonyeshwa kwa Wakala Mteja Asiyesajiliwa atapokea fedha taslimu;
 • 2.1.42. “Zuio la Kodi” maana yake ni kodi ya serikali inayokatwa katika akaunti ya M-PESA ya Mteja wakati wa kufanya miamala ya M-PESA;
 • 2.1.43. “Namba ya Simu ileile kwa Mitandao Tofauti (MNP)” maana yake ni kubadilisha mtoaji wa huduma ya Mtandao kunakofanywa na mteja wakati akiwa amebaki na MSIN yake ama kwa kuhama katika mtandao wetu na kuondolewa katika Mfumo wa M-PESA;
 • 2.1.44. “Mdhamini” maana yake ni M-PESA Limited ambayo inashikilia jumla ya Malipo yote na jumla ya kiasi ambacho ni sawa na uhamishaji wote wa Fedha za Kielektroni kwenye Akaunti yako ya M-PESA kutoka kwa Mteja mwingine kwa niaba yako katika Akaunti ya Mdhamini;
 • 2.1.45. “Akaunti ya Mdhamini” maana yake ni akaunti ya benki ya Mdhamini inayoshikilia jumla ya Malipo yote na jumla ya kiasi ambacho ni sawa na uhamishaji wote wa Fedha za Kielektroni kwenye Akaunti yako ya M-PESA kutoka kwa Mteja mwingine;
 • 2.1.46. “Mwongozo wa Mtumiaji” maana yake ni waraka unaoelezea Mfumo wa M-PESA na matumizi yake;
 • 2.1.47. “Sisi” au “yetu” au “nasi” maana yake ni M-PESA Limited na Mdhamini (pale inapotumika);
 • 2.1.48. “Wewe” au “yako” au “nawe” maana yake ni Mteja;
 • 2.2. Neno "Mteja" litajumuisha jinsia ya kike na kiume kwa pamoja na kampuni au taasisi zinazotambulika kisheria;
 • 2.3. Maneno yanayohusu au kuelezea maana ya umoja katika mazingira yanayokubalika inajumuhisha pamoja na maana ya wingi na kinyume chake.
 • 2.4. Muktasari/Vichwa vya Habari katika Kanuni na Masharti haya ni kwa madhumuni ya urahisi tu na hayaadhiri tafsiri ya Mkataba huu.

3. MAOMBI KWA AJILI YA AKAUNTI
 • 3.1. Mteja anaweza anaweza kujiandikisha kwa ajili ya huduma ya M-PESA ilimradi awe na kadi ya simu ya Vodacom inayofanya kazi.
 • 3.2. Huduma ya M-PESA ni kwa ajili ya akaunti moja kwa mteja, bila kujali Mteja ana idadi gani ya kadi za simu za Vodacom.
 • 3.3. Utatakiwa kumlipa mtoaji wako wa Huduma ya Mtandao wa Simu ya mkononi kwa gharama zote za mtandao zilizoingiwa kwa kutumia Huduma ya M-PESA. Pia utatakiwa kulipa Ushuru uliopo kwa ajili ya matumizi yako ya Huduma ya M-PESA na Ushuru huo unaweza kukatwa mojakwa moja kutoka katika Akaunti ya M-PESA.
 • 3.4. Unaweza kujisajili kwa ajili ya Huduma za M-PESA kwa Wakala yeyote wa M-PESA katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 • 3.5. Mara unaposajiliwa kuwa Mteja, utatakiwa kutoa taarifa zifuatazo kwa ajili ya kujumuishwa katika Fomu ya Usajili au chombo cha usajili kitakachosainiwa nawe:-
 • 3.5.1. Namba ya simu ya mkononi;
 • 3.5.2. Jina kamili;
 • 3.5.3. Utaifa;
 • 3.5.4. Namba ya utambulisho inayohusiana na fomu ya kukubaliwa utambulisho uliotolewa;
 • 3.5.5. Tarehe ya kuzaliwa;
 • 3.5.5. Tarehe ya kuzaliwa;
 • 3.5.6. Jinsia, na
 • 3.5.7. Anwani ya mahali.
 • 3.6. Taarifa zote zilizotolewa lazima ziwe kamili na sahihi katika nyanja zote.
 • 3.7. Tunaweza kukataa maombi yako kwa hiari yetu kwa ajili ya usalama au sababu nyingine yoyote halali.
 • 3.8. Wakati wa kuifanya Akaunti yako kufanya kazi baada ya usajili, kwa kuwekewa Namba za Kuanzia na kuchagua namba za siri, utastahili kuanza kutumia Huduma za M-PESA.
 • 3.9. Unaweza kukataa kufungua Akaunti kwa ajili yako iwapo tutakuwa hatujaridhishwa na uthibitisho wa utambulisho wako.
 • 3.10. Wakati wa kutoa maelezo katika Kituo cha Huduma kwa Mteja kwa njia ya simu au wakati wa kwenda duka lolote la Vodacom, uthibitisho wa kukutambua, kuwa mmiliki halali wa akaunti utajumuisha pamoja na vitu vingine, aina ya kitambulisho chako, namba ya kitambulisho, maelezo binafsi, tarehe ya kuzaliwa, salio lililopo, miamala mitano ya mwisho pamoja na maelezo mengine yoyote yanayofaa.
 • 3.11. Tutapitia upya katika vipindi tofauti na kuhakikisha kuwa nyaraka zako za usajili ni halali kulingana na mahitaji ya sasa ya usajili yanayotolewa kwa mujibu sheria. Utatakiwa kwenda katika duka lolote la Vodacom lililo karibu yako kwa ajili ya uthibitisho wa nyaraka zako za usajili baada ya kupata taarifa ya tofauti yoyote baada ya kupiga *106# kulingana na kifungu cha 3.12 hapo chini.
 • 3.12. Unaweza kuthibitisha wakati wowote hali ya usajili wako kwa kupiga *106# kutoka katika simu yako ya mkononi na ni wajibu wako kurekebisha tofauti zitakazoonekana kwa kutuarifu kulingana na kifungu cha 3.11 hapo juu.
 • 3.13. Hautakiwi kumuachia mtu mwingine au kuhamisha kwa namna yoyote ile akaunti yako ya M-PESA kwa mtu mwingine na hupaswi kuruhusu Akaunti yako ya M-PESA itumiwe na mtu mwingine. M-PESA Limited haitahusika kwa hasara yoyote utakayoipata kama matokeo ya kukiuka masharti haya.

4. HUDUMA ZA M-PESA
 • 4.1. Huduma za M-PESA zinatolewa kwako kulingana na Kanuni hizi za Matumizi:-
 • 4.1.1. Ingawa tutajaribu kuhakikisha kuwa unaweza kutumia kikamilifu Mtandao kupata Huduma za M-PESA ndani ya eneo tunalotoa huduma, hatuhakikishi kuwa Huduma za M-PESA zitakuwepo wakati wote na hatutawajibika au kustahili kwa hasara yoyote itakayotokea kama matokeo ya kutokuwepo kokote kwa Huduma za M-PESA. Huduma za M-PESA si kwamba hazina au haziathiriwi na matukio yanayojumuisha (japo si haya tu) matendo ya Mungu, mandhari ya kijiografia, hali ya hewa, matengenezo yaliyopangwa au kazi za kurekebisha katika Mtandao ambazo zinaweza kuleta matokeo tofauti katika ubora na utoaji wa Huduma za M-PESA. Utapewa taarifa wakati M-PESA Limited watakapokuwa na kipindi cha kutokuwa na huduma au matengenezo yaliyopangwa isipokuwa kwa matukio ya dharura wakati mfumo utakapokuwa haupo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu kwa njia ya tovuti ya Vodacom, ujumbe mfupi wa maandishi au njia nyingine zozote za mawasiliano ya umma.
 • 4.1.2. Katika tukio la uharibifu, upotevu au wizi wa Kadi ya Simu, unashauriwa kutufahamisha haraka kuhusu uharibifu, upotevu au wizi huo. Kisha tutazuia uharibifu, upotevu au kadi ya simu iliyoibwa ili kuzuia matumizi zaidi ya Huduma za M-PESA mpaka itakapopatikana au kubadilishwa. Utawajibika kulipa ada ya kubadilishiwa Kadi ya Simu na utawajibika kwa Tozo na Miamala yote iliyofanywa mpaka ulipotoa taarifa kwetu kuhusu uharibifu, upotevu au wizi. Taarifa kuhusu uharibifu, upotevu au wizi huo inaweza kutolewa kwa kupiga simu katika Kituo cha Huduma kwa Mteja. Utatakiwa kutufidia dhidi ya madai yoyote yaliyofanywa kutokana na Miamala iliyofanywa na simu yako ya mkononi na kadi yako ya simu kabla ya kupokewa kwa taarifa yako.
 • 4.1.3. Tafadhali tambua kwamba usiri wa mawasiliano yako kupitia Mtandao wetu umehakikishwa kwa kiwango kinachofafanuliwa katika Sheria. Unashauriwa kuwa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu na zisizosababishwa na uzembe wetu, kuna hatari ambazo mawasiliano yako yanaweza kuingiliwa isivyo sahihi au kuwafikia watu wengine zaidi ya mpokeaji aliyekusudiwa. Hatutakubali kuhusika kwa hasara, madhara au uharibifu ama wa moja kwa moja au unaoandamana nao unaotokea kwa namna ya uvunjaji huo wa usiri.
 • 4.1.4. Unakubali kuwa tunaweza kuonyesha,kutoa au kupokea taarifa binafsi au nyaraka kuhusu wewe:-
 • 4.1.4.1. Kwenda au kutoka kwa watekelezaji wa kisheria wa ndani ya nchi na wa kimataifa au mamlaka yoyote ya usimamizi au mawakala wa kiserikali kusaidia katika kuzuia, kugundua au uendeshaji wa shughuli za jinai au udanganyifu;
 • 4.1.4.2. Kuwezesha uwezo wetu wa kuendesha shughuli yoyote inayohusiana na mahitaji ya kisheria, kiserikali au udhibiti;
 • 4.1.4.3. Kwa wanasheria au wakaguzi wetu kwenye mahakama yaliyopo kuhusiana na taratibu zozote za kisheria au ukaguzi (japokuwa taratibu zozote kama hizo zinaweza kuwa zenye sura ya umma).
 • 4.1.4.4. Kwa kampuni yoyote ya mawasiliano, wakala wa ukusanyaji wa madeni, wakala wa uwekaji kumbukumbu za mikopo, mfumo wa usimamizi wa mikopo au udanganyifu, wakala wa usalama au mtoaji wa mikopo ya (iwapo ni kama Mkopo wa M-Pawa) a) taarifa yoyote inayohusiana na taarifa zako binafsi za kifedha na maelezo ya jinsi unavyofanya katika kutimiza majukumu yako b) uonyeshaji wowote unaoweza kuwepo ndani ya usajili wa Sheria ya Ulindaji wa Data c) uonyeshaji wowote unaohitajiwa kama matokeo ya agizo la mahakama yoyote ya kisheria au na mamlaka ya kisheria.
 • 4.1.5. Lazima ufuate maelekezo yoyote ambayo tunaweza kukupa katika vipindi mbalimbali kuhusu Huduma za M-PESA. Utapewa taarifa kuhusu mabadiliko yoyote ya huduma za M-PESA inapowezekana kwa njia tovuti ya M-PESA Limited, ujumbe mfupi wa maandishi au njia nyingine yoyote ya mawasiliano ya umma.
 • 4.1.6. Unakubali kuwa tunaweza kuonyesha,kutoa au kupokea taarifa za kimuamala kuhusu wewe katika muundo wa jumla kwenda na kutoka kwa watoaji wetu wa huduma (ikiwa ni pamoja na Mdhamini), madalali, mawakala, au kampuni yoyote nyingine kama inavyoweza kuwa au kwa kampuni yetu tanzu, kampuni mama au mbia, kwa madhumuni yanayofaa ya kiuchumi yanayohusiana na matumizi yako ya huduma za simu ya mkononi au Huduma za M-PESA, kama vile utafutaji wa masoko na madhumuni yanayohusiana na utafiti. Watoaji hawa wa huduma (ikiwa ni pamoja na Mdhamini), madalali, mawakala, au kampuni yoyote nyingine kama inavyoweza kuwa au kuwa kampuni yetu tanzu, kampuni mama au mbia zinafungwa na sheria za usiri zinazotolewa na sheria.
 • 4.1.7. Bila ya kujumuisha miito inayofanywa katika namba zetu za moja kwa moja za Huduma kwa Mteja (ambazo zitatolewa kwako baada ya usajili) na kwa namba zisizo na ada zilizoundwa, tozo za chini za miito zinaweza kutozwa ushuru kulingana na Ushuru uliopo.
 • 4.1.8. Miito yako, baruapepe au ujumbe mfupi wa maandishi unaweza kusimamiwa au kurekodiwa kwa ajili ya matumizi katika shughuli za biashara kama vile udhibiti ubora, mafunzo, kuhakikisha uendeshaji wa mifumo inayofaa, uzuiaji wa matumizi yasiyoidhinishwa ya mfumo wetu wa mawasiliano ya simu na ugunduaji na uzuiaji wa uhalifu.
 • 4.1.9. Huduma za M-PESA zinakupatia uchaguzi wa ama kuthibitisha au kufuta muamala wowote, unatakiwa kuhakikisha msimbo mfupi au namba ya simu ya mpokeaji kabla ya uthibitisho, kwa hiyo unawajibika kuhakiki usahihi wa namba ya simu au msimbo mfupi wa mpokeaji na thamani ya fedha; hatutawajibika kwa miamala yoyote iliyo dosari na kwa muamala wowote unaofanywa kinyume na masharti haya.
 • 4.1.10. Kwa Akaunti yoyote ambayo haitumiki kwa zaidi ya siku zitakazo kuwa zimepangwa (ikiwa kama siku 60 au 90 au 150), ada itaamuliwa na M-PESA Limited na kukatwa moja kwa moja katika Akaunti yako kwa ajili ya udumishaji wa Akaunti kila mwezi. Vilevile, kwa kiasi chochote ambacho kitabaki katika Akaunti yako bila ya kutolewa kwa zaidi ya miaka 5, kitahamishwa na kupelekwa kwenye mamlaka zinazohusika kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ada inayotozwa katika kifungu hiki itachapishwa katika Mwongozo wa Gharama za M-PESA Limited unaopatikana katika tovuti ya Vodacom.

5. KUKUBALI NA KUANZA KWA MASHARTI YA MATUMIZI
 • 5.1. Unatakiwa kukubali Masharti haya ya Matumizi kama yanavyorekebishwa katika vipindi mbalimbali ambayo huanza:-
 • 5.1.1. Wakati wa Usajili; au
 • 5.1.2. Wakati wa kuanza kutumia kwa mara ya kwanza Mfumo wa M-PESA kwa kutumia Namba za Kuanzia.

6. UONDOAJI NA UFUNGAJI WA HUDUMA/UFUNGAJI WA AKAUNTI
 • 6.1. Tunaweza kuondoa (kukataza), kuzuia au kusitisha utoaji wa Huduma za M-PESA (kwa ujumla au kwa sehemu) na/au kufunga Akaunti yako bila kuhusika na hasara yoyote itakayotokea ingawa, tutakuarifu kuwa hatua hiyo inachukuliwa au inaweza kuchukuliwa katika mazingira yafuatayo:-
 • 6.1.1. iwapo tunatambua au kushuku au kuwa na sababu ya kuamini kuwa Kifaa chako cha Simu ya Mkononi au MSIN/Namba ya Siri inayotumiwa kwa Huduma za M-PESA inatumiwa kwa namna isiyoidhinishwa, kinyume cha sheria, isivyo halali au kwa udanganyifu au kwa shughuli za uhalifu (au imekuwa ikitumika hivyo siku za nyuma
 • 6.1.2. iwapo hufuati kanuni zozote zinazohusiana na Huduma za M-PESA ikiwa ni pamoja na Masharti haya ya Matumizi;
 • 6.1.3. iwapo utatuarifu kuwa kadi ya simu yako ya mkononi imepotea au kuibwa au namba yako ya siri imepotea au kuonwa na upande mwingine wowote;
 • 6.1.4. iwapo unafanya kitu chochote (au kuruhusu kitu chochote kufanywa) kwa simu yako ya mkononi ambacho tunafikiri kinaweza kuleta madhara au kuathiri vibaya uendeshaji au usalama wa Mtandao au Huduma za M-PESA;
 • 6.1.5. kwa sababu zilizo juu ya uwezo wetu; na
 • 6.1.6. pale ambapo tunafunga Akaunti yako chini ya Kifungu cha 6.2.
 • 6.1.7. Utekelezaji wa haki hii kama ilivyotangulia kusemwa unategemea Sheria zingine zinazotumika.
 • 6.2. Ili kupata Huduma za M-PESA, kadi yako ya simu lazima iwe inafanya kazi (“iko hewani”) wakati wote. Iwapo kadi yako ya simu haifanyi kazi kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo Akaunti yako ya M-PESA itafungwa na M-PESA Limited na Fedha zozote za Kielektroni zilizomo zitalipwa kwako kwa namna iliyoelezwa katika kifungu cha 6.4. (Pia fedha zinaweza kuhamishiwa katika namba ya M-PESA itakayoonyeshwa).
 • 6.3. Pia tutaifunga Akaunti yako baada ya kupokea maombi yako ya kuifunga.
 • 6.4. Pale ambapo matumizi ya namba yako ya siri yameondolewa au kufungiwa au Akaunti yako kufungwa Salio lolote la fedha lililomo katika Akaunti yako litalipwa kwako kwa fedha taslimu baada ya wewe kufika katika Kituo chetu cha Huduma kwa Mteja. Utalipwa salio lako lolote la fedha kwa fedha taslimu baada tu ya ushahidi unaoridhisha wa utambulisho wako kutolewa.
 • 6.5. Hatutawajibika kwa madhara ya moja kwa moja, yasiyo ya moja kwa moja, yanayoambatana au maalum yanayotokana na kitendo chochote au kosa letu au upande wowote wa tatu ambao tunawajibika nao, ama kutokana na mkataba, au kisheria, iwapo tutaifunga au kuiondoa Akaunti yako kutokana na kifungu hiki cha 6.
 • 6.6. Huduma itasitishwa moja kwa moja iwapo msimbo usio sahihi wa namnba ya siri utaingizwa mara nyingi nawe au na mtu yeyote anayeweza kuitumia simu yako kadri itakavyoonekana kwetu. Hutaweza kutumia huduma za M-PESA mpaka tutakapofungua huduma za M-PESA baada ya maombi yako.

7. TOZO
 • 7.1. Tozo zote zimeonyeshwa katika Mwongozo wa Gharama unaochapishwa na M-PESA Limited katika vipindi tofauti na zipo katika Ofisi Kuu ya M-PESA Limited na au Tovuti ya Vodacom.
 • 7.2. Tozo ni kwa mujibu wa ushuru na ada zilizopo katika viwango vilivyowekwa kwa muda huo.
 • 7.3. Tozo zote zinazolipwa nawe kulingana na matumizi ya Huduma za M-PESA zinaweza kukatwa kutoka katika Akaunti yako bila ya kukupa taarifa ya awali.

  • 8. MIAMALA
   • 8.1. Miamala yote ya Makato kutoka katika Akaunti yako itafanywa kwa Maelekezo ya Kuhamisha yanayoidhinishwa kwa namba ya siri ambayo utaichagua wakati wa kujisajili, au kwa njia nyingine tunayoweza kuielezea katika vipindi mbalimbali. Uthibitisho wa Utambulisho utahitajika kabla ya Muamala wowote kuweza kufanywa na Utambulisho utakaowasilishwa utarekodiwa na Wakala kwa kila Muamala.
   • 8.2. Akaunti yako itaingiziwa fedha wakati utakaponunua fedha za kielekroniki kwa kufanya malipo au wakati fedha za kielektroniki zitakapohamishiwa katika Akaunti yako ya M-PESA kutoka kwa Mteja mwingine na kiasi chote hicho cha fedha kitashikiliwa na Mdhamini kwa agizo lako.
   • 8.3. Unaweza kushindwa kufanya Miamala yoyote kutoka katika Akaunti yako katika tukio ambapo huna kiasi cha kutosha cha fedha za kielektroni katika Akaunti yako kukidhi thamani ya Muamala na Tozo zinazotakiwa.
   • 8.4. Mfumo wa M-PESA utahakikisha na kuthibitisha Miamala yote iliyofanywa kwenye Akaunti yako kwa ujumbe mfupi wa maandishi kwako. Kumbukumbu za Mfumo wa M-PESA zitachukuliwa kuwa sahihi isipokuwa kama imethibitishwa kuwa na tofauti.
   • 8.5. Mara utakapopatiwa Akaunti, utaweza kufanya miamala ifuatayo:-
   • 8.5.1. Kufanya Muamala wa Kuingiza fedha kwa kulipa fedha taslimu moja kwa moja kwa Wakala na kubadilisha na kiasi hichohicho cha fedha za kielektroni kitakachoingizwa kwenye Akaunti yako. Mara fedha hizo zitakapoingizwa, Mfumo wa M-PESA utaingiza fedha za kielektroni inavyopaswa kwenye Akaunti yako.
   • 8.5.2. Kufanya Muamala wa kutoa fedha: -
   • 8.5.2.1. Kwa kubadilisha fedha za kielektroni ili kupata fedha taslimu kwa Wakala yeyote kwa kutuma Maelekezo ya Uhamishaji kwenye mfumo wa M-PESA kulingana na ambavyo Wakala atalipa kiasi kilekile cha fedha taslimu kwako.
   • 8.5.2.2. Uhamishaji wa fedha za kielektroni kwa Mteja mwingine (Mfano: Mteja wa M-PESA au Mteja ambaye sio wa M-PESA) kwa kutuma Maelekezo ya Kuhamisha fedha kwenye Mfumo wa M-PESA kwenda kwenye akaunti ya Mteja huyo, ukiainisha kiasi kitakachohamishwa.
   • 8.5.2.3. Kununua muda wa maongezi wa Vodacom kwa kutuma maelekezo ya kuongezewa muda wa maongezi kwenye Mfumo wa M-PESA na kutoa Maelekezo ya Uhamishaji kwa kiasi kilekile cha fedha za kielektroni kwa Mlipwaji Aliyekusudiwa wa M-PESA Limited.
   • 8.5.2.4. Ununuzi wa muda wa maongezi wa mitandano mingine kwa kutuma maelekezo ya kuongezewa muda wa maongezi kwenye Mfumo wa M-PESA na kutoa Maelekezo ya Uhamishaji kwa kiasi kilekile cha fedha za kielektroni kwa Mpokeaji Aliyekusudiwa wa mtandao mwingine.
   • 8.5.2.5. Kununua Bidhaa na/au Huduma kutoka kwa Wauzaji wa Rejareja Walioidhinishwa kwa kutuma Maelekezo ya Uhamishaji kupitia mfumo wa M-PESA ya kiasi kitakachohamishiwa kwenye Akaunti ya Muuzaji wa Rejareja Aliyeidhinishwa kwa ajili ya ununuzi wa Bidhaa na/au Huduma.
   • 8.5.3. Baada ya Muamala wowote wa Kuingiza fedha na Muamala wa Kutoa fedha kufanywa Mfumo wa M-PESA utaingiza au kutoa kwenye Akaunti yako mara kiasi kitakapoingizwa, kutolewa au kuhamishwa nawe kutoka katika Akaunti yako.
   • 8.5.4. Muamala wowote ambao haukuhitimishwa ndani ya siku 7 au 30 za Maelekezo ya Uhamishaji ya kwanza yaliyotolewa muamala huo utafutwa moja kwa moja na taarifa ya ujumbe mfupi wa maandishi itatumwa kupitia mfumo wa M-PESA wa kufuta utapelekwa kwa Mteja anayetoa Maelekezo ya Uhamishaji.
   • 8.5.5. Mfumo wa M-PESA utathibitisha kila Muamala utakaofanywa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi pamoja na salio lililohuishwa la Akaunti yako.
   • 8.5.6. uamala wowote wa Kutoa fedha utakaotolewa kwa kutumia namba ya siri utatozwa kwenye Akaunti. Unakubali kuwa, isipokuwa mpaka M-PESA Limited itakapopokea taarifa kutoka kwako, kuwa namba yako ya siri, si salama tena na/au kuwa simu yako imepotea au kuibwa, M-PESA Limited inaweza kutegemea katika matumizi ya namba ya siri kama ushahidi wa kuhitimisha ambao Muamala wa Kutoa umeidhinishwa nawe, hata kama kwa hakika umefanywa bila ya mamlaka yako. M-PESA Limited haitahitaji uthibitisho wowote wa maandishi wa Maelekezo yoyote ya Muamala.
   • 8.5.7. Hatuwezi kurudia au kurudisha Maelekezo yoyote ya kuhamisha fedha kwa sababu yoyote ikiwa ni pamoja na tukio la mgogoro wowote na Mteja mwingine yeyote au Muuzaji wa Rejareja Aliyeidhinishwa. Unawajibika kutatua mgogoro wowote utakaotokea na Mteja mwingine yeyote au Muuzaji wa Rejareja Aliyeidhinishwa bila ya kutafuta msaada wa MPESA.
   • 8.5.8. Akaunti yako inaweza kuendeshwa tu kwa kutumia Mawakala/Wauzaji wa Rejareja katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
   • 8.6. Kila Muamala utatolewa na namba ya pekee ya stakabadhi ambayo inajumuishwa katika ujumbe mfupi wa maandishi wa uthibitisho unaotumwa kwako pamoja na salio lililohuishwa la Akaunti yako. Namba hii ya stakabadhi inatumiwa kufuatilia & kutambua Miamala yote iliyofanywa katika Akaunti yako.
   • 8.7. Umetuidhinisha kuwasilisha jina lililosajiliwa la M-PESA na namba ya simu kwa mteja mwingine wa M-PESA kuboresha uhamishaji wa fedha kwa mteja. Kwa mfano, katika kutoa uthibitisho wa utambulisho wa mpokeaji kabla, wakati au baada ya kutuma au uhamishaji wa fedha.
   • 8.8. Wakati unahamisha fedha kwa upande wa tatu kwa akaunti ya makusanyo ya biashara ya M-PESA, tutatuma data za muamala kwa upande huo wa tatu kwa ajili ya uchakataji kwa kutumia seva jumuishi za upande wa tatu. M-PESA Limited haitawajibika kwa kushindwa kukamilika kwa muamala kwa upande wa tatu na utawajibika kwa tozo zote za M-PESA katika Miamala iliyokamilika ya M-PESA./li>

   9. USALAMA NA MATUMIZI YASIYOIDHINISHWA
   • 9.1. Namba ya siri moja tu ndiyo inaweza kuunganishwa katika Akaunti yako wakati wowote.
   • 9.2. Ni wewe tu (mmiliki) unaweza kutumia namba ya simu ya mkononi na namba ya siri.
   • 9.3. Unawajibika kwa uwekaji wa usalama na matumizi bora ya simu yako, kwa kutunza namba yako ya siri, na namba yako ya kuanzia kwa Miamala yako yote inayofanyika kwenye akaunti yako kwa kutumia namba yako ya siri.
   • 9.4. Uthibitishaji wa utambulisho kuwa wewe ni mmiliki sahihi wa akaunti utajumuisha pamoja na mambo mengine japo si haya tu, aina ya kitambulisho chako, namba ya kitambulisho, maelezo binafsi, tarehe ya kuzaliwa, salio katika Akaunti ya M-PESA, miamala 5 ya mwisho yenye maelezo mengine yoyote yanayofaa yatatumiwa kuthibitisha utambulisho wako wakati utakapopiga Kituo cha Huduma, lakini usionyeshe namba yako ya siri kwa mtu yeyote ikiwa ni pamoja na mtu anayepokea simu yako katika Kituo cha Huduma kwa Wateja.
   • 9.5. Unakiri kwamba, kwa kutumia huduma hii unathibitisha kuwa hutatumia huduma kwa madhumuni yoyote ya uhalifu au rushwa na utawajibika kwa matokeo yoyote yatakayotokana na uhalifu, athari, ukosefu wa maadili na vitendo vya kinyume cha sheria katika matumizi ya huduma hii.

   10. WAJIBU WAKO
   • 10.1. Utawajibika kwa Tozo zote zilizopo katika Ushuru uliopo kwa Muamala wowote uliofanywa ikiwa ni pamoja na miito iliyofanywa katika Mtandao wetu kwa kutumia simu ya mkononi iwe miito hiyo ilifanywa nawe au mtu mwingine yeyote au bila ya mamlaka au ufahamau wako.
   • 10.2. Unawajibika kwa vitu vyovyote vilivyohamishwa na au mawasiliano, ambayo yanaainishwa kama kashfa, kinyume cha sheria au kuvunja hakimiliki yoyote na utafidia na kuendelea kutufidia dhidi ya madai yoyote na gharama zilizofanywa dhidi yetu.
   • 10.3. Usitumie Huduma za M-PESA kufanya kosa lolote kinyume cha Sheria.

   11. MABADILIKO
   • 11.1. Tuna haki ya kubadilisha Masharti na Kanuni hizi au Ushuru wakati wowote na kwa kutoa taarifa ya awali na sababu kwako. Mabadiliko yatatolewa taarifa kwa njia ya matangazo kwa ujumbe mfupi wa maandishi, au kwa njia ya Tovuti yetu na au kwa kutumia njia nyingine yoyote inayofaa ILIMRADI utastahili kuwa umetaarifiwa juu ya mabadiliko yoyote hayo bila ya kujali kuwa jambo hilo linaweza kuwa halijaingia akilini mwako.
   • 11.2. Kwa kuendelea kutumia Huduma za M-PESA utastahili kuwa umekubaliana na mabadiliko yaliyoonyeshwa katika kifungu cha 11.1 hapo juu. Iwapo hutakubaliana na mabadiliko yoyote usiendelee kufanya Miamala yoyote vinginevyo utapaswa kuwa umekubali mabadiliko hayo.

   12. WAJIBU WA MDHAMINI
   • 12.1. Mdhamini anakubali kwamba anashikilia Malipo yote yaliyopokewa kulingana na Ununuzi wa fedha za kielektroni au uhamishaji wa fedha za kielektroni katika Akaunti yako ("Kiasi cha Mdhamini") kwa imani na faida yako na kwamba utafaidika kwa stahili za Kiasi chote hicho cha Dhamana kilichomo kwenye Akaunti yako. Unakubali kuwa Mdhamini anaweza kuzishughulikia kumbukumbu za Mfumo wa M-PESA kama ushahidi wa kuhitimisha wa kiasi cha fedha za kielektroni wakati wowote kilichomo kwenye salio la Akaunti yako na Mdhamini hafungwi kufanya ukaguzi wowote huru wa stahiki zako za faida kwa Kiasi cha Dhamana. Zaidi unakubali kwamba, kuhusiana na malipo yoyote kwako kuhusiana na stahiki zako kwa Kiasi cha Dhamana, tunaweza kufanya kwa maelekezo tuliyopewa nawe kwa kutumia namba yako ya siri au maelekezo yanayokusudiwa kutolewa nawe kwa kutumia namba yako ya siri hata kama kiuhalisia yametolewa na upande wa tatu.
   • 12.2. Unakubali kuwa Mdhamini hatakuwa na wajibu wa kuwekeza Kiasi cha Dhamana zaidi ya kwa njia ya kushikilia kiasi hicho katika Akaunti ya Dhamana. Zaidi unakubali kuwa, faida yoyote itakayopatikana katika Kiasi cha Dhamana, utakuwa na stahiki za faida katika riba hiyo kwa namna itakayoamuliwa na M-PESA Limited na Mdhamini atastahili kubakiza riba hiyo kulipia gharama zake na matumizi na/au kulipa kiasi hicho kwa M-PESA Limited kwa gharama na matumizi ya uendeshaji wa Mfumo wa M-PESA na/au kulipa kiasi hicho katika kifungu hicho cha hisani kama Mdhamini atakavyoamua.

   13. UWAJIBIKAJI NA MAMBO YASIYOJUMUISHWA
   • 13.1. Katika tukio ambapo tunatakiwa kubadilisha au kupanga tena uwekaji wako wa namba za mawasiliano kukidhi mahitaji ya kiudhibiti au kwa sababu nyingine yoyote uwajibikaji wetu utakuwa na ukomo wa kubakiza Akaunti yako na inapowezekana, uhamishaji wa Akaunti yako kwenda MSIN mpya, na endapo itashindikana utalipwa salio lililopo katika Akaunti yako kwa fedha taslimu.
   • 13.2. Kwa kiasi kinachoruhsiwa kisheria hatujumuishi haki ya aina yoyote, ama kwa maelezo au kwa ishara, ambayo haimo katika kanuni na mashati haya.
   • 13.3. Wakati Mawakala wa M-PESA wanatakiwa kutoa Huduma za M-PESA kulingana na maelekezo yetu hatutawajibika au kustahili kwa vitendo vya udanganyifu au uendeshaji ambao ni kinyume na maelekezo yetu wanapokupatia huduma za M-PESA au huduma nyingine yoyote. M-PESA Limited imeweka hatua za kuhakikisha unathibitisha au kukataa miamala yote inayofanywa na Wakala wa M-PESA kabla haijakamilika. M-PESA Limited haitawajibika kwa uzembe wako wakati wa kufanya miamala hiyo na Mawakala wa M-PESA.
   • 13.4. Hatutawajibika kwa upotevu wowote unaoupata isipokuwa kama umesababishwa moja kwa moja na upuuzaji wetu au kufanya kwa makosa kabisa. Iwapo tutapuuza au kukosea, tutawajibika tu kwa kiasi cha msingi cha hasara iliyotokea.

   14. MENGINEYO
   • 14.1. Kanuni na Masharti haya (kama ambavyo yanaweza kurekebishwa katika vipindi mbalimbali) yanafanya mkataba wa kisheria unaokufunga wewe na warithi na wateule wako.
   • 14.2. Kanuni na Masharti haya yanaweza yasirithiwe na mtu mwingine yeyote.
   • 14.3. Hakuna kushindwa au kuchelewa kutakakofanywa na mmoja wetu katika kutekeleza haki yoyote ya humu kutakakochukuliwa kama msamaha, hakuna utendaji mmoja au wa sehemu wa yoyote yatakayozuia utendaji zaidi au utendaji mwingine au utendaji wa haki nyingine yoyote.
   • 14.4. Haki zilizomo humu ni za jumla na hazijitengi na haki zozote zinazotolewa na sheria.
   • 14.5. Iwapo kifungu chochote cha Masharti haya ya Matumizi kitaonekana na msuluhishi yeyote, mahakama au chombo chenye mamalaka ya usimamizi kisheria kuwa si halali au kutotekelezeka, kutokuwa halali au kutotekelezeka huko kwa kifungu hicho hakutaathiri vifungu vingine vilivyomo na vifungu vyote ambavyo havijaathirika na kutokuwa halali au kutotekelezeka huko vitabaki kutekelezwa na kufanywa kiukamilifu.

   15. TAARIFA
   • 15.1. Unaweza kupata ulizo la salio kutoka katika simu yako ya mkononi na kuuliza miamala yoyote iliyofanywa kwa kutumia simu yako ya mkononi au piga katika Kituo cha Huduma kwa Wateja au nenda katika duka lolote la Vodacom.
   • 15.2. Taarifa zilizochapishwa za Akaunti yako zinaweza kuombwa nawe katika duka la M-PESA Limited lililoidhinshwa. Taarifa hizo zitatolewa baada ya uthibitisho wa uangalifu wa maombi na baada ya malipo ya ada ya huduma dukani hapo.
   • 15.3. Tutaifunga Akaunti yako baada ya kupokea maombi kutoka kwako.

   16. KUSHINDWA KUFANYA KAZI AU DOSARI YA SIMU
   • 16.1. Hatuwajibiki kwa hasara yoyote itakayotokea kutokana na kushindwa kokote, dosari, au kuchelewa katika Mitandao yoyote ya simu ya mkononi, simu ya mkononi, intaneti au vituo au mitandao mingine yoyote inayosaidia au kuchangia, kutokana na mazingira yaliyo juu ya uwezo wetu. Utapewa taarifa kuhusu mazingira yaliyo juu ya uwezo wa M-PESA Limited kwa njia ya tovuti ya Vodacom, ujumbe mfupi wa maandishi au njia nyingine zozote za mawasiliano kwa umma.

   17. MAWASILIANO
   • 17.1. Tunatakiwa kukutumia taarifa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa namba yako ya simu ya mawasiliano iliyotolewa katika fomu yako ya maombi. Ujumbe huu mfupi wa maandishi ni kwa ajili ya kupewa taarifa tu.
   • 17.2. Tuma taarifa yoyote halali kwetu kwa anwani yetu tuliyoichagua: Huduma ya M-PESA, Vodacom, S.LP 2369, Dar es Salaam, au kuipeleka katika Ofisi Kuu ya Vodacom, Ghorofa ya 7, Vodacom Tower Ursino Estate Kitalu No. 23, Barabara ya Bagamoyo

   18. KWA UJUMLA
   • 18.1. Lazima ulipe gharama zetu zote katika kurudisha kiasi chochote ulichotukopa ikiwa ni pamoja na ada za kisheria, ada ya ukusanyaji na ada ya kukutafuta.
   • 18.2. Utakuwa na haki, kwa busara yako, kufuta masharti haya ndani ya kipindi cha siku kumi baada ya kujisajili kwa huduma za M-PESA.
   • 18.3. Cheti kitakachotiwa saini na meneja wetu yeyote (ambaye uteuzi wake hauhitaji kuthibitishwa) kinachoonyesha kiasi ulichotukopa ni uthibitisho unaojitosheleza wa taarifa zilizoelezwa katika cheti, isipokuwa kama itathibitika kinyume chake.
   • 18.4. Kulingana na kiwango kinachoruhusiwa chini ya sheria tutawajibika kwa hasara ya moja kwa moja na itakuwa na ukomo katika jumla ya thamani yote ya huduma iliyonunuliwa na kulipwa nawe chini ya mkataba huu.
   • 18.5. Unapaswa kutuarifu haraka kwa mabadiliko yoyote ya maelezo yako katika Fomu yako ya Usajili.
   • 18.6. Unakubali kuwa taarifa zako, ikiwa ni pamoja na taarifa zako binafsi, mazungumzo yako na Kituo chetu cha Huduma kwa Mteja yatahifadhiwa kwa madhumuni ya kuweka kumbukumbu kwa miezi 3 kuanzia tarehe ya mazungumzo na Miamala yako itarekodiwa kwa madhumuni ya kuweka kumbukumbu kwa miaka 7 kuanzia tarehe ya kufunga Akaunti yako.
   • 18.7. Kukiwa na tatizo lolote linalohusiana na utoaji wa huduma katika kanuni na masharti haya utatoa taarifa kwa kupiga simu katika Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Vodacom kwa namba 100 au kwa kwenda katika duka la Vodacom lililo karibu kwa msaada zaidi.
   • 18.8. Hakimiliki zote, alama za biashara na haki nyingine za milki ya ubunifu zilizotumika kama sehemu ya Huduma za M-PESA au zilizomo katika nyaraka zetu ni mali ya M-PESA Limited. Unakubali kuwa huna haki yoyote hapa.

   <>strong>19. HUDUMA KWA MTEJA
   • 19.1.1. Unaweza kuwasiliana Nasi kupitia namba 100 ya kituo chetu cha huduma kwa mteja au njia nyingine za mawasiliano ya huduma kwa mteja zilizotolewa katika mitandao ya kijamii au Tovuti yetu (yaani, TOBi Online au Wasilisha maswali) kutoa taarifa ya migogoro, madai au hitilafu zozote katika Huduma.
   • 19.1.2. Wawakilishi wetu wa huduma kwa mteja watashughulikia masuala yaliyotolewa taarifa kwa mujibu wa taratibu zetu za kawaida za kushughulikia malalamiko.
   • 19.1.3. Simu zitakazopigwa katika kituo cha simu zinaweza kurekodiwa kwa ajili ya kuhakikisha ubora au kwa ajili ya taratibu zozote za kikazi ikiwa ni pamoja na, bila ya ukomo, kudhibiti ubora, mafunzo na kuhakikisha uendeshaji bora wa mifumo.
   • 19.1.4. Wasilisha maelezo yako yote muhimu yahusianayo na malalamiko yako (m.f tarehe & muda wa tukio, bidhaa, maelezo ya mtu uliyeongea naye kuhusiana na malalamiko yako n.k) itatusaidia kukuhudumia vizuri. Mchakato wa utoaji malalamiko ni bure
   • 19.1.5. Malalamiko ya fedha za simu - Kama malalamiko yako hayajafanyiwa kazi na/au kuto kukuridhisha, Mlalamikaji una haki ya kuwasilisha malalamiko Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ndani ya siku 21 baada ya kuyawasilisha Vodacom, kwa kutumia namna hii:
   • 19.1.5.1. Hatua ya 1: Ingia kwenye tovuti ya BoT Website: https://www.bot.go.tz kupata fomu ya malalamiko ya FCC
   • 19.1.5.2. Hatua ya 2: Tuma fomu ya malalamiko kwenda BoT kwa kutumia moja kati ya njia zifuatazo:
   • 19.1.5.2.1. Kwa njia ya kufika moja kwa moja The Financial Consumer Unit Bank of Tanzania Head Office, 2 Mirambo Street, Dar Es Salaam, Ground floor, Middle building.
   • 19.1.5.2.2. Kwa njia ya Posta: The Financial Consumer Unit Bank of Tanzania P. O. Box 11884, Dar Es Salaam,
   • 19.1.5.2.3. Kwa njia ya nukushi: +255 22 2234067
   • 19.1.5.2.4. Kwa njia ya simu: +255 22 2233265/ +255 22 2233246
   • 19.1.5.2.5. Kwa njia ya barua pepeTuma kwa; Head of the Financial Consumer Protection Unit i.e. complaints@bot.go.tz
   • 19.1.5.2.6. Kwa njia ya tovuti/mtandaoniOnline) https://www.bot.go.tz
   • 19.1.6. Malalamiko ya fedha za simu - Kama hujaridhishwa na maamuzi au marejeo ya uamuzi wa Benki Kuu ya Tanzania kuhusiana na malalamiko yako ya pesa za kielektroniki, mlalamikaji anaweza kupeleka maombi yake Mahakamani kusikilizwa tena.
   • 19.1.7. Malalamiko ya Mifumo ya Mawasiliano ya Simu: - Kama malalamiko yako hayajafanyiwa kazi na/au kuto kukuridhisha ndani ya siku 30 baada ya kuyawasilisha Vodacom, una haki ya kuwasilisha malalamiko yako kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kutumia namna hii:
   • 19.1.7.1. Hatua ya 1: Ingia kwenye tovuti ya TCRA: www.tcra.go.tz kupata fomu ya malalamiko ya TCRA
   • 19.1.7.2. Hatua ya 2: Tuma fomu ya malalamiko kwenda TCRA kwa kutumia moja kati ya njia zifuatazo:
   • 19.1.7.2.1. Kwa njia ya kufika moja kwa moja The Consumer Affairs Department Tanzania Communication Regulatory Authority Mawasiliano Towers, Plot No 2005/1, block C, Sam Nujoma Road, Dar es Salaam
   • 19.1.7.2.2. Kwa njia ya Posta: The Consumer Affairs Department Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA) Towers, P. O. Box 474, Dar es Salaam
   • 19.1.7.2.3. Kwa njia ya nukushi: +255 22 2412009/10
   • 19.1.7.2.4. Kwa njia ya barua pepe: complaints@tcra.go.tz
   • 19.1.7.2.5. Kwa njia ya tovuti/mtandaoni(Online): www.tcra.go.tz/complaints@tcra.go.tz
   • 19.1.8. Malalamiko ya Mifumo ya Mawasiliano ya Simu: - Kama hujaridhishwa na maamuzi ya TCRA, , Mlalamikaji una haki ya kuwasilisha malalamiko yako Tume ya Ushindani (FCC) ndani ya siku 21 kwa kutumia namna hii:
   • 19.1.8.1. Hatua ya 1: Ingia kwenye tovuti ya FCC: www.competition.or.tz kupata fomu ya malalamiko ya FCC
   • 19.1.8.2. Hatua ya 2: Tuma fomu ya malalamiko kwenda FCC kwa kutumia moja kati ya njia zifuatazo:
   • 19.1.8.2.1. Kwa njia ya kufika moja kwa moja: The Fair Competition Commission GEPF house 2nd Floor, Plot No 37, Regent Estate Bagamoyo Road, Dar Es Salaam.
   • 19.1.8.2.2. Kwa njia ya Posta: The Fair Competition Commission (FCC), GEPF House, P. O. Box 7883, DSM, Tanzania
   • 19.1.8.2.3. Kwa njia ya nukushi: +255 22 2926126
   • 19.1.8.2.4. Kwa njia ya barua pepe: info@competition.or.tz
   • 19.1.8.2.5. Kwa njia ya tovuti/mtandaoni: www.competition.or.tz

   20. MAMLAKA ZA SHERIA NA UTATUZI WA MIGOGORO
   • 20.1.1. Kanuni na Masharti haya yanaongozwa na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   • 20.1.2. Malalamiko au mgogoro wowote utakaotokea au utakaohusiana na Huduma zozote au Kanuni na Masharti haya utapelekwa M-PESA Limited kama ilivyoainishwa kwenye kifungu namba 19 toka malalamiko au mgogoro huo ulipotokea.Kushindwa kupeleka malalamiko au mgogoro huo ndani ya siku hizi kutaipa M-PESA Limited uchaguzi wa kukataa malalamiko au mgogoro huo.
   • 20.1.3. Katika tukio la kutoridhishwa na matokeo kulingana na kifungu cha 20.2 hapo juu upande ambao haujaridhishwa utafata taratibu zilizoainishwa katika kifungu namba 19.

Mipaka ya Miamala kwa Wateja

Customer Transaction Limits

Viwango vinavyofuata vinatumika kwa miamala ya mteja wa M-Pesa kama Sheria ya Taifa ya Mfumo wa Malipo ya 2015 - Kanuni za Fedha za umeme zilizotolewa na BoT

  

Kipengee

Tier1

Tier2

Tier3

kiwango cha juu cha kuhamishar

1,000,000

3,000,000

10,000,000

kiwango cha juu cha kila siku kuhamisha

1,000,000

5,000,000

50,000,000

Kiwango cha juu cha kuifadhi

2,000,000

10,000,000

50,000,000

kiwango cha juu kufanya miamala kwa mwaka*

30,000,000

230,000,000

Not Applicable

Taarifa muhimu za Mteja**

Mpangilio wa kawaida

Nakala ya Kitambulisho/b>

ID, Leseni ya Biashara na cheti cha TIN

 

* Kiwango cha juu kufanya miamala kwa mwaka inahusiana na miamala inayoingia / kutoka katika akaunti ya wateja. Baada ya kufikia kikomo hiki, mteja hawezi kuwa na uwezo wa kupokea fedha za ziada mpaka mwanzo wa mwaka wa kalenda ijayo.

** Kitambulisho kinachokubalika kwa sasa ni Kitambulisho cha Taifa na Hati ya Kusafiria (kwa wanadiplomasia), au namba ya NIDA ukiambatanisha na moja ya vitambulisho kama Leseni ya Kuendesha gari, Kitambulisho cha kupiga kura au Hati ya Kusafiria

**(Tier3) Kundi njia ya 3, hati zote za ID (vitambulisho kama ilivyohainishwa apo awali), cheti cha TIN na Leseni ya Biashara zote zinahitajika, Haikubaliki kutoa moja au mbili tu.

M-Pesa AML Awareness

What is Money Laundering?

This is the process used to disguise the true origin of money or property obtained from any criminal activity.

Why do people do Money Laundering?

Criminal launder money or property to distance the proceeds of crime from their criminal activities, making the proceeds to appear to have originated from legitimate sources.

What offences which constitute Money Laundering?

 • People trafficking
 • Prostitutions
 • Breach of Sanction
 • Counterfeiting
 • Fraud
 • Theft
 • Bribery and Corruption
 • Drug trafficking
 • Tax evasion

 

What do you understand about Terrorist Financing?

 • Terrorism financing is an activity that provides financial support to designated terrorist groups
 • Source of Terrorism financing can came from both legitimate and illegitimate sources.
 • Example of legitimate sources

–         Charity from people and organizations

–         Governments.

Example of illegitimate sources

 • Fraud, Drugs dealing, human trafficking, weapons deals.

 

Money Laundering Process

 • Three stages are usually involved when Money Laundering takes place in order to disguise its original source.
 • These three stages are:
  • Placement – where illegal money is ‘‘placed’’ into an Financial system, such as an   

M-PESA account or bank account without arousing suspicion.

 • Layering – where illegal funds will be moved around from account to account. This often involves reducing the funds into smaller amounts and using different people and business to try and disguise its original source.
 • Integration – where illegal funds are ‘‘integrated’’ back into the legal financial system and appears to be legitimate funds or assets. This can be done though Charity donations, Real Estate development, Investments
 • IMPORTANT – all three stages DO NOT have to occur for Money Laundering to take place. If you suspect activity in any way, it MUST be reported. 
 • The amount of money laundered each year by criminals is over £ 1 trillion
 • Governments.
  • Example of illegitimate sources
 • Fraud, Drugs dealing, human trafficking, weapons deals.

 

What are the consequences of for both employee/customer and company for failing to comply with AML laws?

Company

 • Civil and criminal liability
 • Fines
 • Loss of reputation
 • Limitation on business
 • Loss of operating license

Employee/Customer

 • Personal liability such as fines and imprisonment
 • Disciplinary action including termination of employment for employee

 

What do you understand about “KYC”?

Is the customer identification and verification process. Identification is done though the government issued ID’s such Passport or National ID or Driver License or Voter ID which must have date of birth, country of residence or nationality.

 

What’s the consequences of not knowing your customers?

 • Failure to effectively detect/stop and report suspicious activities
 • Undesirable individuals/entities may end up dealing with us, could cause significant reputational risk to Vodafone
 • Terrorists could use our product channels to remit/receive funds and same could be used to finance a terrorist activity.
 • Breach of AML policy and possible fines
 • Non –compliance of local regulations and laws – incur severe penalties /criticism from regulators

 

Why do we do Transaction Monitoring?

The purpose of Transaction monitoring is to flag unusual activity/transactions for proper investigation and review.

Below are 3 “red flags” that may indicate possible suspicious or unusual transaction

 • Displays dishonesty
 • Reluctance to provide information
 • Incomplete picture of business affairs
 • Abnormal business conduct
 • No business sense

 

 

 

 

What MLRO and SAR stands for?

 • Money Laundering Reporting Officer (MLRO)
 • Suspicious Activity Reporting (SAR)

 

MLRO contact details when reporting suspicious activities (SAR)

 • Phone number; 255754703084

Email; aml@Vodacom.co.tz

M-Pesa AML Knowledge

Name…………………………………………………………….         Company……………………………………………….

Anti-Money Laundering Knowledge Test

 

 1.       What is “Money Laundering”?

........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

 2.       Name at least 4 crimes which underlying Money laundering activities.

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

3.       What is the key difference between Money laundering and Terrorist Financing?

...................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

 4.       Mention 3 stages of Money Laundering?

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….

 5.       What are the consequences of for both employee and company for failing to comply with AML laws?

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

6.       Explain what “KYC” is all about

………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………

 7.       List 3 consequences of not knowing your customer?

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

 8.       What is the purpose of “Transaction Monitoring”?

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

 9.       Discuss 3 “red flags” that may indicate possible suspicious or unusual transaction

……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………….

10.   a. What MLRO stands for?

 

………………………………………………………………………………………………………………………………………………..

b. What SAR stands for?

 

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………….. 

 

c. What is the email address for reporting SAR for Tanzania?

 

…………………………………………………………………………………………………………………………………………………….. 

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa