• Utangulizi
  • Faida
  • Dashbodi
  • Gharama
  • Usajili

Utangulizi

Shule nyingi nchini Tanzania bado zinafanya kazi chini ya utaratibu wa makaratasi, bila kuwa na mifumo ya kisasa kuwawezesha kusimamia shughuli zao za kiutawala na kitaaluma. Pamoja na hayo bado wazazi na walezi wanasumbuka wakati wa kufanya malipo ya ada na huduma nyinginezo za shule kwasababu inawabidi waende benki kufanya malipo kisha wapeleke risiti za benki shule kwa ajili ya uthibitisho wa malipo, mfumo huu unachukua muda mrefu ambao hupoteza muda wa wazazi na walezi kufanya shuhuli nyinginezo.

Kutokana na hayo, shule nyingi hukabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile ufanisi mdogo wa Shughuli zao, usimamizi duni wa taarifa za kiofisi, historia zisizo sawa za kitaaluma za Wanafunzi na cha zaidi ni ukusanyaji duni wa mapato ya shule ambavyo hupelekea Utendaji kazi na ufanisi wa kitaaluma kushuka. .

Ili kuhakikisha changamoto zote zinashughulikiwa, Vodacom M-Pesa imewaletea VODASHULE, ili kurahisisha shughuli za shule, malipo na mawasiliano kati ya wazazi, walimu, na wadau mbalimbali wa shule kiujumla.


VodaShule ni nini?

Vodashule ni mfumo rafiki na mahususi kwa ajili ya kurahisisha uendeshaji wa shughuli za shule, huduma hii imeletwa na Vodacom kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kiutendaji za mashule, kurahisisha mawasiliano baina ya uongozi wa shule, walimu na wazazi pia kuwawezesha wazazi na walezi kukamilisha malipo ya ada na gharama nyingine za shule kupitia simu zao za mkononi, Hivyo kupelekea uendeshaji bora wa shughuli za kielimu Tanzania.

Suluhisho hili linasaidia kuwezesha na kurahisisha michakato ambayo kwa kawaida huonekana kama migumu, kwa kutumia teknolojia hii ambayo inawapa wadau wa elimu uwazi zaidi na udhibiti na hivyo huhakikisha kuwa mfumo wa elimu unafanikiwa kwa pande zote zinazohusika.


Faida

Faida za Vodashule

Faida kwa Shule.

Vodashule hutoa faida nyingi kwa shule kwa kuzisaidia kurahisisha mambo muhimu ya mfumo wa usimamizi wa shule kama;

Kitaaluma

Vodashule ni huduma inayoziwezesha shule kuendesha shughuli za kitaaluma kwa usalama, urahisi na uhakika zaidi. Shule zinaweza kurekodi taarifa zote za wanafunzi ikiwemo mahudhurio ya wanafunzi, Ratiba za mitihani na matokeo, ratiba za masomo darasani n.k. Mzazi au mlezi atazipata taarifa zote za mwanafunzi kwa wakati kupitia aplikesheni ya VodaShule kwenye simu yake.

Kifedha

Vodashule ni mfumo wa kipekee unaoziwezesha shule kusimamia shughuli zote za kifedha kwa urahisi. Shule zitaweza kuona malipo yote ya ada na gharama zote za shule kutoka kwa wazazi au walezi papohapo pia wanaweza kulipa mishahara, kuwalipa wafanyabiashara wanaowauzia bidhaa na huduma, pia wataweza kuhamisha fedha zao benki wakati wowote. Haina haja ya kumtumia mzazi barua kuonyesha kiasi gani anachotakiwa kulipa, kupitia vodashule mzazi ataweza kuona kiasi gani ameshalipa na kiasi gani anatakiwa kulipa. Yote hayo yanarahisisha usimamizi salama na bora wa fedha za shule hivyo kufungua wigo wa huduma nyingine za kifedha kwa mashule kama MIKOPO, BIMA n.k.

Shughuli za uendeshaji:

Shughuli zote za kiutawala na uendeshaji wa shule zimeunganishwa ndani ya mfumo wa VodaShule ili kurahisha usimamizi bora na uendeshaji wa shughuli zote za shule kwa ufanisi zaidi. Shughuli kama usimamiaji wa magari ya shule na mali nyinginezo za shule vyote vimeunganishwa na Vodashule. Ufuatiliaji wa magari ya shule kwa GPS, Udhibiti wa kasi na utambuzi wa vihatarishi hufanyika kwa ufanisi zaidi kupitia VodaShule.

Faida za Wazazi/walezi na Walimu.

Kwa kuzingatia uhalisia wa maisha ya sasa, wazazi hawapati muda wa kutosha kufuatilia mambo ya kila siku ya watoto wao wanapokuwa mashuleni, kutokana na shughuli nyingi za wazazi zinazowapa ugumu wa hata kwenda benki kulipa ada za shule. Lakini kupitia Vodashule wazazi na walezi wamewezeshwa kufanya malipo ya ada za shule wakati wowote na mahali popote kupitia simu zao. Vile vile wanaweza kupata taarifa kuhusu maendeleo ya shule ya watoto wao kupitia aplikesheni ya Vodashule kwenye simu zao wakati wote.

Aplikeshe ya vodashule inawaleta pamoja walimu na wazazi; Mwalimu anaweza kuwasiliana na mzazi/mlezi wa mwanafunzi wake wakati wowote, Pia mwalimu anaweza kuwasiliana na walimu wenzake, wafanyakazi wengine na uongozi wa shule kwa ujumla. Kupitia aplikesheni hii mwalimu anaweza kuweka mazoezi ya darasani, matokeo ya mitihani, kutoa taarifa za vikao, mahudhurio ya mwanafunzi na taarifa nyinginezo.

Faida za Vodashule App kwa wazazi/walezi na walimu:

Urahisi wa Matumizi Upatikanaji Rahisi Inaokoa Muda
Kila mzazi ataweza
kuona taarifa za mtoto
wake kama matokeo,
ratiba za masomo na
mtihani n.k.
Wazazi na walimu wanaweza kuitumia aplikesheni hii muda wowote, kama kulipa ada na gharama za shule kupitia simu zao za mkononi. Walimu na wazazi wanaweza kuweka taarifa za wanafunzi kwa haraka zaidi.
Pia wanaweza kuona kumbukumbu zote za malipo ya ada kupitia aplikesheni ya Vodashule. Hakuna haja ya kusubiri vikao vya wazazi na walimu ili kupeana taarifa za maendeleo ya wanafunzi na mipango ya maendeleo ya shule. Vodashule inarahisisha mawasiliano baina ya wazazi na shule kiujumla.

Wazazi, walezi na walimu wanaweza kupakua Vodashule App kutoka Google Play store au Appstore..


Faida kwa Wanafunzi.

Mawasiliano bora baina ya mzazi/mlezi na mwalimu/shule humpa nafasi mwanafunzi kuweka umakini zaidi kwenye elimu yake na shughuli nyingine za kielimu hivyo kuongeza ufanisi wake kitaaluma. Kupitia Vodashule mwanafunzi hatosumbuliwa na barua au taarifa nyinginezo zitakazo msumbua kisaikolojia au kumpotezea muda wake ambao angeutumia katika shughuli nyingine za shuleni.

Dashbodi

Vodashule Dashbodi

Vodashule dashbodi ni sehemu inayo wakutanisha viongozi wa shule na wadau wake ili kupata taarifa na ripoti mbalimbali zinazohusu shule kwa urahisi zaidi. Dashbodi hii imeandalika kwa namna ambayo itamfanya kila mtumiaji kuona taarifa zinazo muhusu yeye mwenyewe kwa mfano Dashbodi ya Mkuu wa shule ni tofauti na ya mwalimu wa hesabu ambayo pia dashbodi yake ni tofauti na ya mhasibu wa shule ambayo pia dashbodi yake haifanani na ya msimamizi wa wanafunzi. Hivyo kufanya Vodashule kuwa huduma yenye usalama na usimamizi mzuri wa shughuli za kituendaji kwa shule kiujumla.

Gharama

Gharama za huduma.

Mashule hayatatozwa gharama za kutumia huduma hii. Vodacom itawatoza wazazi kiasi cha kawaida kwa kufanya muamala wa kulipa ada na gharama nyingine za shule. Mbali na hiyo, huduma nyingine zote zinazopatikana ndani ya Vodashule ni bure (mfano kuangalia matokeo ya mwanafunzi, ratiba za masomo, ratiba za mitihani, mahudhurio ya darasani ya mwanafunzi na taarifa nyinginezo za mwanafunzi)

Usajili

Kujisajili na Vodashule

Shule zote Tanzania zinakaribishwa kujiunga na huduma hii ya Vodashule ili kunufaika na huduma zilizoko ndani ya mfumo huu wa kielimu. Shule zote za binafsi na Umma kuanzia shule za msingi, sekondari na taasisi za elimu ya juu zinaweza kutumia VodaShule na kufanya shughuli zao za kitaaluma, kiutendaji na kifedha kwa njia ya kidigitali. Ili kujiandikisha Vodashule, Shule inahitajika kuwa shule iliyoidhinishwa na mamlaka husika za elimu nchini Tanzania.

Tembelea VODASHULE PORTAL ili kuisajili shule yako ndani ya mfumo wa Vodashule.

Baada ya kujisajili, timu ya mauzo ya Vodacom itawasiliana na wewe ili kukufuata kukamilisha usajili wa shule na kutoa elimu kuhusu huduma hii na jinsi ya kuitumia, mafunzo hayo yatatolewa kwa shule kiujumla ikiwemo walimu na wahusika wote katika uendeshaji wa shule yako. Baada ya kutoa mafunzo ya jinsi ya kutumia huduma ya Vodashule, timu itawakabidhi vipeperushi vya muongozo wa matumizi pamoja na vipeperushi vinginevyo ili kurahisisha utumiaji wa Vodashule. Kwa upande mwingine Vodacom tunafanya kampeni ya kuongeza uelewa kuhusu Vodashule na pia kuelimisha wazazi/walezi kuhusu umuhimu wa aplikesheni ya Vodashule.


Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa