VPL Updates

TFF Yatoa Tamko Kuhusu Tuhuma za Kabwili kwa Simba

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeiagiza kamati yake ya maadili kufuatilia ukweli kuhusu tuhuma za upangaji matokeo zilizotolewa na golikipa wa Yanga, Ramadhan Kabwili. TFF pia imesema itavijulisha vyombo vingine vya usalama ili visaidie uchunguzi na kuchukua hatua stahiki.

Akizungumza na moja ya vyombo vya habari hapa nchini hivi karibuni, katika mahojiano yake, Kabwili alisema; “Simba waliwahi kunifuata kipindi tupo na kocha Zahera, nilikuwa na kadi mbili za njano na kwenye mchezo wa Yanga na JKT Tanzania, walitaka nitafute kadi ya njano makusudi ili wanipe gari ya IST mpya na nikose mchezo ujao wa watani,” Ramadhan Kabwili.

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa