Huduma Binafsi

Maswali ya Mara kwa mara – Voda Mtonyo

1. Voda Mtonyo ni nini?

Hii ni huduma mpya inayomruhusu mteja wa malipo ya awali kumualika rafiki yake ambaye hajajiunga na PinduaPindua kwa zaidi ya mwezi mmoja na kuweza kupata Bonasi kwa kila Pindua Bando atakayojiunga kutoka Voda Mtonyo.

2. Namna gani mteja anamualika rafiki?

Mteja wa Vodacom mwenye huduma hai ya PinduaPindua anaweza kualika marafiki watatu BURE kila siku na kupata Bonasi kupitia akaunti yake ya M-Pesa, kila rafiki aliyealikwa anapojiunga na Bando za Voda Mtonyo.
Kumualika rafiki piga
*149*03# > 3. Voda Mtonyo > 1. Alika rafiki kisha Ingiza namba ya rafiki
Ili rafiki yako aweze kupatikana kwa mwaliko, inabidi
  • ● Asiwe mteja wa Pindua (asiwe amenunua kifurushi cha Pindua ndani ya siku 30 zilizopita)
  • ● Asiwe amealikwa na mteja mwingine.

3. Je, nitachajiwa kwa kumualika rafiki?

Mialiko mitatu ya awali ndani ya siku ni BURE. Mteja atachajiwa TZS 20 tu kuanzia mwaliko wa 4 kwa siku.

4. Je, ni kiasi gani ninachopata kama Bonasi?

Mteja atapata Bonasi kwa kutoa mialiko hadi ngazi ya 4. Bonasi inatokana na bei ya kifurushi alichonunua mteja (aliealikwa)
Tier/Ngazi Ngazi Zawadi Kwa A
1st B- (Aliyealikwa na A) 10%
2nd C- (Aliyealikwa na B) 5%
3rd D- (Aliyealikwa na C) 2.5%
4th E- (Aliyealikwa na D) 2.5%

5. Je, ni muda gani ambao nitaacha kupokea Bonasi?

  • Baada ya mwaliko kufanikiwa na rafiki kutonunua Pindua Bando ndani ya siku 7, mwaliko unaisha na hutapata Bonasi akinunua bando tena.
  • Bando yako ikiisha, mialiko yako pia itaisha ndani ya siku 3 kama hujanunua bando ya Pindua. Kuendelea kupokea Bonasi usiache kujiunga na Pindua Pindua.
  • Bando ya VODA MTONYO ya rafiki inapoisha, mialiko yako kwake itaisha siku 3 bila kujiunga na Mtonyo Bando. Ili kuendelea kupata Bonasi, rafiki yako anapaswa kuendelea kununua Mtonyo bando.

6. Je, napataje Bonasi yangu?

Mteja atapata Bonasi papo hapo kupitia akaunti yake ya M-PESA baada ya rafiki kujiunga na Bando ya VODA MTONYO..
Mteja anapaswa kuwa na akaunti ya M-PESA ili kupokea Bonasi.

7. Je, naonaje idadi ya marafiki niliowaalika?

Unaweza kuona idadi ya watu uliowaalika na idadi ya marafiki walioalikwa nao pia kwa kupiga
*149*03# kisha 3. Voda Mtonyo > 3. Taarifa > 4. Mtandao wangu
Mfano
Mtandao wa marafiki zako
Ngazi ya 1 (10%) = watu 100
Ngazi ya 2 (5%) = watu 1000
Ngazi ya 3 (2.5%)= watu 450
Ngazi ya 4 (2.5%) = watu 25

Voda Mtonyo - Vigezo na Masharti

Vigezo na Masharti

1. Mteja wa malipo ya awali akiwa na Pindua bando au akinunua Pindua kwa siku 3, anaweza mualika rafiki kujiunga na VODA MTONYO bando na kupata Bonasi watakapojiunga.

2. mwaliko kwa rafiki utaisha kama rafiki hatojiunga na bando ndani ya siku 7 baada ya kupokea mwaliko. Mteja atamualika tena rafiki kununua ili kupata Bonasi kutokana na kujiunga bando baada ya mwaliko.

3. Bonasi ya Voda Mtonyo italipwa kwa viwango vilicyoainishwa tu.

4. Mteja atapata Bonasi papo hapo katika M-Pesa Akaunti.

5. Mialiko mitatu ya mwanzo ni BURE, baada ya hapo kila mwaliko utatozwa 20 Tsh/sms

6. Rafiki atapokea mwaliko ukiwa na namba ya utambulisho kama Voda Mtonyo.

7. VODA MTONYO itapatikana kupitia Voda Mtonyo Menu kupitia *149*03# kisha chagua 3

8. Mara rafiki atakaponunua, atalazimika kujiunga na kutumia Pindua mara kwa mara ili alyemwalika aendelee kupata Bonasi. Vivyo hivyo waalikwa wanapaswa kuendelea kutumia Pindua ili waendelee kupata Bonasi.

9. Vodacom (T) PLC ina haki ya kufanya mabadiliko ya vigezo na masharti au kusitisha huduma hii wakati wowote. Litokeapo lolote kati ya haya, tangazo litatolewa mara moja au katika tarehe maalumu itakayotangazwa.

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa