Kuhusu Vodacom

Matukio muhimu ya uendeshaji

Mnamo Desemba 1999, Vodacom Group (Pty) Ltd. ilishinda zabuni ya kuendesha mtandao wa simu za mkononi za GSM kwaajili ya kutoa Public Land Mobile Network Services (PLMN) katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ilianzisha tawi jipya linaloitwa Vodacom Tanzania Limited.

Mnamo Julai 2000, Vodacom Tanzania ilikamilisha ujenzi wa miundombinu ya GSM na ikaanza rasmi kutoa huduma kwa wateja tarehe Agosti 14, 2000. Ndani ya miezi minne ya kwanza wateja 50,000 waliunganishwa.

Mnamo Septemba 2004, Vodacom iliunganisha zaidi ya wateja milioni moja na kuendelea kukua kwa kasi. Mnamo Septemba 2005, Serikali ya Tanzania ilianzisha mfumo wa kutoa leseni, ambao ulikuwa na nia ya kuimarisha utoaji wa huduma za mawasiliano nchini na hivyo kuleta dhana halisi ya teknolojia.

Kama kiongozi katika soko la mawasiliano ya simu, Februari 2006, Vodacom Tanzania ilifanya maamuzi ya kujadili mabadiliko ya leseni yake ya awali PLMN kwenda katika mfumo mpya wa leseni.

Mnamo Machi 2006, Vodacom Tanzania, ili weka rekodi ya wateja milioni mbili. Mnamo Julai 2006, Vodacom Tanzania ilipewa leseni kuu tatu za huduma katika Sekta ya Mawasiliano ambazo ni, Leseni ya Vifaa vya Mtandao, Leseni ya Huduma za Mtandao na Huduma za Maombi, kutoka mamlaka kwaajili ya kutoa huduma mbalimbali za mawasiliano kwa njia ya sauti na intaneti kitaifa na kimataifa.

Hii ilifungua zama mpya kuongeza kasi ya uwekezaji na utoaji wa huduma bora za mawasiliano kwa Watanzania. Mnamo Januari 2007, Vodacom ilifanikisha kuunganisha wateja zaidi ya milioni tatu, na kuwa mtandao wa kwanza wa simu nchini Tanzania kurekodi namba kubwa ya wateja. Leo, miaka 10 baadaye tuna wateja zaidi ya milioni 10 na bado tunaendelea kukua kwa kasi.

Vodacom Tanzania ni tawi la Vodacom Group (Pty) Limited, Afrika Kusini ambayo pia ni tawi la Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) Limited inamiliki sehemu kubwa kiasi cha asilimia 65% na asilimia 35% iliyobaki inamilikiwa na mbia wa Tanzania, moja Mirambo Ltd.

Vodacom Tanzania ni tawi la Vodacom Group (Pty) Limited, Afrika Kusini ambayo pia ni tawi la Vodafone Group UK. Vodacom Group (Pty) Limited inamiliki sehemu kubwa kiasi cha asilimia 65 na asilimia 35 iliyobaki inamilikiwa na mbia wa Tanzania, moja Mirambo Ltd.

Hakimiliki © 2020 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa