Kuhusu Vodacom

Kuenea kwa mtandao nchini

Vodacom Tanzania imejiwekeza kwenye sanaa ya teknolojia, na hivyo kuimarisha bidhaa zake na hivyo kuwa kiongozi kwenye soko la mawasiliano, kwa sauti, intaneti, laini za kukodishwa, uunganishaji wa PABX, uunganishaji wa kimataifa, ufumbuzi wa WiMAX, ufumbuzi wa mawasiliano mbali mbali juu ya satelaiti au benki, Vodacom Tanzania inatatua mahitaji yote.

Teknolojia zinazopatikana kwa wateja wake, watu binafsi na shirika mbalimbali kupitia Vodacom Tanzania ni pamoja na:

  • GSM 900/1800 nchini kote kufikia asilimia 75.82% ya wakazi wote.
  • GPRS nchini kote kufikia asilimia 75.82% ya wakazi wote.
  • EDGE kupatikana katika baadhi ya miji na jiji yenye idadi ya wakazi asilimia 50%.
  • 3G na HSDPA kupatikana Dar es Salaam, Arusha, Moshi, Mwanza, Mbeya, Bukoba, Kahama, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Namanga, Tanga, Dodoma, Morogoro, Makambako, Mbeya, Tunduma, Lindi, Mtwara na Masasi.
  • WiMAX 802.16d kupatikana katika miji mikubwa miwili inayofunika asilimia 70% ya majengo ya biashara.

Ushindani kwenye mawasiliano umeongezeka kwa kasi kubwa miaka michache iliyopita Tanzania. Mbali na ubora, kupatikana kwa mawasiliano kwa urahisi inabakia sehemu muhimu kwenye ushindani

Hakimiliki © 2018 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa