KUHUSU SISI

Vodacom Tanzania Foundation - Connecting for Good

Taasisi ya Vodacom ya Jamii imesaidia wanawake na wasichana nchini kote kuboresha afya zao, upatikanaji wa elimu bora na kujenga makampuni mapya kwenye nyanzo za kujiajiri. Kufanya kazi na mashirika yasiyo ya kiserikali na washirika, Taasisi ya Vodacom ya Jamii imesaidia miradi zaidi ya 120 hadi leo na kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni 14 ili kuboresha maisha ya waTanzania.

Kutoka kupambana na kukomesha fistula ya uzazi hadi kuwawezesha wanawake katika maeneo ya vijijini kwaajili ya kuwa huru kujitegemea kwa mara ya kwanza, kuanzisha jumuiya ya afya ya kwanza ya malaria na kuelimisha wasichana wadogo kuhusu mazingira safi na usafi, Taasisi ya Vodacom ya Jamii imeendelea kuweka tofauti.

Miongoni mwa miradi yetu, tunajivunia hasa kuwa tumesaidia zaidi ya wanawake 2,000 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa uzazi wa fistula kwa ushirikiano na CCBRT; kujenga madarsa 34 nchini kote na kuwapa madawati 1,035, kutoa na kuunganisha kompyuta zaidi ya 300 katika shule za sekondari na kusaidia wanawake 7,931 wenye mikopo isiyo na riba kwenye miradi yao mbalimbali ya biashara.

Kutumia teknolojia ya simu, Taasisi ya Vodacom ya Jamii imesaidia kufumbua matatizo mbalimbali ya muda mrefu.

Wafanyakazi wa Vodacom ni sehemu muhimu ya kile tunachofanya kwenye misingi ya Vodacom ya jamii ikiwemo kuwahimiza kutoa muda na nyenzo mbalimbali zilizo ndani ya uwezo wao kusaidia matatizo yalio karibu nao.

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa