Kuhusu Vodacom

Vodacom Biashara

Vodacom Tanzania ni zaidi ya kampuni ya simu za mkononi, kwa miaka iliyopita imekuwa ikitoa fumbuzi mbalimbali za huduma kwa wateja. Ili kuweza kuendelea kutimiza lengo hili na kukuza mahitaji ya kampuni mbalimbali hivi karibuni Vodacom imeanzisha kitengo maalum Vodacom Biashara.

Vodacom Biashara inaongoza kwa kutoa fumbuzi mbalimbali kwenye mawasiliano zinazokidhi mahitaji ya wateja, zinazoendeshwa kiteknolojia, kwa gharama nafuu, na kwa ubunifu katika thamani ya hali ya juu. Wateja wa Vodacom sasa wanaweza kukidhi mahitaji yao yote ya mawasiliano kupitia mtandao wa intaneti, aplikesheni za ndani kwa mtoa huduma mmoja.

Kupitia hiki kitengo, Vodacom inatoa teknolojia iliyojitosheleza na kamili yenye fumbuzi mbalimbali za intaneti kusaidia mashirika makubwa kwa madogo kutimiza mahitaji yao kundelea kushindana kwenye ulimwengu wakijiji

Vodacom Biashara pia inatoa huduma zilizojitosheleza za aplikesheni za ndani ukijumuisha za kawaida na maalumu kwaajili ya aplikesheni muhimu na hifadhi za nakala pamoja na za ziada na urejesho wa huduma kutoka kwenye maafa mbalimbali. Huduma za Usalama zinajumuisha vizuizi vya kuingia kwenye kompyuta, barua pepe na uchujaji wa mahudhui ya tovuti na kupambana na matangazo ya biashara yasiofahamika. . Kujua zaidi kuhusu huduma zetu na jinsi ya kupata bofya hapa

Hakimiliki © 2018 Vodacom Tanzania. Haki zote zimehifadhiwa