Huduma Binafsi

1.Aplikesheni ya Vodacom ni nini?

Ni programu ya Vodacom inayomuwezesha mteja wa malipo kablakuwa na usimamizi/ udhibiti wa matumizi ya Intaneti, muda wa maongezi, salio kwenye simu yake

2.Je vitu gani mteja atavipata kwenye Aplikesheni ya Vodacom?

 • Kwenye Home screen:Mteja atakaribishwa kwa jina na namba yake ya simu, ubao wa salio la muda wa maongezi na salio la vifurushi,kuongeza salio na vifurushi, kubadili lugha n.k
 • Ongeza muda wa maongezi: hapa mteja ataweza kuongeza muda wa maongezi kwa kutumia vocha au M-Pesa kwenda kwenye namba yake au ya rafiki au namba nyingine ya Vodacom
 • Nunua Vifurushi: hapa mteja ataweza kununua Vifurushi avipendavyo kwenda kwenye namba yake au ya rafiki au namba nyingine ya Vodacom kwa kutumia salio la muda wa maongezi au M-Pesa..
 • Salio la muda wa maongezi au vifurushi: mteja ataweza kuangalia salio la muda wa maongezi au salio la jumla la Vifurushi. Pia mteja anaweza kuangalia kwa kina maelezo ya salio la kila kifurushi.
 • Vuta chini Home screen ya simu yako kupata salio jipyali>
 • fAngali maelezo binafsi: mteja ataweza kuona maelezo juu ya usajili ( Jina na namba ya simu) pamoja na kama amekamilisha usajili
 • gMsaada: hapa mteja ataweza kutafuta Vodashop ilio karibu

3.Nawezaje kupakua Aplikesheni ya Vodacom?

Mteja anaweza kupakua Aplikesheni ya Vodacom kupitia stoo ya Google au Apple kutegemea aina ya simu anayotumia (mfano simu za Android zitapakua Aplikesheni kutoka stoo ya Google na simu za IOS/Apple zitapakua kutoka stoo ya Apple)

4.Je Aplikesheni ya Vodacom inakubali mfumo gani wa simu?

Aplikesheni yaVodacom inakubali simu zenye mfumo wa Android (toleo la 5.0 au zaidi) na IOS ( toleo la 8.0 au zaidi)

5.Je mteja atumie njia gani kujua mfumo wa simu yake?

Kwa watumiaji wa mfumo wa Android : Nenda Settings  About  Version

Kwa watumiaji wa mfumo wa IOS: Nenda Settings  General  About  Version

6.Je ni mteja atafuata taratibu zipi kuanza matumizi ya Aplikesheni ya Vodacom?

Mteja atatakiwa kupakua na kuweka Aplikesheni ya Vodacom kwenye simu yake na kufungua kuanza matumizi

7.Je kuna malipo yoyote kwenye matumizi ya Aplikesheni ya Vodacom?

Matumizi ya Aplikesheni ya Vodacom ni BURE kwa wateja wa Vodacom

8.Je wateja wote wa Vodacom wanaweza kutumia Aplikesheni ya Vodacom?

Wateja wote wa Vodacom wanaweza kutumia Aplikesheni ya Vodacom.

9.Je mteja anaweza kubadili lugha ya namba yake kwa kutumia Aplikesheni ya Vodacom?

Mteja anaweza kubadili lugha ya namba yake kupitia Aplikesheni ya Vodacom.

10.Je ni hatua gani mteja anatakiwa kufanya akipata tatizo kwenye Aplikesheni ya Vodacom?

 • Zima simu yako na usubiri sekunde 5 kisha uiwashe tena. Baada ya hapo fungua tena Aplikesheni ya Vodacom.
 • Kama tatizo likiendelea iondoe Aplikesheni kwenye simu yako kwa kuibonyeza kwa muda kisha fuata maelekezo
 • Ondoa Aplikesheni na kisha iweke tena kupitia Google playstore kwa watumiaji wa simu za android au Apple store kwa watumiaji wa simu za IOS. Kisha fungua App kujaribu tena
 • Launch the app and retest the issue.
 • • Kama tatizo likiendelea , kusanya taarifa zote muhimu za mteja na simu kisha peleka idara inayohusika kwa uchunguzi zaidi:
Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa