Tuzo pointi

Kwa nini uchague Vodacom kwa Tuzo pointi?

Mtandao bora
kwa Smatifoni yako

Mtandao wa
4G yenye kasi zaidi

Gharama Nafuu
Tuzo pointi

Ni Rahisi na haraka
kwa kununua Tuzo pointi

Tuzo Points

  • Tuzo Pointi
  • Napataje Tuzo pointi?
  • Komboa Tuzo pointi
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Vigezo na Masharti

Tuzo Pointi

Tuzo Pointi ni nini?

Tuzo Pointi ni programu ya Loyalty inayowawezesha wateja wa Vodacom kupata TUZO Pointi kila wanapoongeza salio kwenye simu zao na wanapotumia huduma za M-Pesa zenye makato.

Napataje Tuzo pointi?

Komboa Tuzo Pointi

Maswali Yaulizwayo mara kwa mara

1. TUZO Pointi ni nini?

Hii ni huduma inayowawezesha wateja wa Vodacom (malipo ya kabla/ Baada/uhuru {Hybrid}) kupata TUZO pointi kadri anavyoweka salio kwenye simu yake.

2. Mteja anapataje TUZO pointi?

Malipo ya kabla-Wateja hawa wataweza kujipatia pointi mara tu wanapoongeza salioUhuru-Wateja hawa watapata TUZO pointi mara wanapoongeza salio kwenye akaunti zao za malipo ya kabla

3. Ninapoongeza salio nitapata TUZO Pointi ngapi?

Mchanganuo wa pointi ni kama ifuatavyo:
  Kiwango cha kuongeza salio(TZS) Pointi unazopata
Unapoongeza salio 500 50
1,000 100
2,000 200
5,000 500
10,000 1,000

  Makato ya M-Pesa (TZS) Pointi unazopata
Makato yanayotokana na miamala ya M-PESA 500 13
1,000 25
2,000 50
5,000 125
10,000 250

4. Natumiaje TUZO pointi zangu?

wateja wanaweza kukomboa Tuzo pointi zao kwa njia zifuatazo,
  • a. Kubadilisha pointi kwenda kwenye salio la M-Pesa(makato ni 5%)
  • b. Komboa kutumia "Lipa Kwa pointi" kwa wakala yoyote wa M-Pesa (Makato ni 5%) **Mteja atapiga *149*01#>TUZO>TUZO POINTI>Komboa Pointi>(Nunua Kifurushi/Lipa kwa pointi/Badili kwenda M-Pesa)
  • c. Kununua vifurushi.
Vifuatavyo ni vifurushi ambavyo mteja anaweza kununua kwa kutumia TUZO pointi:
# Faida Muda Gharama (Pointi)
1 Dakika 7 (Voda-Voda) + SMS 20 (Mitandao yote) Saa 24 1,725
2 Dakika 15 (Voda-Voda) + SMS 20 (Mitandao yote) Saa 24 3,450
3 70 MB Saa 24 3,450
4 200 MB Saa 24 7,000

5. Je nawezaje kuangalia salio la pointi zangu?

Kuangalia salio piga *149*01# kisha chagua TUZO kisha TUZO points.

6. Ni kwa muda gani naweza kutunza pointi zangu? Je pointi zangu zinaweza kuisha muda wake?

TUZO pointi zinadumu kwa muda wa miezi 12 kutoka kipindi umezipata.Kama pointi hazijatumika ndani ya miezi 12 zitaondolewa kwenye akaunti ya mteja.Pia kama mteja hajatumia mtandao kwa muda wa siku 30 atapoteza pointi zote alizozikusanya.

7. Je kuna ukomo wa kiwango cha mteja kukusanya pointi?

Hakuna kikomo cha kukusanya pointi, bali pointi zisipotumika ndani ya kipindi cha miezi 12 zitakwisha muda wake.

8. Je nikiongeza salio zaidi ya shilingi elfu 10000 napata pointi ngapi?

Kwa kila Shilingi 10 unayoongeza salio utapata pointi 1Mf: Salio la Shilingi 12,000= TUZO Pointi 1,200.

Terms and conditions

Tuzo Pointi ni nini?

Tuzo Pointi ni programu ya Loyalty inayowawezesha wateja wa Vodacom kupata TUZO Pointi kila wanapoongeza salio kwenye simu zao na wanapotumia huduma za M-Pesa zenye makato.

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa