Je, wewe ni Mwanafunzi wa Chuo?

Furahia ukiwa umeunganishwa na mtandao SUPA wakati uko Chuo!

Tovuti ya kujiunga na ofa ya Mwanafunzi wa Chuo
 • Vodacom UNI ofa ni nini?
 • Unapataje / Kujiunga UNI Ofa?
 • Nani anaruhusiwa kupata UNI Ofa?
 • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
 • Vigezo na Masharti

Vodacom UNI ofa ni nini?

Vodacom UNI ofa ni nini?

Vodacom inakuletea mahali ambapo unaweza kujisajili kama mwanafunzi wa chuo na ukaweza kupata UNI Ofa. Ofa hii itakupa ofa za kipekee na menu ya aina yake kwa wanafunzi waliojisajili.

Mara baada ya kusajiliwa piga *149*42# kupata UNI Ofa zote au kupitia kurasa za mtandao wa Vodacom au MyVodacom App.

Wahi na ujiandikishe ili upate ofa za aina yake kama ya 2000Tsh na MB512 + Dakika 180 VODA + Dakika 20 mitandao yote + SMS 200 kwa siku 7 au chagua Pinduapindua UNI Ofa. Kujua zaidi kuhusu Pinduapindua bonyeza linki ifuatayo PinduaPindua

Unapataje / Kujiunga UNI Ofa?

Unapataje / Kujiunga UNI Ofa?

Ni rahisi, tembelea tovuti ya https://ycckwl.vodacom.co.tz/ycc kwenye simu yako ya mkononi au desktop.
Kujiandikisha kupata UNI Ofa ni bure kabisa au kwa msaada wa kujiandikisha pia tembelea Vodashop.

Nani anaruhusiwa kupata UNI Ofa?

Nani anaruhusiwa kupata UNI Ofa?

Ofa hizi zinapatikana tu kwa wateja waliosajiliwa kwenye mtandao wetu ambao wanastahiki kuwa wanafunzi.
Ofa hizi ni kwaajili ya wanafunzi waliosajiliwa na NACTE au TCU.

Maswali yaulizwayo mara kwa mara

1. UNI ofa ni nini?

Hii ni ofa maalum kwa waliokuwa wamesajiliwa.

2. Nani anastahili kupa UNI ofa?

OFA ni maalum kwa wanafunzi wa chuo waliosajiliwa na NACTE na TCU.

3. Najisajili vipi?

Kujisajili Tembelea Tovuti yetu au fika Vodashop yoyote karibu yako.

4. Nini ninahitaji kujisajili kupata ofa?

Unahitaji kuwa na Kitambulisho cha wakati huo cha Mwanafunzi, au cha Nacte au TCU cha mwanafunzi.

5. Napata OFA mara t baada ya Kujisajili?

Utajulishwa kwa Meseji mara utakapokua umekubaliwa ombi lako, pia unaweza kuangalia kama umekubaliwa ombi kwenye tovuti.

6. Je kuna Gharama ya kujisajili kupata Ofa hii?

Ni bure na hakuna Gharama yoyote kujisali na kupata Ofa hii.

Vigezo na Masharti

VIGEZO NA MASHARTI YA VIFURUSHI VYA UNI

1. Fasili
 • 1.1 Vifurushi vya UNI maana yake ni huduma ya vifurushi vya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na inteneti ambavyo vinapatikana kwa Wateja ambao wanafunzi halali wa chuo kikuu chochote nchini Tanzania na wapo katika orodha ya wanaostahili kupata ofa za Vodacom.
 • 1.2 Lipa Kadiri Unavyotumia maana yake tozo/gharama zinazotozwa unapotumia Huduma bila kifurushi.
 • 1.3 Viwango vya “Pulse” maana yake ni kipimo cha chini kinachotozwa kila unapotumia Huduma.

2. Matumizi
 • 2.1 Vigezo na Masharti haya yatatambuliwa humu kama "Vigezo na Masharti/Masharti ya Matumizi" (dhana hizi zitatumika kwa kubadilishana) yametolewa na Vodacom Tanzania PLC (itatumika/kutambulika kama “Vodacom” au “Sisi” au “sisi wenyewe” au “yetu”) kwa ajili ya kutumiwa na Watumiaji/Wateja wa Vodacom (“Wateja”) (itatumika/kutambulika kama “wewe” au “yako” au “mtumiaji” “wewe mwenyewe”) ambao hutumia vifurushi vya Vijana (“Huduma”).
 • 2.2 Tafadhali soma Vigezo na Masharti haya na Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Watumiaji wa Vodacom ambayo yatakuwa ni sehemu ya Vigezo na Masharti haya, yanayopatikana katika tovuti ya Vodacom. Kwa madhumuni ya vigezo na masharti yaliyoelezwa katika waraka huu Vigezo na Masharti haya yatazingatiwa katika matukio yoyote ya mgongano kati ya Vigezo na Masharti haya na Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Watumiaji wa Vodacom..

3. Tozo na Aina ya Huduma
 • 3.1 Vifurushi vya UNI vinapatikana kwa Wateja wanaokidhi vigezo vya kuwa wanafunzi wa chuo kikuu na wamekubaliwa na Vodacom. Uthibitisho wa kitambulisho cha chuo unahitajika.
 • 3.2 Vifurushi vya UNI vinaweza kununuliwa kupitia menyu ya Vodacom USSD kwa kupiga namba (*149*42#) na App ya My Vodacom (My Vodacom App)
 • 3.3 Huduma hizi zinatumika ndani ya Tanzania
 • 3.4 Huduma hizi zinaweza kununuliwa kupitia muda wa maongezi au Mpesa
 • 3.5 Unaweza kununua vifurushi vya UNI mwenyewe au kumnunulia rafiki
 • 3.6 Bei zote za vifurushi vya UNI zinapatikana katika menyu ya USSD (*149*42#). Bei zinajumuisha kodi ya ongezeko la thamani (VAT)
 • 3.7 Unaweza kujiunga na zaidi ya kifurushi kimoja au kujiunga na kifurushi chochote muda wowote.
 • 3.8 Unaweza kuangalia salio bure kwa kupiga *149*60#

4. Matumizi nje ya Kifurushi/ Lipa Kadiri Unavyotumia (PAYG)
 • 4.1 Gharama za Kulipia Kadiri Unavyotumia zitatumika kama zilivyochapishwa kwenye tovuti ya Vodacom iwapo mteja AMEJIUNGA na anatumia Huduma hii bila kuwa na kifurushi.
 • 4.2 Viwango vya Kulipia Kadiri Unavyotumia kwa wateja wa kimataifa na wanaozuru vinatofautiana kutoka nchi moja na nyingine.
 • 4.3 Una haki ya kubatilisha Huduma bila kifurushi kama UMESHAJIUNGA kwa KUJITOA. Hili linaweza kufanyika kwa kupiga simu namba *149*01#>Huduma za Ziada>Matumizi bila kifurushi >Tengua matumizi bila kifurushi.

5. Muda wa Matumizi wa Vifurushi vya UNI
 • 5.1 Muda wa kutumika kwa vifurushi vya UNI ni muda ambao vifurushi vinaweza kutumika.
 • 5.2 Vifurushi vya UNI vya siku vinatumika kwa saa 24 kuanzia muda viliponunuliwa
 • 5.3 Vifurushi vya UNI vya wiki vinatumika kwa siku 7 kuanzia tarehe viliponunuliwa
 • 5.4 Vifurushi vya UNI vya mwezi vinatumika kwa siku 30 kuanzia tarehe viliponunuliwa
 • 5.5 Ukishatumia kifurushi chako chote ulichopewa ndani ya muda wake wa matumizi au endapo muda wake wa matumizi umeisha, gharama za malipo bila kifurushi zitatumika kulingana na mpango ulivyoonyesha ikiwa umejiunga.
 • 5.6 Unaweza kununua kifurushi kingine cha muda kama huo au muda tofauti wa matumizi wakati wowote. Kipaumbele cha matumizi kitatolewa kwa kifurushi kilichonunuliwa kwanza. Ikiwa muda wa matumizi wa kifurushi kilichonunuliwa baadaye ni mdogo kuliko kifurushi kilichonunuliwa awali basi kipaumbele cha matumizi kitahamia kwenye kifurushi chenye muda kidogo zaidi wa matumizi. Wateja hawataweza kutumia vifurushi vyao baada ya muda wa matumizi kuisha. Vifurushi ambayo havikutumika vitaendelea kutumika iwapo utajiunga na kifurushi kipya kabla ya muda wake wa matumizi kuisha. Ikiwa utajiunga na kifurushi kipya baada ya muda wa matumizi kuisha, kifurushi ambacho hakijatumika kitaisha na huduma zote za kifurushi zitasitishwa mara moja baada ya muda wa matumizi ya kifurushi hicho kuisha

6. Muda wa Matumizi na Spidi
 • 6.1 Vifurushi vyote vya UNI vinaweza kutumika wakati wowote ndani ya muda wa matumizi wa kifurushi
 • 6.2 Mtandao wa kisasa wa Vodacom utatoa huduma ya intaneti yenye spidi ya hali ya juu, lakini spidi hiyo inaweza kuaathiriwa na simu/vifaa vinavyotumiwa na wateja. Simu/Kifaa kinachoendana na teknolojia hii kinahitajika ili kupata kasi ya mtandao yenye ubora.
 • 6.3 Kiwango cha Pulse kwa vifurushi vya UNI vya malipo ya kabla na vile vya Kulipia Kadiri Unavyotumia ni 10KB. Viwango vya “pulse” ni kipimo cha chini kinachotozwa kila unapotumia Huduma.

7. Vigezo na Masharti Mengine Yanayotumika
 • 7.1 Vigezo na Masharti haya yatatumiwa pamoja na Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Watumiaji wa Vodacom.
 • 7.2 Iwapo itatokea mkinzano, mpishano au mgongano kwa vigezo na masharti haya na Vigezo na Masharti ya Jumla kwa Watumiaji wa Vodacom kwa Mteja Aliyejiunga, kulingana na umuhimu na matumizi Vigezo na Masharti haya yatazingatiwa yakifuatiwa na Vigezo na Masharti ya Jumla ya Mtumiaji wa Vodacom.
 • 7.3 Mtumiaji au Mteja yeyote anayetumia Huduma zinazotolewa chini ya Vigezo na Masharti haya atachukuliwa kuwa amesoma na kuelewa Vigezo na Masharti husika.
 • 7.4 Tuna haki ya kusitisha Huduma ikiwa:
 • 7.4.1 utatumia Huduma kwa malengo yoyote yasiyoruhusiwa;
 • 7.4.2 tutabaini matumizi mabaya, kukiuka maudhui, vitendo vya udanganyifu au jaribio la udanganyifu linalohusiana na matumizi yako ya Huduma hii;
 • 7.4.3 tutatakiwa au kuombwa kufanya hivyo ili kutekeleza amri au maelekezo au mapendekezo kutoka serikalini, mahakamani, kwa mdhibiti au mamlaka zozote halali;
 • 7.4.4 tutatilia shaka au kujiridhisha kuwa umekiuka Masharti haya ya Matumizi;
 • 7.4.5 tutatakiwa kufanya hivyo ili kutatua matatizo ya kiufundi au kwa sababu za kuhakikisha usalama baada ya kukupa taarifa za kusitisha huduma hii;
 • 7.4.6 kutakuwa na haja ya kusaidia kuhuisha au kuboresha maudhui au utekelezaji wa Huduma hizi mara kwa mara muda baada ya kukupa taarifa za kusitisha huduma hii;
 • 7.4.7 tutaamua kusitisha kwa muda au kuacha kutoa Huduma hii kwa sababu za kibiashara au kwa sababu nyingine yoyote kama itakayoturidhisha.

  • 8. Kusitisha Utoaji wa Huduma
   • 8.1 Huwezi kukatisha matumizi ya Huduma hii baada ya kujiunga na kifurushi kabla ya muda wa matumizi yake kuisha. Huduma hii zitasitishwa baada ya muda wa matumizi ya kifurushi kuisha.

   9. Mabadiliko ya Vigezo na Masharti haya
   • 9.1 Tunaweza kuongeza au kubadili Vigezo na Masharti haya ya Matumizi kulingana na kifungu cha 9.2. Tunaweza kuongeza ada na tozo mpya au kubadili ada na tozo zilizopo wakati wowote; kutokana na sheria mpya, kanuni za kisheria, kanuni za Serikali au matakwa ya leseni, viwango vya kubadili fedha, kuanzishwa au kubadilishwa kwa kodi ya serikali au kutokana na mapitio yoyote ya mipango ya kibiashara ya Vodacom, mabadiliko ndani ya tasnia, mapendekezo kutoka vyombo vya usimamizi au kutokana na sababu nyingine itakayojitokeza.
   • 9.2 Tutakuarifu mapema ikiwa tunataka kuongeza au kubadili vigezo na masharti haya au ikiwa tunataka kuongeza ada na tozo mpya au kubadili zilizopo wakati au baada ya kujiunga na Huduma hizi. Kiasi cha malipo na aina ya taarifa tutakayokupa zitapitia njia mwafaka zinazotumika na kupatikana kwa wakati huo kwa mfano, tunaweza kukutaarifu kwa barua, barua pepe, simu (ikiwa ni pamoja na ujumbe uliorekodiwa au ujumbe mfupi wa simu wa maandishi) au kwa matangazo katika gazeti la kila siku au kila wiki au katika tovuti yetu au njia nyingine yoyote). Unashauriwa pia kutembelea tovuti yetu mara kwa mara ili kuona mabadiliko hayo kama kwa sababu zisizotarajiwa inawezekana hukupata taarifa za hizo.
   • 9.3 Ikiwa hukubaliani na mabadiliko au nyongeza katika Vigezo na Masharti haya, unaweza kusitisha huduma hizi kwa mujibu wa kifungu cha 10 hapo chini. Ikiwa wewe hujatutaka tusitishe Masharti ya Matumizi na bado unatumia Huduma hizi, utachukuliwa kuwa umekubali mabadiliko hayo tangu yalipoanza kutekelezwa.

   10. Usitishaji wa Utoaji wa Huduma na au Masharti ya Matumizi
   • 10.1 Tunaweza kusitisha Masharti haya ya Matumizi wakati wowote tutakapoamua. Usitishaji huo utafanyika baada ya kukupa Taarifa. Taarifa inaweza kuwa kwa barua, baruapepe, simu (ikiwa ni pamoja na ujumbe uliorekodiwa au ujumbe mfupi wa simu wa maandishi) au kwa tangazo katika gazeti la kila siku au la kila wiki au kwenye tovuti yetu au njia nyingine yoyote. Unashauriwa pia kutembelea tovuti yetu mara kwa mara ili kuona mabadiliko yote yaliyofanyika kwa sababu zisizotarajiwa unaweza kuwa hujapata taarifa.
   • 10.2 Unaweza kusitisha Masharti ya Matumizi/Huduma kwa kuacha kutumia Huduma hizi.

   11. Maelezo ya Jumla
   • 11.1 Hatutahusika kwa kuchelewesha au kushindwa kutekeleza majukumu yetu yoyote yanayohusu matumizi ya Huduma hizi ikiwa kuchelewesha au kushindwa huko kumetokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu wa kutoa Huduma hiyo.
   • 11.2 Huwezi kubadili Masharti haya ya Matumizi na huwezi kuhamisha vigezo hivi kwa mtu au biashara nyingine.
   • 11.3 Masharti haya ya Matumizi yataongozwa na kufasiriwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
   • 11.4 Hatutahusika na hasara isiyo ya moja kwa moja na au inayotarajiwa.
   • 11.5 Mawasiliano yote kuhusu Vigezo na Masharti haya yatafanyika kwa Kiingereza au Kiswahili.
   • 11.6 Huduma kwa Wateja
   • 11.6.1 Unaweza kuwasiliana nasi kupitia kituo chetu cha huduma kwa wateja kwa kupiga namba 100 au njia nyingine za mawasiliano ya huduma kwa wateja zinazopatikana katika mitandao yetu ya kijamii au Tovuti (yaani TOBi Online au Kutuma maoni) kutoa taarifa kuhusu migogoro, madai au tofauti zozote zinazojitokeza katika Huduma hizi.
   • 11.6.2 Wawakilishi wetu wa huduma kwa wateja watashughulikia masuala yaliyowasilishwa kwa kwa mujibu wa taratibu zetu za kushughulikia malalamiko zinazopatikana katika maduka na tovuti.
   • 11.6.3 Tunaweza kurekodi au kufuatilia simu zinaopigwa kwenye Vituo vyetu vya Huduma kwa Wateja au kufanya mawasiliano nawe kwa malengo ya kutoa mafunzo, kuwezesha uthibitishaji wa maelekezo na kutathmini kama viwango vyetu vya huduma vinafikiwa.
   • 11.7 Tunaweza kuhamishia kwa mtu mwingine yeyote sehemu au haki zote na/au majukumu kwa mujibu wa Masharti ya Matumizi baada ya kukuarifu. Pamoja na hayo, haki zako za kisheria hazitaathiriwa na majukumu yako hayataongezeka kutokana na uhamishaji huo. Hutaweza kuhamisha haki na wajibu wako kwa mujjibu wa Masharti ya Matumizi.

   12. Mawasiliano & Malalamiko
   • 12.1 Ikiwa unataka kupata taarifa zaidi piga simu kupitia huduma kwa wateja kama ilivyoelezwa hapo juu.
   • 12.2 Ikiwa hujaridhika kwa lolote kuhusiana na huduma zinazotolewa, tafadhali wasiliana na Kituo cha Huduma kwa Wateja. Watafurahi kukusaidia na kukufafanulia taratibu za kushughulikia malalamiko kwa undani. Tutajitahidi kushughulikia malalamiko yako mapema iwezekanavyo. Hata hivyo, mara nyingi malalamiko yatapaswa kufanyiwa uchunguzi. Kama hivyo ndivyo, tutakupa mrejesho ndani ya siku 7 za Kazi kuthibitisha upokeaji wa malalamiko yako na muda wa kuyashughulikia. Ikiwa malalamiko yako hayatapata ufumbuzi, utashauriwa namna ya kufanya..

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa